Maisha ya Temeke: Uhuni, defender za polisi hadi kunusurika kuuawa kisa mwanamke

Maisha ya Temeke: Uhuni, defender za polisi hadi kunusurika kuuawa kisa mwanamke

Aisee wewe kweli umeishi Temeke, sisi watoto wa Kijitonyama miaka hiyo tulikuwa tukienda club billcanass watoto wa Temeke hatuwasogelei kabisa. Mwaka 2017 niliwakalisha wahuni watatu baada ya kumuibia simu mdada ambaye alishuka kwenye daldala Yombo dispensary. Kilichonikasirisha ni kwamba yule dada anapokonywa simu watu wametulia tu wanaangalia, medani na ukakamavu ulinisaidia, kizuri zaidi walitulia baada ya mshkaji wangu niliyemfuata mitaa ya kwao nikawa namsubiria kwenye kiglocery pembeni na kituo cha daladala ambaye ni mwanajeshi kutokea akawachana.
 
Aisee wewe kweli umeishi Temeke, sisi watoto wa Kijitonyama miaka hiyo tulikuwa tukienda club billcanass watoto wa Temeke hatuwasogelei kabisa. Mwaka 2017 niliwakalisha wahuni watatu baada ya kumuibia simu mdada ambaye alishuka kwenye daldala Yombo dispensary. Kilichonikasirisha ni kwamba yule dada anapokonywa simu watu wametulia tu wanaangalia, medani na ukakamavu ulinisaidia, kizuri zaidi walitulia baada ya mshkaji wangu niliyemfuata mitaa ya kwao nikawa namsubiria kwenye kiglocery pembeni na kituo cha daladala ambaye ni mwanajeshi kutokea akawachana.
Siku hizi usela mabinumepungua,mkuu.

Hata hayo matukio ya kuporana mchana kweupe yamepungua sana,wahuni wanavizia usiku.

Ulifanya kitendo cha kishujaa sana kumpambania huyo sister.
 
Siku hizi usela mabinumepungua,mkuu.

Hata hayo matukio ya kuporana mchana kweupe yamepungua sana,wahuni wanavizia usiku.

Ulifanya kitendo cha kishujaa sana kumpambania huyo sister.
Alinishukuru sana kwakweli ilibidi abaki na mimi mpaka wenyeji wake walipokuja kumchukua maana aliogopa sana kuendelea na safari peke yake.
 
Kwa mtazamo wako, Afande Tyson angetoboa kwa Ustadhi?.
Ostadhi yupo vizuri,ila kusema Tyson angetoboa au asingetoboa hapa Sina jibu.

Kwa sababu nilichokiona ni watu kuwa na phobia/woga tu juu ya huyu afande ila wengi hatukuwahi kumuona akipambana mapambano halisi na mtu mwenye ujuzi wa mapigano.

Asilimia kubwa ya stori za afande Tyson ni kama yule dogo wa Arusha dangote kwamba ni mtu hatari kiasi watu wazima na midevu wakimuona wanatetemeka na wanabadilisha Njia,ila siku walipomchoka walimsaga kama nyanya. Woga mbaya sana,alafu ukijumlisha na stori za hear and say ndiyo unaingiwa na ubaridi balaa.

Wabongo tuna asili ya ukunguru...Ni waoga balaa,ndiyo maana hata mtu anayepiga gym akajaza mwili anaweza kukuchapia mkeo live na ukamwangalia kumbe fala tu aliyetunisha misuli.

Kwa hiyo hapa nampa benefit of doubt ostadhi kwa sababu namjua alikuwa vizuri kimedani.
 
Alinishukuru sana kwakweli ilibidi abaki na mimi mpaka wenyeji wake walipokuja kumchukua maana aliogopa sana kuendelea na safari peke yake.
Safi,mkuu. Hivi ndiyo inapaswa kuwa mtu ukiwa mtaalamu wa mapigano...kusaidia walio dhaifu.

siyo kupigana pigana hovyo mwenye maana kugombania wanawake.
 
Safi,mkuu. Hivi ndiyo inapaswa kuwa mtu ukiwa mtaalamu wa mapigano...kusaidia walio dhaifu.

siyo kupigana pigana hovyo mwenye maana kugombania wanawake.
Upo sahihi self defence iwe pamoja na kusaidia wanyonge wenye haki. Naoemdaga sana nikute mtu anamuonea mwenzake alafu mbishi, huyo huwa naadhibu kwa kiasi cha mwadhibiwa kujutia ujinga wake alafu nampeleka mbele kwa amri labda aombe msamaha kwa aliyekuwa akimuonea na muonewaji akaridhia.
 
