Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?

Maisha ya Udalali: Kumzunguka dalali ni sawa?

Dada kuna sheria mpya inaandaliwa, muda wowote muswada wake utapelekwa bungeni kusomwa,...itawalazimisha madalali kusajiliwa kwa level ya mtaa/kata/wilaya/mkoa na taifa. Na pia watatakiwa wawe na taaluma husika kutoka vyuo vinavyotambulika.
Ubabaishaji ulizidi na serikali inakosa mapato huku wananchi wakiumia.

Hapo ni sawa, bora umlipe kihalali kuliko kumlipa mtu ambaye kwanza kazi aliyofanya hailingani na malipo anayodai na halipi kodi popote. Binafsi siwezi mlipa dalali pesa ya mwezi mmoja, mpaka walete hiyo sheria.
 
Sijajua ni uoga, Udaslamu au ni unini unaopelekea watu kuwahanya madalali kiasi hicho, imagine mwenye nyumba pia anamuogopa dalali! Au ni ule ubabe mbuzi wa mitaani kwamba anaweza kukuvamia akakupiga?!

Okay, mi nyumba ninayoishi inajulikana kwa mtaa huu mzima kuwa Landlady hataki madalali, hata wakileta mteja wanampa mteja namba ampigie mwenyewe mwenye nyumba halafu wanakaa pembeni wanakusikiliza makubaliano yenu.

Nilienda na dalali mmoja bahati nzuri ilikuwa jumapili, tukafika tukakuta mafundi wanamalizia vitu vidogo vidogo nje ikiwemo na kufitisha geti, tukaomba namba mafundi wakatupa, nikampigia akanambia naomba dakika 10 natokea nyumbani kwangu nakuja. Dalali akanambia usimwambie mi ni dalali mwambie tu ni rafiki yako nikamuuliza why akasema tunasikia hatakagi madalali (bila ye kujua nikashangilia kiroho roho). Yule mama akaja nikaongea nae tukakubaliana ilikuwa katikati ya mwezi nikamwambia basi nadeposit now kwa mpesa 500k ili nihold nyumba maana watu wengi walikuwa wanatafuta nyumba, halafu mwisho wa mwezi nadeposit 1M iliyobaki then nahamia tukawa tumemalizana na mwenye nyumba kimtindo huo tukaachana. Dalali bila kujua amejiloga mwenyewe akaanza Bosi nyumba umeshachukua sasa chetu vipi, nikamwambia nina laki hapa niwape 50k tuachane maana 250k siwezi wapa mnaona nyumba yenyewe nalipa kwa installment sina hela, wakaanza ohh tuko wengi hiyo hailipi na blah blah, nikajiuliza kichwani wapo wengi? Na pale amenipeleka mmoja? Na amenipeleka kunionesha tu! Nikamwambia chukua tu hii 50k sababu nimekutoa kwa kazi zako kiheshima tu kiroho safi akaendeleza malalamiko, nikaichomoa nikampa nikapanda bajaji huyooo. Sasa mwisho wa mwezi wakawa wananivizia waone ninavohamia wanidai, nilimjibu tu kiufupi hiyo hela sina labda nikipata ntakwambia. Hadi leo hii ndio nitolee.

Huwa namuuliza mwenye nyumba wanasema kuna siku utakosa wateja, ananijibu kazini kwangu kila mwaka inaingia intake mpya nianze kukimbizana na madalali mimi? Hata nikikosa nitatumia connections zangu kupata wateja, Mama mmoja mstaarabu sana na msomi pia.
Hio ndio inatakiwa yani, hawa madalali wanahisigi hela ni nyepesi sana. Yani nikupe laki 2 kwa kunionesha nyumba tu! Na labda usinikutanishe na mwenye nyumba maana nikikutana nae tu umeisha!
 
Kesi ya kuzungukwa hiyo ni kati yake na Mmiliki sio mimi Mteja, kama Mmiliki kakubali biashara bila Dalali wake basi wamalizane wao kwa wao.
 
Kuna baadhi ya business dalali yuko kihalali na ana sheria inayolinda kazi yake.

Mfano: Insurance Brokers (hawa ni madalali), kuna brokers wa shares/stocks (huwezi kuuza share zako bila kupita kwa hawa watu), kuna mawakala wa michezo (sports agents), kuna sales agents kama wa flights nk nk.

Tatizo la hawa wa nyumba na mazao ni kwa sababu nchi yetu haijaamua kurasimisha hizi biashara, ndiyo maana kuna janja janja nyingi sana. Wateja tunaona kama tunapigwa, na mifumo ya malipo haiko sawa, kwa sababu unapolipa miezi 12 ya kupanga nyumba, dalali alitakiwa achukue kule kwa aliyepokea hela na si kwa wewe uliyetoa, au kuwe na 50 50.
 
