Acha kujidanganya, ukienda huko unakuwa mtumwa wa mfumo na ni vigumu kutoboa kwa ngozi nyeusi. Pesa unayopata inaishia kulipia nyumba na bili za maji, umeme, gesi, hapo inabidi upige vibarua kama mbwa na wakati mwingine kazi za usiku na baridi kali. Kupata kazi kwenye mfumo rasmi wa ajira ni ngumu labda uwe kichwa hasa.....wengi ambao mna wenge mnakuwa hamjawahi kufika, mmepashuhudia ulaya kwenye TV au kusimuliwa na watu kama mleta mada...
Mimi nadhani waswahili wengi hapa ndo tuna miss point. Mimi included!
Ok..Ulaya maisha magumu, kazi za box, baridi kali..nk. Lakini bongo maisha yakoje? mtu ameajiliwa anapata mshahara wa laki mbili, read again laki mbili! Hata dola mia haifiki! Professor wa University of Dar es salaam, aliyefundisha zaidi ya miaka 30..hapeleki nyumbani mshahara wa million tano! read again....five million! Pension system ndo hivyo..haieleweki... Kila mwenye ajira serikalini more than 80% wanategemea kuishi kwa ujanja ujanja na virushwa vidogo vidogo....mshahara haukutani na hauwezi kukidhi hata basic needs za mwanadamu! Serikali hata ingepeleka tons and tons za madawa hospitali..hao hao wahusika ndo wanapita mlango wa nyuma kuyauza hayo madawa. Wananchi wengi bongo wanakufa kwa magonjwa yanayotibika kabisa....uhai hauna thamani tena! Wananchi Tunahusudu siasa za majungu na ujinga kuliko hata wanasiasa wenyewe...
Halafu leo unamshangaa Prof. Kabudi mwanasheria Nguli kafundisha mlimani miaka nenda rudi..anateuliwa uwaziri anamshukuru Rais kumtoa JALALANI? Sasa kama University of Dar ni Jalalani huko halmashauri za Songea na Kigoma si ni chooni kabisa?
Leo unapata wapi courage ya kudharau mtu anayebeba box kwenye winter na kulipwa dola 20 au 30 kwa lisaa (conservative estimates?). Unapata wapi courage ya kudharau watu kwamba wanaosha vyoo au kusafisha barabarani? Kwani kazi maana yake ni nini? Unakuta huyu huyu anayebeba mabox kwenye warehouse...anaishi maisha mazuri yenye kuthamini utu na kusaidia ndugu zake hapa Tanzania! Leo unasema wewe ni engineer bongo..wakati hata calvert za barabara zetu wanajenga fundi mchundo kutoka china? Daktari wa bongo akienda Ulaya hataweza kupractice..itabidi aanze upya..na bado huyo anapata guts za kudharau watu wanaosafisha vyoo ulaya?
Watanzania tuamke! Ndo maana hatuishi kugombana na serikali kwa hivi viajira ambayo hata huwezi kujitunza bila kuiba pesa za wavuja jasho wenzako.....achilia mbali kutunza familia!
Yes, Ulaya au US maisha siyo marahisi. Na wala hakuna sehemu maisha yalipo marahisi. Lakini ukiishi kwa discipline ukapambana..lazima utatoboa. Tatizo wengi wetu akili za umasikini zinatutesa sana. Bado tunaamini kwamba kazi ya maana ni ya kuajiriwa ofisini..hata kama unafanya kazi kwa muhindi unalipwa 150k!
Ushauri wangu..vijana amkeni mpambane. ukipata mchongo wa kwenda popote wewe nenda kafie mbele. Hata ukipata kazi ya ulinzi Syria au Yemeni kwa makampuni ya wamarekani ya ulinzi..nenda..usiogope kufa kwa mabomu. Inawezakana bongo usife kwa mabomu lakini ukafa kwa kugongwa na bajaji ambayo haina bima au kipindupindu!
Tuache negativities watanzania! Tupeane moyo wa kustruggle. Siyo kila anayeenda ulaya atapitia airport na passport na kusindikizwa na familia. au ni msomi anaenda kufanya masters kwa scholarship za wahisani....wengine ni watoto wa masikini. ..Mchongo wa Ulaya inabidi upambane mwenyewe bila baba fisadi wa kukutafutia scholarship za ujanja ujanja!
Imani yangu kubwa...watanzania songeni mbele mkatafute maisha. Hata akina Karl Peters, Livingstone, Columbus na wengine wengi... walitoboa wakaacha comfort zone zao wakaja huku kwetu "kuvumbua" dunia nyingine. Ni kupitia wao nchi zao zilitawala mataifa mengine na kuwa na dola kubwa kiuchumi! Tusiogope kufagia barafu au kusafisha vyoo huko Ulaya. Wengi wametoboa kupitia hizi njia na kazi za fedheha (kama wasomi wetu wa bongo wanavyoziita)
Masanja