Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Moja ya vitu ambavyo sikuwahi kukubaliana navyo ni ile dhana ya kusema eti maisha ya Europe ni ya upweke. Upweke unautengeneza mwenyewe tu, ila ukweli ni kuwa maisha ya Ulaya ni mazuri Sana hasa Norway.

Bongo bado Sana, tusiongopeane na kujipa moyo. Anayeweza kuja aje ashuhudie. Na inapaswa kuwa challenge kwa serikali yetu kujitahidi walau nusu tu ya maisha ya huku. Inawezekana.

Huku public facilities zipo kwa kiwango Cha juu sana, Ni wewe tu kuamua kuenjoy au laa. Wengi huwa hawajui wafanye nini wakifika huku na hivyo kuishia kuona maisha ni magumu, Ila kwa ambao ni hustlers Kama Mimi aisee huku Ni penyewe kabisa.

Kingine ambacho nimekiona Cha tofauti ni huku tulipo hakuna mwizi Wala kibaka. Sasa nikimmbuka kule home nabaki nachoka tu. Usiku inafuga mbwa wakali Ila bado wanajema wanazama ndani na kuiba. Ieleweke, bado naipenda Sana nchi yangu na Sina maana na kuipondea Ila nazungumzia uhalisia naoona kwa macho yangu na si kusimuliwa.

Mimi napenda Sana soccer hivyo Mara mojamoja napopata nafasi huwa nasogea viwanja vya jirani ili kuweza kufanya mazoezi na huwa napata sana positive feedback kutoka kwa naofanya nao, bahati mbaya umri tu umeenda Ila bila hivyo ningetest zali langu huku [emoji1787][emoji1787].

Tuache dhana potofu, Mara zote nimesisitiza watu kuwa positive kwenye maisha, hii itasaidia kukufanya uwe na focus, Ila kila kitu ukichukulia kwa negative basi na matokeo huwa negative.

Chini ni picha za ground napofanya mazoezi.

Mie mwenyeji wangu South Africa nilipomkuta kamkatia bima mbwa nilikata tamaa kabisa kama Tz tutakuja walau kuifikia SA
 
Uwe muelewa na wwwe. Yeye kama kaenda awamu hii na analeta mrejesho alichoona huko , shida iko wapi?
Kwani nimesema kuna shida mama?! Nashangaa tu sasa hivi Stori zimekuwa nyingi. Tena mtu mmoja analeta Stori tano hata watu wakimtimua anafungua uzi mwingine.
 
Mkuu tupeane ramani jinsi ya kuingia huko binafsi nna ndoto za kuzamia moja Kati ya Scandinavian nations toka kitambo Mkuu nikiingia huko tu the rest is upon myself coz binafsi ni hastler super so naamini sitakwama Per Diem
Ukute sasa per diem mwenyewe yupo sisi kwa sisi hapo Manzese, Kigogo mwembe Jando, kwa binti Kahenga Luanga au Buza Kwa Lulenge.
 
Kwani nimesema kuna shida mama?! Nashangaa tu sasa hivi Stori zimekuwa nyingi. Tena mtu mmoja analeta Stori tano hata watu wakimtimua anafungua uzi mwingine.
Huyu jamaa alianzaga kwenye ile id yake nyingine akiwa ukraine halafu akafika Norway. Alichoharibu akaposti picha za mtu yuko Helsinki finland akisema yuko Norway. Watu humu jamvini wakamshutukizia wakamsambulia nakumuambia hizo picha ni za Finland siyo Norway. Toka siku iyo kaingia mitini. Sasa hivi kaja vingine
 
Sasa, jamani utalinganishaje social welfare ya Norway na Tanzania. Mbona bado ndio tunatibu makovu ya adhali za ukoloni? Pia ha viongozi bado Ni kizazi Cha mkoloni tu?
 
Back
Top Bottom