Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

kipimo cha uswazi ni kelele , pilikapilika ya watu mara huyu kapita huku mara yule kule, wanawake wanavaa madelaa, duka flani linauzwa sigara hadi panadol, nyumba hazijapangiliwa , vijana na syltle zao za nywele, unamka asubuhi unarudi jion vijana wapo tu wanakula story za mafanikio na watu waliofanikiwa wanazungumzwa sana huko na hatari kuliko zote ni videmu vya huko ukipiga mtupo huru tu kesho unamka na UTI, ila pamoja na shida zote hizo uswaz ni sehemu ya watu wenye furaha na wengi wana vipaji vya asil
Mkuu ukipazoea utapaona kawaida tu, sisi kwetu hatuja kulia Uswahili wala uraiani tokea wadogo sasa mzee wetu akastaafu serikalini tukaamia sinza kipindi hicho tupo wadogo miaka 20 hatuja vuta, kuna vitu tulikuwa tuna vishangaa kimoja tulikuwa hatuja vizoea ni watu kupita pita mpaka saa 4 ndiyo wanaisha kupita na Sinza kipindi hicho siyo uswahilini sana lakini sisi tulikuwa tunashangaa mbona watu wengi kuanzia saa kumi na mbili jioni, lakini baadae tuka zoea tukaona kawaida, na wewe ukienda kuishi uswahilini utakuja kupa zoea.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Kama kijana mpambananaji mwenye focus kaa mbali na wanawake wana mikosi Sana haya Mambo Nina ushahidi nayo uswahilini uchawi unatisha.
Kaka kwahiyo wanawake wa mbezi beach kwa zena kawawa hawana mikosi?????Au oyster bay hakuna uchawi??????Tufafanulie kidogo kaka maana sisi mafanikio yetu ya kimaisha tumeyapatia uswahilini kaka!!!
 
Habari za mchana,

Maisha ya uswahili sio poa poa kama hujayazoea unaweza pata shida sana kuna.

Kuna kipindi nilienda kwa Azizi Ally kumsalimia mtu huko sasa kufika pale tunapiga story gafla kaingia mtu hila hodi anatoa taarifa nachukua mboga kule nini ugali kidogo nilishangaa ase akaona pembeni kuna matunda akabeba.

Ikabidi nimuulize mwenyeji wangu hivi huku ndio maisha gani haya mnaishi mtu anaingia kama kwake anachukua vitu kiholela holela why akawa anacheka.

Siulizi kwa ubaya hila nataka kujua hizo tabia za kienyeji zinatokaga wapi?
Maisha ya uswazi raha sana ikiwa utayakubali mzee baba.
 
Ukiridhika na maisha ya uswahilini..you're done..unaukaribisha umasikini

Uswahilini iwe kama stepping stone kipindi cha kujitafuta ili mambo yakikaa fresh unahamia sehemu zilizotulia lakini kamwe usiridhike na kuishi uswazi
 
Back
Top Bottom