Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?

hakuna kitu sipendi duniani kama udalali mi huwa naona ni wizi,hata wale wanaokatisha ticket stend mawaona kama madalal tu nao wananikera balaa,basi moja,trip Moja nauli tofaut,KUMZUNGUKA DALALI NAONA IKO POA SANA
wale wakatisha tiketi ndo kiboko sasa yaan ukiwa na safar afu hujui nauli ya unakoenda ahahahaa watakupiga ushangae

juzi naenda mwanza nkapanda basi moja na mdada mmoja anashukia dodoma. nauli wamemkatia elfu 40 wakat mie wa mwanza nmelipa 35 daah nlisikitka sana. mm siez kulipa nauli mpaka nipeleleze je nauli ya nnako3nda ni sh ngapi?? yaan pale kwny bus naenda nkiwa na nauli yangu kichwan.
 
Mkuu wewe muoga mno.
Yaani mjini hapa mtu anitishe kiasi hiko?
Halafu napendaga ligi za hivyo.
Unkinidindishia ndo nafanya kusudi.

Bora uje kistaarabu tukae mezani naweza walau kukupa hela ya serengeti 4.
Ila vitisho mhh
Itakua alimuona mwana ni wa kuja tu hapa mjini,akaona mikwara yake jamaa ataingia king.
 
Kwenye nyumba/Mali hawakubali kupokea pesa directly kutoka kwa mteja mpaka dalali awepo.

Na wao wanawategemea madalali kuwaletea wateja kabla yako na baada yako.
Ni mwenye nyumba mpuuzi ndio atafanya hivyo.

Mie nalipa kodi 250k kwa mwezi na kipindi natafuta nyumba nilimtafuta dalali flani mkubwa tu akanizungusha maeneo tofauti almost nyumba zote za mjini zilizokuwa wazi kipindi hicho alinionesha. Niliweka mafuta kwenye chombo chake akanizungusha almost 2 days.

Nilipopata hii nyumba ambayo ndio naishi kwa kuwa ilikuwa 0km na pia kali sana nilipiga hesabu zangu freshi nikalipa advance. Mzee mwenye nyumba ni Don level za akina Laswai maana ndio washkaji zake. Nilichukua namba zake na mapema tu kesho kabla hajatoka kwenda mishe nikamuibuka mwenyewe kumkabidhi kimango.

Kiufupi swala la kumpa dalali 250k halikuniingia akilini. Imagine unampa dalali hela yote hio kwa sababu zipi? Kwakuwa kanionesha nyumba ile pale? Japo alikuja kusanuka nishalipa hela direct kwa mzee kijanja akaanza kunisumbua kuhusu genji lake nikamwambia nimesafiri nikamtumia 50k na kumuahidi ntamuongezea nikirudi kisha nikamtwanga block!
 
Hahah mwambie Don msela wake Mzee Laswa.. hali ngumu sasa hivi Tra mixer wazee wa makumbusho wamemkaba kinyama koo.
 
Anasema Laswai yuko hoi maana walimsafisha mipunga yote ya bureau de change. Landlord wangu yeye alipona katika ule msako alisanuliwa mapema akafunga bureau yake.
 
Weeeee nilizitema mbona.
No ni pesa ya kodi mwezi mmoja nilimpa. Si unajua zao. Mwezi mmoja wa kwao.
Hahah we utakuwa muoga sema.. Sasa mie niko ndani ya gari huyo dalali atanifanya nini cha maana? 😝😝😝 Labda antupie majini ila kwa kusema atanivamia or sumthn ni uongo!
 
