Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Maisha ya ufungwani/ mahabusu ni machungu ndugu zanguni

Mkanganyiko kukanganya

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2022
Posts
1,204
Reaction score
5,053
Maisha ya mahabusu/ mfungwa ni magumu na mabaya ila siyo kwa ubaya ule unaovumishwa mitaani kwamba kule kuna
  • Kupigwa na wababe
  • Kunyang'anywa chakula
  • Kuteswa
  • Kubakwa n.k ni hapana
Maisha yanaenda kawaida ikiwa kwa upande wa burudani
  • Television ipo
  • Draft/bao lipo
  • Mpira wa miguu upo
"Kwaya kwa waimbaji n.k

Vile vile watu wanapiga ibada kila siku jioni na asubuhi dini zote kuu mbili kwa muda wao. Na pia baadhi ya watu wanasali/swali haswa kwakuwa tegemeo lao lililobaki ni Mungu tu kuwatoa huko.

Changamoto kubwa ni kisaikolojia
  • Kukosa uhuru
  • Kutoona familia/marafiki
  • Papuchi hakuna
  • Msosi ni ugali mwaka tena ni mchana tu hakuna supper😂
  • Asubuhi uji bila sugar mwaka
Ile hali ya kupangiwa kila kitu kula, kulala, kuamka, kazi ngumu, adhabu, kuhesabiwa inakera sana unaweza rukwa na akili. Maisha ya mahabusu/ ufungwani ili uishi kwa amani fuata taratibu na sheria zao bila shuruti. Ujuaji na ubishi utabondwa/ utataabika sana😂😂

Jela ni kubaya, kugumu usijempeleka mtu kwa kumwonea/kumbambikia kesi ni laana. Pia kama kuna kesi yeyote ambayo unahisi itakupeleka jela jitahidi sana mmalizane uraiani usijepelekwa huko.

Mtu anaonesha ubabe mtaani na kusema "jela siogopi nimeshakaa kwani jela kitu gani??" Ujue huyo mjinga hajawahi pelekwa 😂😂😂😂😂

NB: Ni machache niliyojua kwa jela hii na kila jela kuna mambo yake

MWISHO
Kule ni nyumbani kwa wote wakati wowote, omba Mungu akuepushe na kule kuzimu ndogo.
 
Jela jela siyo mchezo watu wanapata mateso kulala kwa marungu ,kula kwa mijeledi ,chechela sege dansi nondo gereza inside ndichi ngombe lupango kunapoteketeza.

Yeyote kumfika hukumu inaweza au mkono wa sheria kidogo kuteleza, wanaokwenda jela siyo wote wana hatia wengine wanakwenda kwa kesi za kusingiziwa....."Hallow afande gewe ebu libambike kesi ya mauaji tupate kidogo kaulaji".
 
Hili hasa ndio la kuzingatia.
Kweli mkuu kule muda wowote unaweza kwenda haijalishi we nimwema kiasi gani!!

Mtu anaweza umia/kufa/ibiwa/bakwa/nyang'anywa katika mazingira yako ambapo wala hukushiriki ila sasa ndo ukawa suspect namba moja, mpaka upelelezi ukamilike si ajabu umesota mahabusu muda Sana au umepigwa namba mazima
 
Kweli mkuu kule muda wowote unaweza kwenda haijalishi we nimwema kiasi gani!!
Mtu anaweza umia/kufa/ibiwa/bakwa/nyang'anywa katika mazingira yako ambapo wala hukushiriki ila sasa ndo ukawa suspect namba moja, mpk upelelezi ukamilike si ajabu umesota mahabusu muda Sana au umepigwa namba mazima
Mungu atunusuru na kila shari.
 
Jela jela siyo mchezo watu wanapata mateso kulala kwa marungu ,kula kwa mijeredi ,chechela sege dansi nondo gereza inside ndichi ngombe lupango kunapoteketeza.

Yeyote kumfika hukumu inaweza au mkono wa sheria kidogo kuteleza, wanaokwenda jela siyo wote wana hatia wengine wanakwenda kwa kesi za kusingiziwa....."Hallow afande gewe ebu libambike kesi ya mauaji tupate kidogo kaulaji".
Kweli mkuu
 
Back
Top Bottom