Wengi mmeongopa sana kuhusu uswazi au neno uswazi halijaeleweka kwenu .
Eti uswazi ukute kimba chooni ? Nop wadanganye wa kwenu .
Eti uswazi wana style zao za kunyoa hasa vijana ? Acha uongo uswazi unyoaji wengi uwafuatisha wasanii
Eti uswazi sijui bla bla gani , punguzeni kukariri maisha wakati wengine mmetoka huko vijijini mnakunya kwenye misitu leo mnajifanya kuyashangaa maisha ya uswazi .
Sifa za uswazi ni hizi .
Mazoea yaliyopita mipaka kwa watu wake .
Matusi kwa rika zote si babu wala bibi .
Maisha ya bei za chini sana mfano kupata sukari ya mia .
Watu kuishi chini ya dollar ila maisha yanaenda .
Uchawi hasa kwenye viduka vyao yaani tunaita chuma ulete.
Watu wa huko kupenda masherehe yasiyokwisha tunaita shughuli .
Elimu kwa watoto wa kule sio kipaumbele kwa wazazi .
Ukabaji na wizi uliokithiri .
Kujiita majina ya wasanii wa mbele mara Fatuma kuitwa Fetty Rish .
Kupata vitu vya ndani kwa bei za chini kupita kawaida .
Uwepo wa watu ambao ni wababe wa mtaa yaani unaweza ibiwa usiku asubuhi ukaripoti kwa hawa wababe na ukapata mali yako safi .
Uswazi hakuna mtu atakuuliza unafanya kazi gani ? Zaidi usiwe mtu official sana kimavazi sababu watakuita wa kishua na pia watakuhisi ni usalama sababu hiyo kazi sio mtoto wala mkubwa wote wanaijua .
Uswazi kila ukipiga story na watu wa huko si ajabu kila mtu kukuambia ana nduguye ni afisa usalama
Uswazi sio polisi wala baka baka yaani wajeda hawaogopwi na pia wanakaa vijiweni kula story na wana mtaa ikabidi hata ganja wanavuta wote
Cc .keko magereza na askari wake hasa vijana .
Uswazi hawaogopi cheo chako ila wanaogopa hela yako kwa msemo wa dolari zako tu .
Uswazi kila familia ina ndugu alizamia nje hajarudi mpaka leo .
Uswazi kwa dar wengi ni waislamu isipokuwa wachache sana hasa watu kuja waliowahi mjini zama zile
Uswazi ishi na rika zote vizuri hutajutia ila ukijitia huna muda na wana mtaa huwezi kuendelea utaibiwa mpaka ukome
Uswazi si ajabu choo kimoja kutumika na nyumba tatu kwa mpigo na ratiba ya usafi inazihusu nyumba zote .
Ukifika uswazi usikubali kusema unatoka mkoa gani sema ni wa dar utaheshimika kiasi chake ila kujitabanaisha mkoa utokao wao uanza kukuhisi wewe ni mshamba .
Oya jamani dar asilimia 80% ni uswazi japo kila sehemu inatofautiana uswahili wake hivyo msijipe presha wengi wenu mnaishi uswahilini tu ila hamjajua tu.
Haya nayaeleza kupitia exprience yangu huko KEKO, TANDIKA , TEMEKE na kwingineko katika viunga vya jiji la dasalam
Wale wa Masaki tukutane hapa tukumbushane enzi.