Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Maisha ya Ulaya hasa Norway ni mazuri sana, Bongo bado sana

Hahahahaaaaa......mkuu mwache mwenzio akajaribu bahati yake......😃😃😃
Mkuu kuna umri na hali fulani ya maisha ukifikia hapa Bongo ukienda nje kupiga box utaishia kuwa frustrated na utarudi mbio hapa Tz. Nimeshuhudia haya nisemayo. Kule ni kuzuri uende mapema wakati una umri fulani wa kuchakarika na hali yoyote.
 
Nachokipenda kuhusu Ulaya,kila kitu kiko nadhifu na katika mpangilio. Viwanja vya michezo ( kuanzia vya viwango vya juu hadi ngazi a mitaani). Maeneo ya kupumzika, maeneo ya kuchezea watoto,bustani nzuri n.k

Bongo ni aibu, hadi leo hii eti uwanja wa Uhuru hauna taaa kwa ajili ya kucheza mechi za usiku au kufanya mazoezi. Sijui kipaombele chetu ni nini km taifa! Kila kitu kiko ovyoovyo! Shule na vyuo vingi havina kabsa viwanja vya michezo. Shuleni ni kusoma weeee!! hakuna ku-relax. Vipaji vingi vinapotea kizembe zembe huku kilio cha ajira kikitawala na watu wamekalia vipaji vyao.

Nikiwa natembea barabarani huwa najisonya peke angu kwa namna mambo yalivyo. Ni kichefu chefu kitupu!! Mmmxxxxuu!

Very true.
 
Hakuna shida yoyote mkuu tena hela ipo nje nje. Nenda tu, ila ninachosema ni hiki KAMA UNA UWEZO WA KUINGIZA PESA YA KUENDESHA MAISHA YAKO BILA MAWAZO NA UMRI UMESOGEA USIENDE. Ila kama maisha yako ya kuungaunga huna famili,umri bado chini ya 30yrs nenda kabahatishe.
😆😆😆😆!
 
Acha kujidanganya, ukienda huko unakuwa mtumwa wa mfumo na ni vigumu kutoboa kwa ngozi nyeusi. Pesa unayopata inaishia kulipia nyumba na bili za maji, umeme, gesi, hapo inabidi upige vibarua kama mbwa na wakati mwingine kazi za usiku na baridi kali. Kupata kazi kwenye mfumo rasmi wa ajira ni ngumu labda uwe kichwa hasa.....wengi ambao mna wenge mnakuwa hamjawahi kufika, mmepashuhudia ulaya kwenye TV au kusimuliwa na watu kama mleta mada...
Ni kweli mimi sijawahi kufika mkuu.lazima niwe na wenge mkuu .hata hiyo tv sina!
 
Nachokipenda kuhusu Ulaya,kila kitu kiko nadhifu na katika mpangilio. Viwanja vya michezo ( kuanzia vya viwango vya juu hadi ngazi a mitaani). Maeneo ya kupumzika, maeneo ya kuchezea watoto,bustani nzuri n.k

Bongo ni aibu, hadi leo hii eti uwanja wa Uhuru hauna taaa kwa ajili ya kucheza mechi za usiku au kufanya mazoezi. Sijui kipaombele chetu ni nini km taifa! Kila kitu kiko ovyoovyo! Shule na vyuo vingi havina kabsa viwanja vya michezo. Shuleni ni kusoma weeee!! hakuna ku-relax. Vipaji vingi vinapotea kizembe zembe huku kilio cha ajira kikitawala na watu wamekalia vipaji vyao.

Nikiwa natembea barabarani huwa najisonya peke angu kwa namna mambo yalivyo. Ni kichefu chefu kitupu!! Mmmxxxxuu!
Hahahhahaa...ndo maana nasema panachosha sN
 
pointless hata hapa bongo tunabaguana wenyewe kwa wenyewe.wenye nacho anambagua asiekua nacho na mwenye position flan anamdharau wa chini.bora uonekani mbwa ulaya ukitafuta maisha bora.kuliko kubaki tz ukiitwa mnyonge ukiwa kwenye ajira tembo mshahara sungura.
Naudhika sana kuskia habari za kubaguliwa..kwan ukinibagua mm nakonda nn? Argh
 
Mkuu kuna umri na hali fulani ya maisha ukifikia hapa Bongo ukienda nje kupiga box utaishia kuwa frustrated na utarudi mbio hapa Tz. Nimeshuhudia haya nisemayo. Kule ni kuzuri uende mapema wakati una umri fulani wa kuchakarika na hali yoyote.
Mkuu ingefaa ungewapa vijana muongozo wa umri ili wenyewe wajitafakari........
 