Masela walipita na saa yangu CASIO Mwembeyanga, nimetoka zangu home Gerezani Kkoo, nikasema niende kwa uncle mitaa hiyo. Kufika Mwembeyanga nikasema niangalie mpira kidogo. Nikajisahau kidogo nikaweka mikono nyuma, msela alipita nayo kama kipanga.
 
Siku hizi usela mabinumepungua,mkuu.

Hata hayo matukio ya kuporana mchana kweupe yamepungua sana,wahuni wanavizia usiku.

Ulifanya kitendo cha kishujaa sana kumpambania huyo sister.
Mambo ya macamp camp yalivyoisha na uhuni uhuni nao ukaisha kwa kiasi kikubwa... Vijana waliokulia, temeke, mbagara, mwananyamala, tandale, magomeni, kinondoni baadhi ya maeneo wanaelewa haya mambo.
 
Nilipoanza kupata Hela nikahama kutoka mitaa niliyokuwa naishi(nyumbani) kisha nikahamia mtoni mtongani,kule chini wanakuita mtaa wa ndekereko(ndengereko street).

Maisha yalikuwa yanaenda vizuri tu hakukuwa na tatizo.

Siku Moja jumapili nimeamka zangu,nilikuwa na ratiba ya kufua nguo. Nikaingia kokoni kwenda kufua mana hapakuwa mbali na nyumba niliyokuwa nakaa.

Kwa niliowaacha ninaposema “nilienda kufua kokoni” ni hivi; ukienda kigamboni ukawa unapita kwenye daraja la kigamboni “Nyerere bridge” ukiangalia upande wa kulia Kuna mkondo wa bahari unaelekea upande wa kusini. Kule mbele umegawanyika umetengeneza pacha,upande mmoja umeelekea mtoni kijichi(msende sema beach,hadi vikunai-magorofa ya nssf ukaja kuungana na mto mzinga/kongowe) na hapa na hii pacha nyingine kabla ya ile pacha ya mtoni kijichi ndiyo imekuja kutokea kurasini,kule nyuma ya makao ya Kanisa katoriki-TEC,Kijiji cha wavuvi na kutokea mtoni mtongani kisha huu mkondo ukaja kuungana na mto kizinga(ule wa kongowe unaitwa mto mzinga na huu wa mtongani karibu na daraja la treni pale chini unaitwa mto kizinga).

Sasa basi, kwenye hii mikondo bahari miwili(huu wa kijichi na huu unakuja mtongani Kuna misitu mikubwa ya mikoko na chini yake Huwa yanapita maji ya bahari kipindi cha bamvua(maji kuwa/maji kukaa in English “tides”) na Kuna siku za bamvua kule chini mtongani Kuna kiwanja cha mpira kunakuwa hakuchezeki maana maji ya bahari yanajaa kuanzia saa Tisa jioni uwanja wote.

Kwenye hii mikondo bahari Kuna(hasa mtongani Kuna chemchemi za maji ambazo zinatitirisha maji kuelekea baharini. Wenyeji wa maeneo haya wamechimba visima vidogo vidogo wanachota kwa ajili ya shughuli za bustani na kufulia nguo. Sasa haya maeneo ndiyo wenyeji huyaita “KOKONI”. Hapa nilikuwa natoa elimu ya geography kidogo ya jinsi haya maneno kuanzia daraja la kigamboni hadi kijichi/mtongani.

Let's stick into our lane.

Hiyo jumapili nikaweka nguo zangu kwenye ndoo na kusogeoa KOKONI kwenda kufua. Nilipomaliza nikardudi home kuandika nguo kisha kuzisubiri ili zikauke kisha niendele na misele mingine.

Maeneo ya uswahilini huwezi kufua nguo alafu ukasepa zako,ukirudi utakuta kamba tu,wahuni wameshapita nazo.

Wakati nasubiri nguo zikauke Huku nafanya maandalizi ya chai,ghafla simu ikaingia meseji nikaangalia nani ametuma meseji muda huo nikakuta text imeandikwa “oii Satoh Hirosh jioni twenzetu mitaa ya Temeke-Kichangani nataka tukamcheki shemeji yako”. Alikuwa Mwanangu Mzee wa bandari Y-lala. Nikamjibu “poa nimekusoma”.

Jioni ikafika,Y-lala akaja home akanikuta Bado sijajiandaa.

Y-lala: Mzee baba,saa 11 hii jioni hadi muda huu haujajiandaa wakati nilishakupanga kitambo?

Mimi: Mapema yote hii tunawahi nini,Mzee? Subiri jua lipoe poe. Kwanza kichanganj hapo siyo mbali.

Y-lala: sema jiandae kabisa,ili saa12 itukute kule,tuwahi kurudi. Tukichelewa kwenda tutachelewa pia kurudi.

