Sijajua ni uoga, Udaslamu au ni unini unaopelekea watu kuwahanya madalali kiasi hicho, imagine mwenye nyumba pia anamuogopa dalali! Au ni ule ubabe mbuzi wa mitaani kwamba anaweza kukuvamia akakupiga?!
Okay, mi nyumba ninayoishi inajulikana kwa mtaa huu mzima kuwa Landlady hataki madalali, hata wakileta mteja wanampa mteja namba ampigie mwenyewe mwenye nyumba halafu wanakaa pembeni wanakusikiliza makubaliano yenu.
Nilienda na dalali mmoja bahati nzuri ilikuwa jumapili, tukafika tukakuta mafundi wanamalizia vitu vidogo vidogo nje ikiwemo na kufitisha geti, tukaomba namba mafundi wakatupa, nikampigia akanambia naomba dakika 10 natokea nyumbani kwangu nakuja. Dalali akanambia usimwambie mi ni dalali mwambie tu ni rafiki yako nikamuuliza why akasema tunasikia hatakagi madalali (bila ye kujua nikashangilia kiroho roho). Yule mama akaja nikaongea nae tukakubaliana ilikuwa katikati ya mwezi nikamwambia basi nadeposit now kwa mpesa 500k ili nihold nyumba maana watu wengi walikuwa wanatafuta nyumba, halafu mwisho wa mwezi nadeposit 1M iliyobaki then nahamia tukawa tumemalizana na mwenye nyumba kimtindo huo tukaachana. Dalali bila kujua amejiloga mwenyewe akaanza Bosi nyumba umeshachukua sasa chetu vipi, nikamwambia nina laki hapa niwape 50k tuachane maana 250k siwezi wapa mnaona nyumba yenyewe nalipa kwa installment sina hela, wakaanza ohh tuko wengi hiyo hailipi na blah blah, nikajiuliza kichwani wapo wengi? Na pale amenipeleka mmoja? Na amenipeleka kunionesha tu! Nikamwambia chukua tu hii 50k sababu nimekutoa kwa kazi zako kiheshima tu kiroho safi akaendeleza malalamiko, nikaichomoa nikampa nikapanda bajaji huyooo. Sasa mwisho wa mwezi wakawa wananivizia waone ninavohamia wanidai, nilimjibu tu kiufupi hiyo hela sina labda nikipata ntakwambia. Hadi leo hii ndio nitolee.
Huwa namuuliza mwenye nyumba wanasema kuna siku utakosa wateja, ananijibu kazini kwangu kila mwaka inaingia intake mpya nianze kukimbizana na madalali mimi? Hata nikikosa nitatumia connections zangu kupata wateja, Mama mmoja mstaarabu sana na msomi pia.