Anasema Laswai yuko hoi maana walimsafisha mipunga yote ya bureau de change. Landlord wangu yeye alipona katika ule msako alisanuliwa mapema akafunga bureau yake.
Kweli aisee nasikia jamaa mpunga wake wa bureau mpk leo bila bila,hata afya yake kwa sasa hivi ni changamoto.
 
batmanwafez,

Nilishawahi fanya hivyo maan hela ya kumpa sikuwa nayo.....hata kama akijua mimi nachojua yeye anakuwa na makubaliano na mwenye nyumba, kwa hiyo kama akiambiwa na mwenye nyumba kuwa hakuna chumba kesi imeisha hapo, so mimi navyohisi hawezi kukusumbua kwa lolote maan mkataba ni wako na mwenye nyumba
Hapana si hivyo!
Kwani bila huyo dalali Huyo mwenye nyumba ungemjuaje? Kuna kitu kimefanya ukamjua mwenyewe ambae ndio huyo dalali? Cha msingi ni kuwalipa ela zao kama mlivyokubaliana ,Kwa sababu kwao hio ndio kazi sasa usipowalipa ela yao unategemea nini? Unaweza kutokuwalipa lakini sifikiri kama ni jambo zuri.
 
Habarini wakuu poleni na majukumu. Ttwende kwenye mada.

1. Unatafuta chumba/kiwanja, ukaingia Jamiiforums ukaona tangazo la dalali na ametaja eneo na bei.
Sasa kuepuka kumlipa ile 10%

Kwakuwa unafahamu lile eneo wewe unaenda unaulizia mwenyewe na ukalipa direct kwa mwenye mali.
Je, hiyo ni sawa?

2. Unatafuta chumba cha kupanga ukampata dalali ana chumba kizuri tu na ukakipenda. Bwana dalali akakupeleka kukiona hicho chumba ila mteja ukadai hujakipenda, ukampa elfu 10 yake ya kukuzungusha.

Baada ya muda ukarudi ukaongea na mwenye nyumba direct ukamlipa kodi yake. Hapa ukawa umeruka kumpa dalali kodi ya mwezi mmoja.

Swali kwa wadau (dalali na wateja)

1. Je, ni sawa mteja kumzunguka kutumia mbinu hizo?

2. Je, huyu dalali akigundua kuwa umemzunguka atakufanya nini, kuna sheria au taratibu zozote?

Wadau (dalali na mteja) waliowahi kufanya hivi.

Share na sisi tafadhilini.
Mkuu kuna sheria yoyote inayokutaka wewe umlipe huyo dalali hyo 10% ya kazi yako???
 
Sio @Tunzo
Kwny magari madalali ni wajinga tena mataahira kabisa.

Kuna dalali mmoja wa kule kupatana.com na hata humu JF yumo sana tu akiuza magari, alikua anauza nissan flan hivi kwa Mil 13.5,nikapambana sana nikampata mmiliki wa hio gari mwishowe akaiuza kwa mil 8.3 tu.

Kumuuliza mmiliki anasema dalali alimwambia huko mitandaoni anaiuza kwa mil.9 kumbe anaiuza mil 13.5m na amesababisha gari imekaa mwaka mzima bila kuuzika.
 
Huyo alikua zaidi ya kilaza
wale wakatisha tiketi ndo kiboko sasa yaan ukiwa na safar afu hujui nauli ya unakoenda ahahahaa watakupiga ushangae

juzi naenda mwanza nkapanda basi moja na mdada mmoja anashukia dodoma. nauli wamemkatia elfu 40 wakat mie wa mwanza nmelipa 35 daah nlisikitka sana. mm siez kulipa nauli mpaka nipeleleze je nauli ya nnako3nda ni sh ngapi?? yaan pale kwny bus naenda nkiwa na nauli yangu kichwan.
 
Udalali ni kazi kama zingine. Heshimu makubaliano.
Kuna sheria ambayo inawa-walinda madalali, kila mtu anaefanya kazi ya udalali lazima awe amesajiliwa, kwa mfano madalali wanaofanya kazi za udalali wa mahakama wanasajiliwa na msajili wa mahakama kuu huko Tanzania, madalali wengi walioko mtaani ni wahuni hata ofisi hawana, wanafanya kazi kihuni, ni madalali wachache waliosajiliwa na msajili wa madalali. Kuna Sheria ya Udalali ya mwaka 1928 ni ya zamani na imepitwa na wakati. Ni vizuri madalali wakafaamika, na akiwa na leseni inakuwa nzuri zaidi, akikutapeli unaweza kumreport na utaratibu ukafuatwa kupata haki.
 