Mimi: poa nimekusoma,Wacha nikaoge kabisa maana mzee ukitaka jambo lako!!? Ila kama una genye si umwite tu kwako badala ya kwenda kwao?

Y-lala: Hapana,Leo kasema hawezi Kuja,alafu we huchoki kushida home wakati ni weekend? Si tunafanya kama tunanyoosha viungo?

Mimi: poa umeshinda,Wacha nikamwage maji fasta.

Nikaingia ndani na kuzama bafuni kuoga.

Dakika kadhaa…sauti.

Oya mwanangu unaogesha scania pulling huko bafuni? Au unapiga nyeto*? Fasta basi Mzee tusepe. Mbona unaoga muda mrefu sana? Ilikuwa sauti ya Y-lala.

Y-lala alikuwa anapenda kunizingua sana ile kishkaji. Alafu yeye mwongeaji,ila Mimi siyo mwongeaji. Tulikutana introvert na extrovert.

Nilipotoka bafuni(lilikuwa bafu la nje,na yeye hakuwa mbali na hilo eneo) akaniangalia usoni wakati nataka kuingia ndani Huku anatabasamu akasema “sema mwanangu huko bafuni ulikuwa una kazi mbili,mbona macho mekundu?

Mimi: Sabuni iliingia machoni bana. Mbona umenikalia kooni,kaka? Mimi siyo kama wewe,Mimi mtoto wa Mungu. Nilimjibu Huku nazama ndani nacheka. Naye akacheka Huku anaongea ila sikumzingatia.

Baada ya dakika kadhaa nikatoka nje nikiwa tayari mimejiandaa kwa safari ya kwenda kichangani.

Y-lala : sema SH unapenda sana kutupia. Mbona umepania sana kuvaa?

Mimi: sasa unataka twende kutembea tukiwa kama tunaenda kuomba kazi viwandani kwa wachina,kaka? Alafu umesahahu sisi ni wazee wa bandari. Mbona unapenda unyonge?

Y-lala: Poa twenzetu,sema tupitie home nikabadili viatu.

Wakati huo jamaa ananisifia nilikuwa nimevaa black jeans plain na fulana nyeupe plain pia,shingoni nimevaa rozari na kuuweka msalaba kwa ndani. Chini nilikuwa nimevaa buyu(American boot 🥾) Rangi nyeusi. Hili boot lipo hadi Leo hii naandika. Nimelihifadhi kama archive. Huwa nagawa viatu na nguoara kibao ila hii American boot Huwa siigawi mama Ina historia ndefu na Mimi.

Na kiukweli tangu nipo kachalii sana Mimi ni mtu ninayependa kuvaa. Na siyo kuvaa tu,Huwa napenda kuvaa vizuri. Ni muumini mkubwa wa ule msemo wa “dress well no matter what the occasion” na ile “never underestimate the power of dressing well”.

Nakumbuka miaka hiyo kwenye graduation ya darasa la Saba,sister alikuja kunitunza. Muda wa kufungua gift 🎁 nikakuta ameniwekea suruali na t-shirt. Nilipoziangalia tu nikasema kamwe siwezi kuvaa hii midosho. Si Bora sister angenipa Hela ninaenda mwenyewe kununua nguo kisha nimkabidhi aweke kwenye hii gift box!!? Ilipita kama mwezi hivi akaniuliza “mbona sijawahi kukuona umevaa hata siku Moja zawadi nilizokutunza?” Nikamjibu zile hazinitoshi kubwa,kumbe niligawa kwa mtoto wa mama mkubwa,ahahah.

Safari ya kuelekea kwa Y-lala kwenda kubadilisha viatu ikaanza…

Kisha tukaingia mtongani juu,tukavuka barabara ya kilwa na kuhamia upande wa pili kuanza kuitafuta kichangani karibu na kanisa la Roma kwa mrembo wake.

Baada ya dakika kadhaa tukafika kichangani.

Tukaonana na huyu bibie,akanichangamkia sana ile Shem mambo vipi,mara umependeza,unapenda kuwa kama mtu wa mbele Shem!! Huku anacheka.

Tuliposalimiana nikawapa nafasi ya kuongea wawili,kama unavyojua tena wapendanao.

Huwa Kuna sehemu wanakaa ambako hakuna watu wengi Wala wapita Njia,hapo wanaweza kukaa hata masaa mawili na Kuna muda wanafanya mambo yao ya ajabu mara wanyonyane mate kama unavyojua tena wapenzi wawili wakikaa pamoja ni utoto tu unaendelea.

