Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Per Diem

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2018
Posts
2,189
Reaction score
3,724
Moja ya vitu ambavyo sikuwahi kukubaliana navyo ni ile dhana ya kusema eti maisha ya Europe ni ya upweke. Upweke unautengeneza mwenyewe tu, ila ukweli ni kuwa maisha ya Ulaya ni mazuri Sana hasa Norway.

Bongo bado Sana, tusiongopeane na kujipa moyo. Anayeweza kuja aje ashuhudie. Na inapaswa kuwa challenge kwa serikali yetu kujitahidi walau nusu tu ya maisha ya huku. Inawezekana.

Huku public facilities zipo kwa kiwango Cha juu sana, Ni wewe tu kuamua kuenjoy au laa. Wengi huwa hawajui wafanye nini wakifika huku na hivyo kuishia kuona maisha ni magumu, Ila kwa ambao ni hustlers Kama Mimi aisee huku Ni penyewe kabisa.

Kingine ambacho nimekiona Cha tofauti ni huku tulipo hakuna mwizi Wala kibaka. Sasa nikimmbuka kule home nabaki nachoka tu. Usiku inafuga mbwa wakali Ila bado wanajema wanazama ndani na kuiba. Ieleweke, bado naipenda Sana nchi yangu na Sina maana na kuipondea Ila nazungumzia uhalisia naoona kwa macho yangu na si kusimuliwa.

Mimi napenda Sana soccer hivyo Mara mojamoja napopata nafasi huwa nasogea viwanja vya jirani ili kuweza kufanya mazoezi na huwa napata sana positive feedback kutoka kwa naofanya nao, bahati mbaya umri tu umeenda Ila bila hivyo ningetest zali langu huku [emoji1787][emoji1787].

Tuache dhana potofu, Mara zote nimesisitiza watu kuwa positive kwenye maisha, hii itasaidia kukufanya uwe na focus, Ila kila kitu ukichukulia kwa negative basi na matokeo huwa negative.

Chini ni picha za ground napofanya mazoezi.

IMG_20210529_212135_270.JPG
IMG_20210529_212142_112.JPG
 
Nachokipenda kuhusu Ulaya,kila kitu kiko nadhifu na katika mpangilio. Viwanja vya michezo ( kuanzia vya viwango vya juu hadi ngazi a mitaani). Maeneo ya kupumzika, maeneo ya kuchezea watoto,bustani nzuri n.k

Bongo ni aibu, hadi leo hii eti uwanja wa Uhuru hauna taaa kwa ajili ya kucheza mechi za usiku au kufanya mazoezi. Sijui kipaombele chetu ni nini km taifa! Kila kitu kiko ovyoovyo! Shule na vyuo vingi havina kabsa viwanja vya michezo. Shuleni ni kusoma weeee!! hakuna ku-relax. Vipaji vingi vinapotea kizembe zembe huku kilio cha ajira kikitawala na watu wamekalia vipaji vyao.

Nikiwa natembea barabarani huwa najisonya peke angu kwa namna mambo yalivyo. Ni kichefu chefu kitupu!! Mmmxxxxuu!
 
Moja ya vitu ambavyo sikuwahi kukubaliana navyo ni ile dhana ya kusema eti maisha ya Europe ni ya upweke....
Safi sana mkuu. Keep up the spirit!

Najua watu wana-dis kwamba ni ushamba sijui nini na nini ila believe me you are inspiring others. Mimi ni traveller na I have always been an ambassador so people can travel.

Usikatishwe tamaa na watu waliopo negative all the time. Watu watasema tu hata ufanye nini, as long as maneno ya watu hayakufanyi uote mapembe just go on and do what you like (writing about you).

One love and enjoy your moment to the fullest
 
Back
Top Bottom