Ni mwenye nyumba mpuuzi ndio atafanya hivyo.

Mie nalipa kodi 250k kwa mwezi na kipindi natafuta nyumba nilimtafuta dalali flani mkubwa tu akanizungusha maeneo tofauti almost nyumba zote za mjini zilizokuwa wazi kipindi hicho alinionesha. Niliweka mafuta kwenye chombo chake akanizungusha almost 2 days.

Nilipopata hii nyumba ambayo ndio naishi kwa kuwa ilikuwa 0km na pia kali sana nilipiga hesabu zangu freshi nikalipa advance. Mzee mwenye nyumba ni Don level za akina Laswai maana ndio washkaji zake. Nilichukua namba zake na mapema tu kesho kabla hajatoka kwenda mishe nikamuibuka mwenyewe kumkabidhi kimango.

Kiufupi swala la kumpa dalali 250k halikuniingia akilini. Imagine unampa dalali hela yote hio kwa sababu zipi? Kwakuwa kanionesha nyumba ile pale? Japo alikuja kusanuka nishalipa hela direct kwa mzee kijanja akaanza kunisumbua kuhusu genji lake nikamwambia nimesafiri nikamtumia 50k na kumuahidi ntamuongezea nikirudi kisha nikamtwanga block!

Sijajua ni uoga, Udaslamu au ni unini unaopelekea watu kuwahanya madalali kiasi hicho, imagine mwenye nyumba pia anamuogopa dalali! Au ni ule ubabe mbuzi wa mitaani kwamba anaweza kukuvamia akakupiga?!

Okay, mi nyumba ninayoishi inajulikana kwa mtaa huu mzima kuwa Landlady hataki madalali, hata wakileta mteja wanampa mteja namba ampigie mwenyewe mwenye nyumba halafu wanakaa pembeni wanakusikiliza makubaliano yenu.

Nilienda na dalali mmoja bahati nzuri ilikuwa jumapili, tukafika tukakuta mafundi wanamalizia vitu vidogo vidogo nje ikiwemo na kufitisha geti, tukaomba namba mafundi wakatupa, nikampigia akanambia naomba dakika 10 natokea nyumbani kwangu nakuja. Dalali akanambia usimwambie mi ni dalali mwambie tu ni rafiki yako nikamuuliza why akasema tunasikia hatakagi madalali (bila ye kujua nikashangilia kiroho roho). Yule mama akaja nikaongea nae tukakubaliana ilikuwa katikati ya mwezi nikamwambia basi nadeposit now kwa mpesa 500k ili nihold nyumba maana watu wengi walikuwa wanatafuta nyumba, halafu mwisho wa mwezi nadeposit 1M iliyobaki then nahamia tukawa tumemalizana na mwenye nyumba kimtindo huo tukaachana. Dalali bila kujua amejiloga mwenyewe akaanza Bosi nyumba umeshachukua sasa chetu vipi, nikamwambia nina laki hapa niwape 50k tuachane maana 250k siwezi wapa mnaona nyumba yenyewe nalipa kwa installment sina hela, wakaanza ohh tuko wengi hiyo hailipi na blah blah, nikajiuliza kichwani wapo wengi? Na pale amenipeleka mmoja? Na amenipeleka kunionesha tu! Nikamwambia chukua tu hii 50k sababu nimekutoa kwa kazi zako kiheshima tu kiroho safi akaendeleza malalamiko, nikaichomoa nikampa nikapanda bajaji huyooo. Sasa mwisho wa mwezi wakawa wananivizia waone ninavohamia wanidai, nilimjibu tu kiufupi hiyo hela sina labda nikipata ntakwambia. Hadi leo hii ndio nitolee.