Mimi nikasogea mbali kidogo Kuna kijiwe kimoja maarufu Huwa nawasubiri hapo. Hapa kwenye hiki kijiwe ni kijiwe cha wacheza pool table. Na boda boda Huwa wanashinda karibu na hapo kama kijiwe chao. Kwa kiasi Fulani washikaji wa hapa wananifahamu kwa sura na Mimi nawafahamu kwa sura maana karibia Kila mwezi Huwa tunakuja na Ylala kutembea hii mitaa ya kichangani na Mimi huweka jambo hapa kucheki pool table japo siyo mchezaji mzuri.

Sasa baada ya kama nusu saa kupita,GHAFLA nikasikia makelele kutoka upande ule alipo Y-lala na mwanamke wake. Sikujali maana hivi ni vitu vya kawaida uswahilini. Mara kelele zikazidi kiasi Kila mmoja pale kwenye pool table kupay attention nini kinaendelea upande ule.

Baada ya muda mtu mmoja mmoja akaanza kusogea upande ule. Na Mimi nikasema hapa hapaeleweki wazee wa kazi(polisi) wanaweza kuja wakati wowote,ngoja nikamcheki Y-lala tusepe zetu.

Ile nakaribia alipo Y-lala….lahaulaaa!!!

Mara nasikia “Tena ms*ng* mwenzie si huyu hapa sharo”. Nilipoangalia kwa umakini nikaona Y-lala yupo chini na demu wale akiwa amesimama lakini angalia. Nikiangalia zaidi ni kama jamaangu alikuwa amepigwa na Hawa wahuni hadi kupelekea kukaa chini. Kwa ufupi jamaa alikuwa ameshataitiwa na Hawa wahuni mama name hivi kwa hesabu za haraka haraka.

Wakati jamaa wananitolea matusi watu watatu wakawa wanakuja upande wangu Huku wamefura kwa hasira. Kwa kifupi walikuwa katika mkao wa kunifanya kitu chochote kibaya. Moyo ukaanza kwenda mbio kwa woga na mshangao maana nilikuwa sijui nini Y-lala amaefanya alafu mbaya zaidi jamaa wanakuja upande wangu Huku wamekunja ngumi na mmoja anakuja Huku anavua mkanda.

Nikasikia mwingine anasema “nyie maboya mnajikuta masharukh-khan siyo? Yani mnatoka huko mnakotoka mnakuja kutamba mtaani kwetu na kutuchukulia mademu zetu au siyo? Sasa leo ndiyo mtajua hapa mmekojoloea transformer. Unajua kwa walio kaa hood/mtaani wanaelewa maneno ya mtaani wahuni wanavyoongea. Huwa eanaongea kibabe kiasi kwamba mikwara yao hata angekuwa shetani asingethubutu kukaa..angekimbia.

Mapak hapa nikasema hapa nipo katika hatari. Napaswa kujiokoa na napaswa kumuokoa mwanangu Y-lala.

NIKAVUTA FOCUS..!!

Jamaa hawakujua enzi hizo nilikuwa mtu wa medani. Kung Fu nilikuwa naipiga vibaya mno. Wakataka kuniingia kichwa kichwa na jamaa aliyekuwa anachomoa mkanda alikuwa wa tatu kutoka nyuma ya Hawa wawili mbele ambao walishanikaribia…!

Nilichofanya nilikaa kwenye stance ya pigo kwa yule mtu wa nyuma ambaye nilimwona hatari zaidi. Niliwazunguka Hawa jamaa wa mbele kwa Kasi ya mwanga na kumfikia yule wa tatu ambaye tayari alikuwa ameshasokota ule mkanda wake na kubakiza eneo dogo na kile kipande cha bizm sijui mnaita(kile chuma cha kufungua mkanda,sina uhakika na jina lake). Katika ile speed kwa kutumia mguu wa kulia nilipiga mtama mzito(back low kick) jamaa akaanguka kama mfuko alafu nikashindilia na teke karibu na jicho(nitaeleza mbele kwa nini nimeelezea kwa ufasaha kiasi hiki). Jamaa akakata moto palepale. Alafu kumbuka chini nilikuwa nimevaa American boot…alooo!

Jamaa wawili kabla hawajajua nilichofanya na hawajapata muda wa kutafakari nikaruka flying kick Moja,mmoja akaenda chini na huyu mwingine chap nikamtembezea yoko gel.

Wale jamaa wengine kule kwa Y-lala Bado hawakusanuka mbele yao nimesimama mtu hatari Sana. Wanasema “aagh unajifanya mtata siyo” wakamwacha Y-lala wote sasa wakawa wanakuja kwangu. Nadhani kupitia hii chance ndiyo Y-lala alichomoka na kunitoroka maana kuanzia hapo sikumwona tena. Msala wote ukabaki kwangu. Y-lala hayupo,mwanamke wake hayupo.. Balaa zito!!

