Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Ila ukipata demu wa Uswazi aliyetoboa anakuwa mshamba kishenzi, kila akifanyacho anajibandika mtandaoni ili wenzake waone kapata mfano wa hawa mademu (Kajala, Aunt Ezekiel, Hamisa Mobeto, Giggy Money).

Kwa aunt ezekieli huo ni uwongo asilimia zote mfwatilie utaona kwenye account yake imejaa matangazo na home kwake ana kaa na familia yake yule ana hishi ki africa sio kistaa kama wengine

Huwezi kumkuta sehemu za ovyo ovyo pia ni muungwana theni hawezi kuongea sana unajua kwanini aliacha kuigiza tamthilia ya mama kimbo?
 
Miguu ya kuku na utumbooo, mia mia uswazi raha sanaa.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwani maeneo gani wajeda wanaogopwa??
 
Mpaka sasa hakuna hata mmoja anayeishi uswazi amekomenti. Sawa washua

Yote mmeongea mko sahihi kwa kifupi maisha ya huku ukija mgeni unaweza kusema kama tunaigiza lakini ndio siku zinasonga

Vigoma vya kanga moko vya uruguai ndo pake Mwanaidi ananyanyua dela kichupi njenje watoto wanafurahi wahuni tunabambia usiombe liwe linapigwa dundo la Balaa MC mzuka huo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Waswahili wanaishi maisha ya amani sana kwasababu hawataki makubwa,wameridhika na wanaishi kwa kutegemeana.

Hata wewe leo hii ukiridhika na kutonia makuu utaishi maisha ya amani na furaha. Ukifuatilia utafahamu kwamba watu wa mwambao huishi maisha marefu zaidi. Kuna sababu zake...

Chanzo kikubwa cha sonona, msongo wa mawazo, ukosefu wa furaha na magonjwa mengine ya akili ni tamaa ya pesa na kutamani mambo makubwa kuliko uwezo wako.

Mtu halali kabisa kisa Apartment Upanga, I-Phone mpya, BMW, Lotion yenye SPF, Brazilian Hair na mengineyo. Yuko radhi hata aue binadamu mwenzake, au kumuibia na kumtapeli ili avipate....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…