Moja ya vitu ambavyo sikuwahi kukubaliana navyo ni ile dhana ya kusema eti maisha ya Europe ni ya upweke. Upweke unautengeneza mwenyewe tu, ila ukweli ni kuwa maisha ya Ulaya ni mazuri Sana hasa Norway.

Bongo bado Sana, tusiongopeane na kujipa moyo. Anayeweza kuja aje ashuhudie. Na inapaswa kuwa challenge kwa serikali yetu kujitahidi walau nusu tu ya maisha ya huku. Inawezekana.

Huku public facilities zipo kwa kiwango Cha juu sana, Ni wewe tu kuamua kuenjoy au laa. Wengi huwa hawajui wafanye nini wakifika huku na hivyo kuishia kuona maisha ni magumu, Ila kwa ambao ni hustlers Kama Mimi aisee huku Ni penyewe kabisa.

Kingine ambacho nimekiona Cha tofauti ni huku tulipo hakuna mwizi Wala kibaka. Sasa nikimmbuka kule home nabaki nachoka tu. Usiku inafuga mbwa wakali Ila bado wanajema wanazama ndani na kuiba. Ieleweke, bado naipenda Sana nchi yangu na Sina maana na kuipondea Ila nazungumzia uhalisia naoona kwa macho yangu na si kusimuliwa.

Mimi napenda Sana soccer hivyo Mara mojamoja napopata nafasi huwa nasogea viwanja vya jirani ili kuweza kufanya mazoezi na huwa napata sana positive feedback kutoka kwa naofanya nao, bahati mbaya umri tu umeenda Ila bila hivyo ningetest zali langu huku [emoji1787][emoji1787].

Tuache dhana potofu, Mara zote nimesisitiza watu kuwa positive kwenye maisha, hii itasaidia kukufanya uwe na focus, Ila kila kitu ukichukulia kwa negative basi na matokeo huwa negative.

Chini ni picha za ground napofanya mazoezi.

Hivi huchoki na mapicha yako ya kudownload?!!! Utaacha lini ujinga huu!!!

Kama umeyapatia huko ni yako. Naamini una ndugu jamaa na marafiki unaowajua na ambao unaweza kuwapa msaada wa kufika huko na kufanikiwa zaidi kuliko kushinda kujomwambafai nyuma ya batan za simu humu Jf kwa ambao hutujui halafu tuna hamsini zetu . Acha ushamba.
 
Inategemea na mtu na mtu kwa sababu hatufanani. Kwangu mimi nyumbani ni nyumbani tu; na duniani huko huwa nakwenda tu kuosha macho na kurudi. Ni uamuzi tu nadhani; malengo ya mtu na anavyoyachukulia maisha [emoji1545][emoji1545]
Inategemea na mtu na sehemu ulipokwenda wengine wao wanapenda kukaa nyumbani na wengine kutoka kwenda nje!!
 
Naudhika sana kuskia habari za kubaguliwa..kwan ukinibagua mm nakonda nn? Argh
Mara nyingi maneno haya unayoandika yanatoka kwa mtu ambae hajaishi kwenye mazingira ya ubaguzi wa rangi. Vitu vingine ni vigumu kuelezewa ukaelewa ni mpaka uishi navyo ndio utajua athari zake na kwanini dunia nzima inaongelea racism.
#BlackLivesMatter
 
Mkuu anadanganya hivyo halafu anawapata vijana wako desperate wanafuata pm kumuomba awasaidie. Atawajibu yeye hawezi lakini ana jamaa yake yuko Dar ambaye ndio yeye. Atakuitisha Million 7 akusaidie michongo ya norway. Kashawapiga wawili na mmoja ni mdogo wangu. Nilimuonya dogo hakunisikia
Mdogo wako kamtumia 7m?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Ujana unaishia 35yrs. Ila kwa maoni yangu umri mzuri ni chini ya 30yrs na uwe huna familia.
Tena ukiwa 25 ni poa kabisa, unafanya maisha yako huko huko hadi kuoa....unauzoea mfumo wa maisha ya huko tangu ukiwa kijana.
 
Acha kujidanganya, ukienda huko unakuwa mtumwa wa mfumo na ni vigumu kutoboa kwa ngozi nyeusi. Pesa unayopata inaishia kulipia nyumba na bili za maji, umeme, gesi, hapo inabidi upige vibarua kama mbwa na wakati mwingine kazi za usiku na baridi kali. Kupata kazi kwenye mfumo rasmi wa ajira ni ngumu labda uwe kichwa hasa.....wengi ambao mna wenge mnakuwa hamjawahi kufika, mmepashuhudia ulaya kwenye TV au kusimuliwa na watu kama mleta mada...
Lakini mbona wabeba box wengine wengi wametoboa huko?

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom