Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Kima Cha chini Cha mshahara wa serikali ni 270,000 Takribani dola 130 kwa mwezi , huo sio utumwa ?

Hizo dola kwa ulaya unaingiza kwa masaa kadhaa tu.
Mambo sio rahisi namna hii ulaya, lazima ufanye kazi kama mtumwa ili utoboe

Wengi wangetajirika
 
Wazungu wana ubaguzi sana dhidi ya ngozi nyeusi, sema labda kama una hulka ya kujikombakomba.....vinginevyo utaboreka zaidi ukilinganisha kuishi na jamii ya weusi wenzako..
Well said!! Ni kipaji icho
 
Hakuna shida yoyote mkuu tena hela ipo nje nje. Nenda tu, ila ninachosema ni hiki KAMA UNA UWEZO WA KUINGIZA PESA YA KUENDESHA MAISHA YAKO BILA MAWAZO NA UMRI UMESOGEA USIENDE. Ila kama maisha yako ya kuungaunga huna famili,umri bado chini ya 30yrs nenda kabahatishe.
Ila kweli kama unaweza kupata m2_5 kwa mwezi unaenda ulaya kufanya nini
 
Nadra sana kunikuta naandika uongo uongo mkuu... hainip ahueni yyt ile .kwani huko nje shida kubwa ni nn? Usinipe habari za upweke sijui kutengwa! Mm ndo maisha yangu yako hvyo ..nipe sababu zingine!
Kinachonisukuma kwenda huko wanalipwa vyema sana..sina kazi nayoishindwa sijui nione kjnyaa nop..sina hizo! Imagine ww unakzania walau kwa mwezi upate faida ya 3m.
Lakini wenzetu hako ni kamshahara ka masiku ..!imagine!
Madam we inaonyesha mpambanaji!!!
 
Nachokipenda kuhusu Ulaya,kila kitu kiko nadhifu na katika mpangilio. Viwanja vya michezo ( kuanzia vya viwango vya juu hadi ngazi a mitaani). Maeneo ya kupumzika, maeneo ya kuchezea watoto,bustani nzuri n.k

Bongo ni aibu, hadi leo hii eti uwanja wa Uhuru hauna taaa kwa ajili ya kucheza mechi za usiku au kufanya mazoezi. Sijui kipaombele chetu ni nini km taifa! Kila kitu kiko ovyoovyo! Shule na vyuo vingi havina kabsa viwanja vya michezo. Shuleni ni kusoma weeee!! hakuna ku-relax. Vipaji vingi vinapotea kizembe zembe huku kilio cha ajira kikitawala na watu wamekalia vipaji vyao.

Nikiwa natembea barabarani huwa najisonya peke angu kwa namna mambo yalivyo. Ni kichefu chefu kitupu!! Mmmxxxxuu!

Wanao tuongoza ni watu ambao ni self-centred, hao hao ndo wanabadili maeneo ya wazi kuwa viwanja vya makazi na mwisho wa siku wanagawana wao. Kwa nje wanaonekana wanatupenda lakini roho zao hapana. Public interest siyo kipaumbele kwao.
 
Mimi nadhani waswahili wengi hapa ndo tuna miss point. Mimi included!

Ok..Ulaya maisha magumu, kazi za box, baridi kali..nk. Lakini bongo maisha yakoje? mtu ameajiliwa anapata mshahara wa laki mbili, read again laki mbili! Hata dola mia haifiki! Professor wa University of Dar es salaam, aliyefundisha zaidi ya miaka 30..hapeleki nyumbani mshahara wa million tano! read again....five million! Pension system ndo hivyo..haieleweki... Kila mwenye ajira serikalini more than 80% wanategemea kuishi kwa ujanja ujanja na virushwa vidogo vidogo....mshahara haukutani na hauwezi kukidhi hata basic needs za mwanadamu! Serikali hata ingepeleka tons and tons za madawa hospitali..hao hao wahusika ndo wanapita mlango wa nyuma kuyauza hayo madawa. Wananchi wengi bongo wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kabisa....uhai hauna thamani tena! Wananchi Tunahusudu siasa za majungu na ujinga kuliko hata wanasiasa wenyewe...

Halafu leo unamshangaa Prof. Kabudi mwanasheria Nguli kafundisha mlimani miaka nenda rudi..anateuliwa uwaziri anamshukuru Rais kumtoa JALALANI? Sasa kama University of Dar ni Jalalani huko halmashauri za Songea na Kigoma si ni chooni kabisa?

Leo unapata wapi courage ya kudharau mtu anayebeba box kwenye winter na kulipwa dola 20 au 30 kwa lisaa (conservative estimates?). Unapata wapi courage ya kudharau watu kwamba wanaosha vyoo au kusafisha barabarani? Kwani kazi maana yake ni nini? Unakuta huyu huyu anayebeba mabox kwenye warehouse...anaishi maisha mazuri yenye kuthamini utu na kusaidia ndugu zake hapa Tanzania! Leo unasema wewe ni engineer bongo..wakati hata calvert za barabara zetu wanajenga fundi mchundo kutoka china? Daktari wa bongo akienda Ulaya hataweza kupractice..itabidi aanze upya..na bado huyo anapata guts za kudharau watu wanaosafisha vyoo ulaya?

Watanzania tuamke! Ndo maana hatuishi kugombana na serikali kwa hivi viajira ambayo hata huwezi kujitunza bila kuiba pesa za wavuja jasho wenzako.....achilia mbali kutunza familia!

Yes, Ulaya au US maisha siyo marahisi. Na wala hakuna sehemu maisha yalipo marahisi. Lakini ukiishi kwa discipline ukapambana..lazima utatoboa. Tatizo wengi wetu akili za umasikini zinatutesa sana. Bado tunaamini kwamba kazi ya maana ni ya kuajiriwa ofisini..hata kama unafanya kazi kwa muhindi unalipwa 150k!

Ushauri wangu..vijana amkeni mpambane. ukipata mchongo wa kwenda popote wewe nenda kafie mbele. Hata ukipata kazi ya ulinzi Syria au Yemeni kwa makampuni ya wamarekani ya ulinzi..nenda..usiogope kufa kwa mabomu. Inawezakana bongo usife kwa mabomu lakini ukafa kwa kugongwa na bajaji ambayo haina bima au kipindupindu!

Tuache negativities watanzania! Tupeane moyo wa kustruggle. Siyo kila anayeenda ulaya atapitia airport na passport na kusindikizwa na familia. au ni msomi anaenda kufanya masters kwa scholarship za wahisani....wengine ni watoto wa masikini. ..Mchongo wa Ulaya inabidi upambane mwenyewe bila baba fisadi wa kukutafutia scholarship za ujanja ujanja!

Imani yangu kubwa...watanzania songeni mbele mkatafute maisha. Hata akina Karl Peters, Livingstone, Columbus na wengine wengi... walitoboa wakaacha comfort zone zao wakaja huku kwetu "kuvumbua" dunia nyingine. Ni kupitia wao nchi zao zilitawala mataifa mengine na kuwa na dola kubwa kiuchumi! Tusiogope kufagia barafu au kusafisha vyoo huko Ulaya. Wengi wametoboa kupitia hizi njia na kazi za fedheha (kama wasomi wetu wa bongo wanavyoziita)

Masanja
Usiongee tena kaka umemaliza, una spirit ya utafutaji na ya ushawishi, positivity!
 
Tukutane abroad mkuu!!!
 
Back
Top Bottom