Hapo ni sawa, bora umlipe kihalali kuliko kumlipa mtu ambaye kwanza kazi aliyofanya hailingani na malipo anayodai na halipi kodi popote. Binafsi siwezi mlipa dalali pesa ya mwezi mmoja, mpaka walete hiyo sheria.
Saingine wanakupeleka kwenye nyumba ambazo hazikaliki unakuta ushampa hela na kodi umelipa usiku hulali! ila watasema nyumba nzuri haina shida 🤣🤣🤣
 
Kesi ya kuzungukwa hiyo ni kati yake na Mmiliki sio mimi Mteja, kama Mmiliki kakubali biashara bila Dalali wake basi wamalizane wao kwa wao.
Na hata hio ya kulipa mwezi mmoja kiutaratibu anatakiwa alipe mwenye nyumba. Amuachie dalali mwezi mmoja katika ile 6!
Ila ujanja unatumika kumtwisha mpangaji gunia la misumari.
 
Mimi baadhi ya shughuli zangu huwa nahitaji huduma ya Dalali...kuna wakati nasema ngoja nikaze nisiwatafute wale hela yangu bure...ila najikuta mambo yanasinzia naamua kuwatafuta na mambo wanafanikisha.

Ingawa nao wana nafasi yao ila kuna wakati wanakera.
 
wale wakatisha tiketi ndo kiboko sasa yaan ukiwa na safar afu hujui nauli ya unakoenda ahahahaa watakupiga ushangae

juzi naenda mwanza nkapanda basi moja na mdada mmoja anashukia dodoma. nauli wamemkatia elfu 40 wakat mie wa mwanza nmelipa 35 daah nlisikitka sana. mm siez kulipa nauli mpaka nipeleleze je nauli ya nnako3nda ni sh ngapi?? yaan pale kwny bus naenda nkiwa na nauli yangu kichwan.
Hahaaaaa, wale jamaa wanakera sanaaaa...
Anakufuata kuanzia nje, Unamwambia kabisa wewe usijisumbue kama unavyonisindikiza hivi nikifika nitapanda basi lako au nikupe chochote,
Anaitikia kabisa "wewe hunipi chochote watanipa kule" Cha kushangaza ukifika anaanza "ukinisaidia hata mia tano sio mbaya"... hapa ndio wanachefuaga,

Mimi sikuhizi nikienda stend natembea na ticket niliyokwisha itumia mkononi nimeining'iniza,
Hakuna anaye kufuata.
 
Ukutane na mwenye nyumba Mbea...
Unamfuata kimya kimya muyamalize..

Anamtonya dalalii..
"mtu wako yupo hapa anakuzunguka"...
Bongo kuna mambo yamekaa kikatuni katuni, ila ni watu ndio wanayafanya.
 
Nilikuwa namsaidia rafiki yangu aliyehamia Dodoma kutafuta nyumba, Anakupeleka kwenye nyumba tofauti na unayoitarajia halafu anaanza kazi imesimama hii si unaona [emoji3] Ilifika muda niliwauliza kwa ukali “hivi ni sisi hatuna akili au ni ninyi hamna akili”?
Na imagne vyenye ulivokuwa unaongea kwan ukali, nmebaki kucheka had mbavu znauma mweeeeeeh.
 
Habarini wakuu poleni na majukumu. Ttwende kwenye mada.

1. Unatafuta chumba/kiwanja, ukaingia Jamiiforums ukaona tangazo la dalali na ametaja eneo na bei.
Sasa kuepuka kumlipa ile 10%

Kwakuwa unafahamu lile eneo wewe unaenda unaulizia mwenyewe na ukalipa direct kwa mwenye mali.
Je, hiyo ni sawa?

2. Unatafuta chumba cha kupanga ukampata dalali ana chumba kizuri tu na ukakipenda. Bwana dalali akakupeleka kukiona hicho chumba ila mteja ukadai hujakipenda, ukampa elfu 10 yake ya kukuzungusha.

Baada ya muda ukarudi ukaongea na mwenye nyumba direct ukamlipa kodi yake. Hapa ukawa umeruka kumpa dalali kodi ya mwezi mmoja.

Swali kwa wadau (dalali na wateja)

1. Je, ni sawa mteja kumzunguka kutumia mbinu hizo?

2. Je, huyu dalali akigundua kuwa umemzunguka atakufanya nini, kuna sheria au taratibu zozote?

Wadau (dalali na mteja) waliowahi kufanya hivi.

Share na sisi tafadhilini.
Dalali ni kazi Kama kazi zingine hata Mino Raiola ni dalali was CR7 ila tu kwa sababu tunatumia neno agent ndio maana anaheshimika.

Dalali azungukwi Wala madalali hatuzungukani "what goes around comes around around",ukimzunguka dalali atajua tu coz hiyo sehemu anayokupeleka ndio shamba lake huwa tunakusanya elf 20 ishurini za service charge kila siku ,siku nikileta mteja kwa hiyo chumba lazima mwny nyumba atanitonya bwana chumba kimechukuliwa na mteja X Mara paap nakukuta ndio unatoka chooni na kitaulo chako akiya Mungu naondoka na taulo nakuacha kama ulivyo.

Muhimu kuheshimu pale mwenzio anapopatia kipato ,usimdharau mtu sababu anafanya hyo job,just nimekutana na dalali wa magari ambaye ni dokta wa hospital kapiga vitu vyake MUHAS hapo akaanza kunitisha nikamwambia tulia mm mwnywe dalali wa nyumba ila mhandis alikuja kuniuzia gari.Kwa hiyo tuka merge now akipata wateja wa nyumba ananipasia na mm nikipata wa magari nampasia tunagawana asilimia kitu na box.
 
Back
Top Bottom