Jamaa baada ya kuona wenzao watatu hawainuki wakagwaya kunijia kindezi. Wakawa kama wananizunguka,alafu mmoja nikamwona kama ameshika kitu mkononi. Nikawaza Hawa wahuni hawakosi visu au vitu vyenye ncha Kali. Nisipoongeza focus na kumaliza mchezo ndani ya dakika 3 naweza kukutwa na jambo baya. Na nisipoangalia hapa nakufa…!

Nikakumbuka enzi zile najifunza kung Fu,sensei alinifundisha mambo kadhaa kuhusu kung Fu ambayo ni FOCUS, FLEXIBILITY,POWER na CONTROL. Nikasema hapa ndiyo nimeingia rasmi kwenye real battlefield.

Wale jamaa niliwapiga vibaya mno. Na kwa kuwa walikuwa wengi nilikuwa nawapiga zaidi mateke ya chini kwenye ugoko(shin kick &low kicks),wengine niliwapiga pigo la mawash geri ili wasiweze kuamka.

Jamaa walipoona wamezidiwa kwa vipigo na hali zao kuwa mbaya sana wakaanzs kupiga kelele za “mwiziiiii” huyu jamaa na mwezie ni wezi”. Wakati huo tayari watu walikuwa wameshajaa. Si unajua uswhilini. Watu kibao wametuzunguka.

Kuna ambao walikuwa wanataka kuingilia ili kwa kuanza kuvunja miti iliyo karibu kana mihogo,mawe nk ila Kuna sauti zingine miongoni mwao zilikuwa zinasema “huyu dogo siyo mwizi,acheni kwanza”.

Wakati huo nilikuwa nimeshahama kutoka kuwa mtu wa kawaida na kuwa kumbe wa ajabu. Yeyote anayeonekana mbele yangu na kunikaribia kwa namna yeyote,Hana bahati. Nilikuwa naipiga mapigo ya either uzimike au ukae chini usiinuke kabisa.


Wakati huo pale chini Kuna watu kadhaa wameshalala hawawezi kuamka na watu wakiwa wanazidi kujaa kutoka maeneo tofauti kiasi kwamba nikazidi kuogopa.

Kuna jamaa nikasikia sauti yake kutoka mbele yangu ambako nilikuwa nimeweka stance ya pigo akiniita “white tulia kwanza,imekuwaje mbona tulikuwa pale kwenye pool table? Imekuwaje?” Hapo ndiyo fahamu zikanijia na kuanza kurudi kuwa mtu wa kawaida. Isivyo bahati Mimi sijui kuongea. Hasa kwa speed au katika majibizano ya ana kwa ana ndiyo kabisa lazima nizidiwe kuongea.

Mimi: Nilikuwa na mshikaji wangu hapa kumcheki demu wake anaitwa Habiba(code). Sasa ghafla nikasikia sauti za kama mtu anapigwa wakati huo Mimi nipo kwenye pool table pale. Nilipokuja hapa na baadhi ya washikaji wa pale kwenye pool table kuangalia nini kinaendelea ndiyo nikaona Hawa jamaa wanakuja upande wangu na kuanza kuishambulia pasipo Mimi kujua sababu.

Jamaa aliyeniuliza swali: Ni kweli jamaa tulikuwa nae pale pool table,Oya nyie wa**** huyu dogo amewakosea nini hadi muanze kutaka kumpiga.

Jamaa mmoja pale chini: (Huku anaongea kwa maumivu makali Huku amejishika tumbo) Hawa madogo wezi **** zao.

Mwingine aliyesimama: wamewaibia nini?

Mdada: Nyie waongo,sema mmeona wivu Habiba kutembea na yule mkaka mwingine. We jumanne si umeshaachwa? Sasa mbona unazidi kumfata fata mwenzio?


Ghafla…! Watu wakaanzs kutawanyika Kila mmoja anakimbia kusikojulikana.

Kufumba na kufumbua…! Polisi Hawa hapa.

Wakatuweka chini ya ulinzi wote waliotukuta pale,wale jamaa wote hawakuweza kuinuka wakasombwa kama kuku na tukaingizwa kwenye defender kisha safari ya kuelekea ‘chang’ombe police post’ ikaanza.

Wakati huo tayari ilikuwa usiku kama saa mbili. Tukashuka police nakuingia ndani.

Afande: vua mkanda na kabidhi Kila kitu kwenye dawati kisha andikisha jina.


Mimi: Fasta nikatoa mkanda,kisha simu na wallet na kuunyonga mkanda ukawa kama jongoo aliyejisokota kisha nikaweka kwenye buyu(American boot niliyovaa) na wallet na simu nikaweka kiatu kingine.

