Ulaya na Marekani kwa upande wangu napendea vitu vitatu tu:
1. Huduma bora za afya. Yaani mtu unaweza kupata shambulizi la kiharusi (stroke) dakika tano ambulance imeshafika ushapigwa MRI tatizo limeshafahamika wanakufungua ubongo mara moja. Na karibu kila hospitali ina uwezo wa kufanya haya maoperesheni magumu hata kama ni kwa dharula.
2. Kutokuwa na rushwa hizi za kijinga. Unahamia kwenye nyumba unapiga simu tu au unalog kwenye mitandao yao unalipa na kila kitu chapu chapu - maji, umeme, mtandao...kila kitu kishafanyika. Yaani unaweza kufanya karibu kila kitu mwenyewe tu tena haraka haraka ushapata huduma. Kinachonichoshaga bongo ni huu utaratibu wa rushwa na nepotism karibu kila sehemu utakayohitaji huduma. Kitu kidogo utazungushwa weee mpaka uchoke.
3. Elimu elimu elimu - hasa kwa sisi wenye watoto....
Mengine yote kwangu huwa simaindi sana kwa sababu huwa naona ni ya kawaida tu. Na nyumbani daima ni nyumbani bana ala!!!