Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Ila ukipata demu wa Uswazi aliyetoboa anakuwa mshamba kishenzi, kila akifanyacho anajibandika mtandaoni ili wenzake waone kapata mfano wa hawa mademu (Kajala, Aunt Ezekiel, Hamisa Mobeto, Giggy Money).

Kwa aunt ezekieli huo ni uwongo asilimia zote mfwatilie utaona kwenye account yake imejaa matangazo na home kwake ana kaa na familia yake yule ana hishi ki africa sio kistaa kama wengine

Huwezi kumkuta sehemu za ovyo ovyo pia ni muungwana theni hawezi kuongea sana unajua kwanini aliacha kuigiza tamthilia ya mama kimbo?
 
SISI TUSHAZOEA MAISHA HAYO,KULA PEMBEZONI WA CHOO,KULALA BARAZANI NA BOXER,HUYU ANASIKILIZA TAARABU,HUYU ANACHEKI MOVIE YANI KELELE HADI RAHA,KUMTONGOZA MAMA MWENYE NYUMBA ILI AKPUNGUZIE KODI,NYIE WATOTO WA KISHUA ACHENI KUJA USWAZI HUKU HAKUWAFAI HIVI ULISHAWAHI KULA UGALI NA CHUMVI??
Miguu ya kuku na utumbooo, mia mia uswazi raha sanaa.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wengi mmeongopa sana kuhusu uswazi au neno uswazi halijaeleweka kwenu .

Eti uswazi ukute kimba chooni ? Nop wadanganye wa kwenu .

Eti uswazi wana style zao za kunyoa hasa vijana ? Acha uongo uswazi unyoaji wengi uwafuatisha wasanii

Eti uswazi sijui bla bla gani , punguzeni kukariri maisha wakati wengine mmetoka huko vijijini mnakunya kwenye misitu leo mnajifanya kuyashangaa maisha ya uswazi .

Sifa za uswazi ni hizi .

Mazoea yaliyopita mipaka kwa watu wake .

Matusi kwa rika zote si babu wala bibi .

Maisha ya bei za chini sana mfano kupata sukari ya mia .

Watu kuishi chini ya dollar ila maisha yanaenda .

Uchawi hasa kwenye viduka vyao yaani tunaita chuma ulete.

Watu wa huko kupenda masherehe yasiyokwisha tunaita shughuli .

Elimu kwa watoto wa kule sio kipaumbele kwa wazazi .

Ukabaji na wizi uliokithiri .

Kujiita majina ya wasanii wa mbele mara Fatuma kuitwa Fetty Rish .

Kupata vitu vya ndani kwa bei za chini kupita kawaida .

Uwepo wa watu ambao ni wababe wa mtaa yaani unaweza ibiwa usiku asubuhi ukaripoti kwa hawa wababe na ukapata mali yako safi .

Uswazi hakuna mtu atakuuliza unafanya kazi gani ? Zaidi usiwe mtu official sana kimavazi sababu watakuita wa kishua na pia watakuhisi ni usalama sababu hiyo kazi sio mtoto wala mkubwa wote wanaijua .

Uswazi kila ukipiga story na watu wa huko si ajabu kila mtu kukuambia ana nduguye ni afisa usalama

Uswazi sio polisi wala baka baka yaani wajeda hawaogopwi na pia wanakaa vijiweni kula story na wana mtaa ikabidi hata ganja wanavuta wote
Cc .keko magereza na askari wake hasa vijana .

Uswazi hawaogopi cheo chako ila wanaogopa hela yako kwa msemo wa dolari zako tu .

Uswazi kila familia ina ndugu alizamia nje hajarudi mpaka leo .

Uswazi kwa dar wengi ni waislamu isipokuwa wachache sana hasa watu kuja waliowahi mjini zama zile

Uswazi ishi na rika zote vizuri hutajutia ila ukijitia huna muda na wana mtaa huwezi kuendelea utaibiwa mpaka ukome

Uswazi si ajabu choo kimoja kutumika na nyumba tatu kwa mpigo na ratiba ya usafi inazihusu nyumba zote .

Ukifika uswazi usikubali kusema unatoka mkoa gani sema ni wa dar utaheshimika kiasi chake ila kujitabanaisha mkoa utokao wao uanza kukuhisi wewe ni mshamba .

Oya jamani dar asilimia 80% ni uswazi japo kila sehemu inatofautiana uswahili wake hivyo msijipe presha wengi wenu mnaishi uswahilini tu ila hamjajua tu.

Haya nayaeleza kupitia exprience yangu huko KEKO, TANDIKA , TEMEKE na kwingineko katika viunga vya jiji la dasalam

Wale wa Masaki tukutane hapa tukumbushane enzi.
Kwani maeneo gani wajeda wanaogopwa??
 
Mpaka sasa hakuna hata mmoja anayeishi uswazi amekomenti. Sawa washua

Yote mmeongea mko sahihi kwa kifupi maisha ya huku ukija mgeni unaweza kusema kama tunaigiza lakini ndio siku zinasonga

Vigoma vya kanga moko vya uruguai ndo pake Mwanaidi ananyanyua dela kichupi njenje watoto wanafurahi wahuni tunabambia usiombe liwe linapigwa dundo la Balaa MC mzuka huo
 
umenikumbusha bro!
Kuna siku nilikuwuwa na dem hela ya gesti iliunganishwa jwa malipo ya demu hivyo tukaenda kwenye machaka ya makaburini!
Wakati nakula mzigo akaja msera akaa pembeni kidogo sana akaanza kuvuta bange!
Nikamwambia demu tuhame, akasema nikiinuka silali tena nasepa!
Nikaona isiwe tabu....
Yule msela Akaanza kuinuiza, bange nipe nguvu sitaki ujinga, firauni alikojoa pakaota mmea mtakatifu ukaitwa bange, anaesema bange haramu haramu yeye na mamake!......
Uswazi kwetu!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Waswahili wanaishi maisha ya amani sana kwasababu hawataki makubwa,wameridhika na wanaishi kwa kutegemeana.

Hata wewe leo hii ukiridhika na kutonia makuu utaishi maisha ya amani na furaha. Ukifuatilia utafahamu kwamba watu wa mwambao huishi maisha marefu zaidi. Kuna sababu zake...

Chanzo kikubwa cha sonona, msongo wa mawazo, ukosefu wa furaha na magonjwa mengine ya akili ni tamaa ya pesa na kutamani mambo makubwa kuliko uwezo wako.

Mtu halali kabisa kisa Apartment Upanga, I-Phone mpya, BMW, Lotion yenye SPF, Brazilian Hair na mengineyo. Yuko radhi hata aue binadamu mwenzake, au kumuibia na kumtapeli ili avipate....
 
Back
Top Bottom