Afande; Dogo una viatu vikali hivyo,hahahah. Ngoja wenzio kesho asubuhi wakiwa wanaenda mahakamani wakitoka wapite navyo. Hapo kubali umeshapoteza hivyo viatu(akacheka Tena kwa dharau)

Mimi: Afande naomba unihifadhie basi huko kwako.

Afande: Dogo unajaribu kunitumikisha? Yani nikuhifandhie matakataka yako Huku kwenye dawati. (Akanitukana)

Mimi: (nikachomoa 10k kwenye wallet na kuirudisha ndani ya kiatu). Afande nakuombea. Akaona nimeshika elfu Kumi akaichukua na kuvishika viatu akavihifandhi upande wao kwa chini Huku namwangalia kwa makini anapoweka.

Unajua American boot ni kiatu kikubwa sana(kina nafasi) kiasi kwamba ukihifadhi wallet na vitu vidogo vidogo vinakaa bila shida ndiyo maana nilipoweka vitu vyangu vilikaa vyote bila mtu kujua kama ndani Kuna vitu zaidi ya hivyo viatu vyenyewe. Afande akadhani ameweka viatu tu kumbe Kuna wallet yenye Hela kama 40k,simu na mkanda niliokukunja. Kumbuka nilipotoka na Ylala kwenda kutembea,kwenye wallet niliweka elfu 50. Kwa hiyo nikatoa elfu Kumi kumpa afande ili anihifadhie viatu vyangu sehemu salama maana pale kwenye viatu vingi ni kweli kesho nisingevikuta. Mtu akiruhusiwa tu anapita na viatu vyovyote anavyoviona vinamfaa.

Tukazama ndani.

Ilikuwa kama naota maana sikuwahi kudhani siku Moja ningekuja kulala sello. Kweli kwenye maisha hatuijui kesho yetu.

Upande wa pili Y-lala baada ya kukimbia alienda Moja kwa Moja Temeke mitaa ya home kutoa taarifa ya nini kimetokea. Fasta bro na yeye wakaja hadi kichangani kumuangalia,wakapata taarifa nimepelekwa polisi. Wakaja wakakuta jina langu limeandikishwa wakapumua maana walidhani nimekufa,ahahaha.

Unajua kuitiwa mwizi mtaani na ukapona siyo mchezo. Mtaani ukiitiwa mwizi hasa hii mitaa niliyokulia hawakupi nafasi ya kujitetea,ni mawe na vipigo tu vinafuata..Hadi unakufa.

Ila Mimi kwa sababu pengine kuonekana pale kwenye pool table au niseme Mungu hakutaka kuruhusu nide ile siku,basi nilipona.

Usiku mule ndani sikulala. Aisee cello siyo pazuri hata kidogo.

Kadili muda ulivyozidi kwenda walikuwa wanaingizwa watu wa ajabu ajabu. Huyu kaja anavuja damu,huyu anayembelea mikono,kachezea kipondo mtaani akaokolewa na polisi,anaburuza miguu Huku anaacha alama za damu chini.

Yani hadi chooni Kuna watu wametulia hawana habari.

Jamaa mmoja akaniuliza “we sharo umekuja kufanya nini humu? Mbona hufananii na haya mazingira?”

Nikawa Sina jibu nimekausha tu maana walinifanya nimeingia ndani nipo nao hapo hapo wamelala wengi wao hawawezi kutembea. Yule niliyempa teke la jicho ndiyo nikamwona vizuri kumbe nilimuumiza sana na lile boot,alikuwa anavuja damu alafu analia chini chini. Huruma ikaniingia.

Asubuhi ndugu wakaja kuniletea chakula na kuniona.Ghafla nikasikia jina langu linaitwa nikaamka ghafla.

Nikatoka nje nikamkuta Brother pale kwenye dawati. Afande wa kike akaniuliza “wewe ndiye Satoh Hirosh?” Nikamjibu ndiyo?

Afande: mbona unakuwa muhuni alafu hufanani na uhuni?

Mimi: Kimya,nikavuta tu pumzi.

Bro alikuwa ananitazama kwa hasira sana.

Sikumbuki hata nililetewa nini maana sikutaka kula chochote,nikardudi ndani.

Bro na wengine waliokuja kunicheki wakakaa kule nje kabisa kungojea muda. Nadhani walikuwa wanafanya process za kunitoa.

Baadae muda wa saa nane mchana nikaitwa Tena nikaambiwa umetolewa ila kesho unatakiwa uje kituoni. Kesho mnapaswa muende mahakamani. Moyo ukafanya paaa! Nikajiuliza kwamba kesi imekuwa kubwa kiasi hiki kweli? Ssasysi nitafungwa!! Maana jamaa kule ndani walikuwa hawawezi kutembea.