Huwa namuuliza mwenye nyumba wanasema kuna siku utakosa wateja, ananijibu kazini kwangu kila mwaka inaingia intake mpya nianze kukimbizana na madalali mimi? Hata nikikosa nitatumia connections zangu kupata wateja, Mama mmoja mstaarabu sana na msomi pia.
 
Hiyo kitu ilinitokea siku ya kwenda kufanya malipo sikuenda pamoja na dalali Japo baadaye niliwapa ela
Changamoto ya udalali chain inakuwa ndefu.
MI nilimuagiza jamaa mmoja, na Yeye akamuuliza mtu mwingine,mtu mwingine naye akatuunganisha kwa watu wa eneo lile. Pesa ikatolewa kwa mtu wa kwanza kila dalali anadai ela, wakaishia kudhurumiana
Mkuu, Biashara hii ya hovyo haiwapi usalama wa kisheria mtafuta nyumba kwa maana ya legal protection.
 
Sijajua ni uoga, Udaslamu au ni unini unaopelekea watu kuwahanya madalali kiasi hicho, imagine mwenye nyumba pia anamuogopa dalali! Au ni ule ubabe mbuzi wa mitaani kwamba anaweza kukuvamia akakupiga?!

Okay, mi nyumba ninayoishi inajulikana kwa mtaa huu mzima kuwa Landlady hataki madalali, hata wakileta mteja wanampa mteja namba ampigie mwenyewe mwenye nyumba halafu wanakaa pembeni wanakusikiliza makubaliano yenu.

Nilienda na dalali mmoja bahati nzuri ilikuwa jumapili, tukafika tukakuta mafundi wanamalizia vitu vidogo vidogo nje ikiwemo na kufitisha geti, tukaomba namba mafundi wakatupa, nikampigia akanambia naomba dakika 10 natokea nyumbani kwangu nakuja. Dalali akanambia usimwambie mi ni dalali mwambie tu ni rafiki yako nikamuuliza why akasema tunasikia hatakagi madalali (bila ye kujua nikashangilia kiroho roho). Yule mama akaja nikaongea nae tukakubaliana ilikuwa katikati ya mwezi nikamwambia basi nadeposit now kwa mpesa 500k ili nihold nyumba maana watu wengi walikuwa wanatafuta nyumba, halafu mwisho wa mwezi nadeposit 1M iliyobaki then nahamia tukawa tumemalizana na mwenye nyumba kimtindo huo tukaachana. Dalali bila kujua amejiloga mwenyewe akaanza Bosi nyumba umeshachukua sasa chetu vipi, nikamwambia nina laki hapa niwape 50k tuachane maana 250k siwezi wapa mnaona nyumba yenyewe nalipa kwa installment sina hela, wakaanza ohh tuko wengi hiyo hailipi na blah blah, nikajiuliza kichwani wapo wengi? Na pale amenipeleka mmoja? Na amenipeleka kunionesha tu! Nikamwambia chukua tu hii 50k sababu nimekutoa kwa kazi zako kiheshima tu kiroho safi akaendeleza malalamiko, nikaichomoa nikampa nikapanda bajaji huyooo. Sasa mwisho wa mwezi wakawa wananivizia waone ninavohamia wanidai, nilimjibu tu kiufupi hiyo hela sina labda nikipata ntakwambia. Hadi leo hii ndio nitolee.

Huwa namuuliza mwenye nyumba wanasema kuna siku utakosa wateja, ananijibu kazini kwangu kila mwaka inaingia intake mpya nianze kukimbizana na madalali mimi? Hata nikikosa nitatumia connections zangu kupata wateja, Mama mmoja mstaarabu sana na msomi pia.
Dada kuna sheria mpya inaandaliwa, muda wowote muswada wake utapelekwa bungeni kusomwa,...itawalazimisha madalali kusajiliwa kwa level ya mtaa/kata/wilaya/mkoa na taifa. Na pia watatakiwa wawe na taaluma husika kutoka vyuo vinavyotambulika.
Ubabaishaji ulizidi na serikali inakosa mapato huku wananchi wakiumia.
 
Back
Top Bottom