Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?

Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?

batmanwafez

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
882
Reaction score
1,346
Habarini wakuu poleni na majukumu. Ttwende kwenye mada.

1. Unatafuta chumba/kiwanja, ukaingia Jamiiforums ukaona tangazo la dalali na ametaja eneo na bei.
Sasa kuepuka kumlipa ile 10%

Kwakuwa unafahamu lile eneo wewe unaenda unaulizia mwenyewe na ukalipa direct kwa mwenye mali.
Je, hiyo ni sawa?

2. Unatafuta chumba cha kupanga ukampata dalali ana chumba kizuri tu na ukakipenda. Bwana dalali akakupeleka kukiona hicho chumba ila mteja ukadai hujakipenda, ukampa elfu 10 yake ya kukuzungusha.

Baada ya muda ukarudi ukaongea na mwenye nyumba direct ukamlipa kodi yake. Hapa ukawa umeruka kumpa dalali kodi ya mwezi mmoja.

Swali kwa wadau (dalali na wateja)

1. Je, ni sawa mteja kumzunguka kutumia mbinu hizo?

2. Je, huyu dalali akigundua kuwa umemzunguka atakufanya nini, kuna sheria au taratibu zozote?

Wadau (dalali na mteja) waliowahi kufanya hivi.

Share na sisi tafadhilini.
 
Nao kuna muda wana kaupumbavu fulani umempa kabisa specifications za chumba /nyumba unayotaka na anakuhakikishia kabisa anayo unaenda kuangalia hata haifananii kibaya zaidi anavyoisifia sasa utadhani ataishi yeye ili mradi tu akupige hela ya udalali ndio maana wanazungukwa.
 
Iwapo umegundua kuna tofauti kubwa ya bei kati ya dalali na mwenye nymba ya kiwanja, vunja mkataba kwa kumalizana na mwenye mali, kisha mfahamishe ykweli dalali, haki yake sio zaidi ya 10%
 
Udalali ni kazi kama zingine. Heshimu makubaliano.
Wanalipa Kodi? Serikali inawatambua?

Bora udalali wa Nyumba lakini huu udalali wa mazao ya wakulima Ni utapeli mtupu.

Mkulima anapeleka mazao sokoni. Lakini haruhusiwi kuyauza direct kwa mteja mpaka apite kwa dalali Wala sio utaratibu wa kisheria still analanguliwa Bei na Sasa jamii imebariki na kuwaita walanguzi
 
Hapo ni kuamua tuu kuheshimu makubaliano, hasa kama nimeona bila wewe ningepata tabu..

Pia naangalia hicho cha udalali unakula mara ngapi na kiasi gani,..

Nimewazunguka sana k.koo, hasa wale unaenda nunua bidhaa, ukifika kumbe sio muuzaji yeye anakusubirisha, "Subiri nikakuletee store".
Mara ya kwanza utanishika, Ya pili nakuja na mtu akuungie Mkia, mpaka store/godauni au kwa mmiliki wa mali/bidhaa...

Baada ya hapo Hutonionaa, ishatokea kama watatu hivi Ile paaap, Umeenda mara nyingine, unamkuta au anakukuta kule chimbo store/godauni/Kwa mwenye mali wasiko taka ukujue akiwa kwenye mishe zake tena za udalali,
Kama binadamu unapata ka aibu flani hivi, ila tatizo aibu Haikupi tonge, inabidi maisha yaendelee.

Japo naona Kuna mstari mwembamba sana unamtenganisha Dalali na Tapeli.

Lakini pia wana msaada, kuna muda wanarahisisha sana maisha, kuna mambo pengine bila wao usingefanikiwa kabisa, Binafsi mpka nitafute Dalali kwenye inshu yoyote, Ni kama kweli njia binafsi zote zimekwama.

Kwahio kama MLIKUBALIANA, na akakusaidia mlipe...
Ukimzunguka wewe ni TAPELI, hamna kupindisha lugha.
 
Nimekutana na dalali mjinga sijapata kuona.
Jinga jinga hasa.
Na hela anaikosa.

Anabaki kupiga piga simu kila saa.

Sikutaka kumzunguka.

Juzi nimeenda na cash mzigo wa maana nilipie.

Namuambia mpigie mwenye mali tumsikie.
Ooooo hiii nilimpeleka mtu jana aliluwa na pesa kama yako kaikataa.
Sawa alikataa jana lakini mpigie mda huu nisikie.
Hataki.

Nikaondoka.
Nikasema we fala sikupigii utapiga mwenyewe.
Akapiga utaongeza ngapi nikakomaaa kuwa nina ile ile tena imepungua nitaandika deni.
Akasema mwenye mali kasafiri nikasema fresh.

Uzuri mzee wangu mmoja anamfahamu mwenye mali na alimtajia bei ile ile niliyonayo.

Ndo ishaisha hiyo.

Jana tena dalali anapiga kutaka kujua hela imepungua au iko pale pale hapo ndo nilipomcheka na kumshusha.

Mali nalipia kesho bila yeye ndo imeisha hiyo.

Na ni hela pungufu ya ile aliyoikataa.

Means cha juu angepata sema alitaka cha juu zaidi.

Kakosa vyote.
 
batmanwafez,

Nilishawahi fanya hivyo maan hela ya kumpa sikuwa nayo.....hata kama akijua mimi nachojua yeye anakuwa na makubaliano na mwenye nyumba, kwa hiyo kama akiambiwa na mwenye nyumba kuwa hakuna chumba kesi imeisha hapo, so mimi navyohisi hawezi kukusumbua kwa lolote maan mkataba ni wako na mwenye nyumba
 
Nimekutana na dalali mjinga sijapata kuona.
Jinga jinga hasa.
Na hela anaikosa.

Anabaki kupiga piga simu kila saa.

Sikutaka kumzunguka.

Juzi nimeenda na cash mzigo wa maana nilipie.

Namuambia mpigie mwenye mali tumsikie.
Ooooo hiii nilimpeleka mtu jana aliluwa na pesa kama yako kaikataa.
Sawa alikataa jana lakini mpigie mda huu nisikie.
Hataki.

Nikaondoka.
Nikasema we fala sikupigii utapiga mwenyewe.
Akapiga utaongeza ngapi nikakomaaa kuwa nina ile ile tena imepungua nitaandika deni.
Akasema mwenye mali kasafiri nikasema fresh.

Uzuri mzee wangu mmoja anamfahamu mwenye mali na alimtajia bei ile ile niliyonayo.

Ndo ishaisha hiyo.

Jana tena dalali anapiga kutaka kujua hela imepungua au iko pale pale hapo ndo nilipomcheka na kumshusha.

Mali nalipia kesho bila yeye ndo imeisha hiyo.

Na ni hela pungufu ya ile aliyoikataa.

Means cha juu angepata sema alitaka cha juu zaidi.

Kakosa vyote.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
Mziki wake utaujua VP unajua??!!! akigundua ushachukua mzigo. Mbona utaomba pooo.

Mimi back in the days dalali nilimzunguka. Weeeee mziki mnene. Unajua wale wanakua wengi. So mmoja akifanikisha wanagawana woote. So wenzake wakiona mbona Mali imeuzwa wanaanza kuulizana na kuchunguza dalali nani kauza mzigo halaf kala pesa bila ration kufanyika.

Kama ni nyumba mbona utahama.

Dalali alivogundua nimemzunguka aliniwekea vitisho mpk vya kunidhuru. Yaani nili give up mwenyewe nikamuita tuyamalize kwa kumpa haki yake.
 
Back
Top Bottom