Afande: umeacha viatu,mkanda,wallet na simu. Kagua vitu vyako kama vipo na vimetimia kisha upotee. Alafu dogo acha uhuni utapotea.

Mimi: afande vitu vyangu vipo huko kwenu.

Afande: Huku vimefikaje?

Mimi: nilimwomba afande wa Jana usiku anihifadhie huko.

Afande: (Huku maafande wengine pia wakinikazia macho) dogo unaonekana tunajiamini sana eeh? Hii ni mara ya ngapi kufika hapa?

Afande Alikuwa ananikuliza Huku ameinama chini anaangalia Huku na kule.

Mimi: eeeh hivyo hivyo ndiyo viatu vyangu!!

Afande: (wakishirikiana na wenzie kutabasamu) dogo mjanja mjanja sana. Kumbe uliweka viatu vya bei mbaya Huku chini?

Mimi: (Huku nikiingiza mkono na kutoa kitu kimoja baada ya kingine kwenye viatu) afande vitu vyangu vimetimia.

Jamaa hawakunijibu,nikaanza safari ya kutoka nje Mimi na bro.

Njiani brother alinisema sana.

Bro: SH umeanza kujitegemea juzi tu umeshaanza uhuni. Inakuwaje unapigana na watu karibia muuane? Alafu nasikia walikuwa wanakuita mwizi,hujui kama ulibaki kidogo ufe? Unajua hii kesi ni ngumu sana maana unaweza kuozea jela hivi hivi. Nasikia wale jamaa umewaumiza sana.

Mimi: (Huku nikiwa nimezidiwa na woga baada ya kusikia naweza kuozea jela maana ni kweli jamaa wameumia sana hasa yule wa jichoni ambaye kule mwanzo nilisema nitaelezea kwa nini nilikuwa naelezea kwa ufasaha. Kule kituoni ndani ndiyo nilimshuhudia live). Kaka Mimi Sijafanya chochote kibaya,jamaa walikuwa wamenivamia.

Uzuri ndugu zangu wananijua Mimi siyo mtata Wala mkorofi na hata bro alipokuja kunitoa alikuwa ananisoma jinsi Gani najuta na kuumia kwa kilichotokea.

Kesho yake asubuhi nilifika kituoni Chang'ombe na bro. Nikapakiwa kwenye Ashok Mimi na watuhumiwa wenzangu safari ianze kwenda mahakamani.

Lakini gari ilichelewa sana kuondoka. Kumbe kule ndani brother alikuwa anajaribu kuongea na ndugu wa wale jamaa ili kesi imalizwe tu mtaani. Hata hivyo kesi ilikosa nguvu maana hakukuwa na ushahidi wowote kuwa Mimi nilikuwa mwizi na wale ndiyo watu ambao nilitaka kuwaibia. Kinyume chake wao ndiyo walionekana wezi.

Kesi iliisha mtaani na nikawa huru.

Mwanangu Y-lala aliponiona alikuwa analia tu Hana cha kuongea. Alijua mwanae ndiyo basi Tena hataniona. Samahani zilikuwa nyingi sana maana yeye na mwanamke wake walinikimbia na kuniachia msala niumalize mwenyewe.

Siku zikakatika.

Siku Moja Tena tukapanga kwenda kichangani kwa Habiba Mimi na mshikaji wangu Y-lala. Penzi kitovu cha uzembe.

Siku hiyo nafika mitaa ile ile kwenye pool japo siku hii ilikuwa mapema zaidi nikakuta stori ya “dogo kuwapiga watu kama 15 kwa mpigo”.

Jamaa wa kwanza: Aaah mwanangu dogo alikuwa anapiga kareti vibaya mno. Alinipigia watu kama 15 ndani ya dakika kadhaa tu.

Jamaa wa pili: Kuna teke hilo alinipigia dah!! Kama nilikuwa naangalia movie asee!! Dogo yuko vizuri. Alafu huwezi kumdhania maana bonge la sharo ukimwona.

Jamaa mwingine: Sema Jamal ameumia vibaya karibu na jicho,bila kumuwahi hospitali wangetoa jicho maana lilikuwa limevimba alafu limevilia damu balaa.

Wakati huo bila wao kujua wanayemwongelea alikuwa mitaa ile ile, Mimi nilikuwa mpole tu nawasilikiliza Hawa jamaa lakini nikasema kweli mbongo mpe kichwa cha habari,stori ataitunga mwenyewe. Wale watu mbona hawakufika hata 10 alafu jamaa anasema nimewapiga kama watu 15. Tena stori Ina chumvi nyingi balaa.

Kwa kifupi hii stori ilikuja kuwa maarufu mitaa ile yote maan ukitembea kama moto wa msituni. Nilikuwa nasikia sehemu mbali mbali wanamsimulia huyo “dogo” pasi na kujua mtu mwenyewe ni Mimi.

Baadae nikaachana na mambo ya kung Fu,hadi Leo Huwa napasha push up tu na mazoezi madogo madogo mara Moja moja.

Thank you for your time.

The End.
Nakuja keko machungwa kesho kutwa nilikuwa natafuta mtu wa kupimana naye uwezo mbeya nzima sijampata .
 
Temeke hiyo..Kuna mhuni alikuwa anaitwa msolopa na mwanae Kosovo...Ila Kuna mitaa inaitwa taa nyekundu ...veterinary na magurue ni hatari....pia watoto wakushua walipatikana chang'ombe...na ushenzini ni unubini kwa kina mh temba bila kusahau keko yote.
 
Vijana wa temeke walikuwa wanapenda sana kuzamia kwa madiba
Na wengi wamerudishwa kwenye ndege za cargo kama maiti.

Walipofika kule usela ukawa mwingi sana wakakutana na wasouth ambao kuchomana visu au kukupiga shaba ni kama anaua inzi tu.

Bro wangu yupo south tangu mwaka 2000 ila Mimi Sina hamu Nako.
 
Temeke hiyo..Kuna mhuni alikuwa anaitwa msolopa na mwanae Kosovo...Ila Kuna mitaa inaitwa taa nyekundu ...veterinary na magurue ni hatari....pia watoto wakushua walipatikana chang'ombe...na ushenzini ni unubini kwa kina mh temba bila kusahau keko yote.
Hakika Wewe ni mtoto wa Temeke.

Ila hadi Leo keko uhuni na usela mavi haujaisha. Wanawazingua sana washamba wa kuja pale taifa Benjamin Mkapa kukiwa na mechi.

Kuna siku ya Simba day jamaa walijaza ndoo simu walizopiga Benjamin Mkapa.
 
Mambo ya macamp camp yalivyoisha na uhuni uhuni nao ukaisha kwa kiasi kikubwa... Vijana waliokulia, temeke, mbagara, mwananyamala, tandale, magomeni, kinondoni baadhi ya maeneo wanaelewa haya mambo.
Mchiriku ulipokufa na uhuni umepungua Dar.

Mwanzo uliopoanza muziki wa singeli lkitaka kuja na uhuni wa mchiriku,ila madogo waliposwitch na kuimba singeli yenye Radha ikaleta ustaarabu.

Umesema makempu umenikumbusha Enzi hizo za kina jenerali Rupozi,Baba Isaya,wazee wa seven survival na ile kempu yao pale mtoni mtongani.

Life is fleeting.
 
Masela walipita na saa yangu CASIO Mwembeyanga, nimetoka zangu home Gerezani Kkoo, nikasema niende kwa uncle mitaa hiyo. Kufika Mwembeyanga nikasema niangalie mpira kidogo. Nikajisahau kidogo nikaweka mikono nyuma, msela alipita nayo kama kipanga.
Pole sana,mkuu.

Sasa hivi mwembe yanga serikali imepajenga vizuri sana. Pamekaa kistaarabu kama ulaya.

Pana gardens za kupumzika na viwanja vya michezo,walking sides nk.

Umepita siku za hivi karibuni?
 
Mchiriku ulipokufa na uhuni umepungua Dar.

Mwanzo uliopoanza muziki wa singeli ukitaka kuja na uhuni wa mchiriku,ila madogo waliposwitch na kuimba singeli yenye Radha ikaleta ushtaarabu.

Umesema makempu umenikumbusha Enzi hizo za kina jenerali Rupozi,Baba Isaya,wazee wa seven survival na ile kempu yao pale mtoni mtongani.

Life is fleeting.
Mnanda ulikua unafunga hadi barabara, nakumbuka mitaa ya kwa mama Zakaria kanyamala😅😅😅 baada ya show kuisha nyumba za jirani wote wanalia.

Macamp yalitengeneza uhasama mkubwa hadi kufanya ukanda na ukanda watu wasitembeleane, bifu zilikua nyingi sana na uhalifu ndio ulikua ndani yake.

Ilikua beach tu siku za eid mkikutana macamp mahasimu watu walikua wanauwana😅😅😅 ni panga zinatembea hatari hatari yani.
 
We mwamba ni story teller mzuri sana...umenifanya niingie kitaani kabisa
Ila Uzi umekosa wasomaji,naona ndiyo unafukuliwa sasa hivi.

Inaonekana jf watu wanapenda stori nusunusu, ili watu wakubembeleze at the same time Uzi uwe unatembea na kupata wasomaji wapya wengi zaidi.

ukimaliza fasta fasta kama mimi wanapotezea kama hivi,ahahaha.
 
Back
Top Bottom