Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Maisha ya uswahili kama hujayazoea unaweza pata shida

Ukitaka ufurahie vizuri maisha ya uswazi uwe mtu wa akili ndogo, upeo mdogo na mwenye kuridhika mapema na maisha madogo.
Uishie darasa la.3, uwe na nyumba mbovu, uwe na watoto wadogo wengi!; ukitaka kujua hesabu yao asubùhi hesabu vifungu vya mavi!; awe mchawi wa kienyeji, awe na majungu na mmbeya, awe na wake wengj, awe na mshipa......
 
Kipindi bado najitafuta miaka ya nyuma kidogo nilikua napenda sana kuishi uswazi maana hakuna anaenifuatilia ila ukizoea kule ebhana dah maisha ya kawaida unayaona magumu.

Ilifika stage nikawa nalala mlango wazi muda wote usiku nakula bhange na hakuna kenge alikua anasogelea mlango ila nikaja kubadilika bi mkubwa alikuja kunitembelea akanishauri kukaa kule ni kujipotezea malengo hapo ndipo nikastuka na kuyaaga maisha ya uswazi
Ukiwa uswazi, ulikua unavuta bange, ila baada ya kuhamia uzunguni Bange umeaacha.
 
HV keko nako uswazi mm ninaishi hapo japo nhc napaenda San ila kutoka mitaa chache uingiie mitaa Ni balaa tupu Ni uhuni na kushinda na Madera bila chupi

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
Keko kwa kiasi kikubwa ni uswazi mkuu,
Labda huo upande wa nhc hadi maduka mawili kuna mitaa mizuri, middle class kabisa ila hii zone inayotokea hadi mitaa ya kurasini ni 🔥🔥🔥
 
Habari za mchana,

Maisha ya uswahili sio poa poa kama hujayazoea unaweza pata shida sana.

Kuna kipindi nilienda kwa Azizi Ally kumsalimia mtu huko sasa kufika pale tunapiga story gafla kaingia mtu hila hodi anatoa taarifa nachukua mboga kule nini ugali kidogo nilishangaa ase akaona pembeni kuna matunda akabeba.

Ikabidi nimuulize mwenyeji wangu hivi huku ndio maisha gani haya mnaishi mtu anaingia kama kwake anachukua vitu kiholela holela why akawa anacheka.

Siulizi kwa ubaya hila nataka kujua hizo tabia za kienyeji zinatokaga wapi?
Uswazi watu wanaishi kijamaa... ukisikia ujamaa ndio huo sasa
 
uun
Wengi mmeongopa sana kuhusu uswazi au neno uswazi halijaeleweka kwenu .

Eti uswazi ukute kimba chooni ? Nop wadanganye wa kwenu .

Eti uswazi wana style zao za kunyoa hasa vijana ? Acha uongo uswazi unyoaji wengi uwafuatisha wasanii

Eti uswazi sijui bla bla gani , punguzeni kukariri maisha wakati wengine mmetoka huko vijijini mnakunya kwenye misitu leo mnajifanya kuyashangaa maisha ya uswazi .

Sifa za uswazi ni hizi .

Mazoea yaliyopita mipaka kwa watu wake .

Matusi kwa rika zote si babu wala bibi .

Maisha ya bei za chini sana mfano kupata sukari ya mia .

Watu kuishi chini ya dollar ila maisha yanaenda .

Uchawi hasa kwenye viduka vyao yaani tunaita chuma ulete.

Watu wa huko kupenda masherehe yasiyokwisha tunaita shughuli .

Elimu kwa watoto wa kule sio kipaumbele kwa wazazi .

Ukabaji na wizi uliokithiri .

Kujiita majina ya wasanii wa mbele mara Fatuma kuitwa Fetty Rish .

Kupata vitu vya ndani kwa bei za chini kupita kawaida .

Uwepo wa watu ambao ni wababe wa mtaa yaani unaweza ibiwa usiku asubuhi ukaripoti kwa hawa wababe na ukapata mali yako safi .

Uswazi hakuna mtu atakuuliza unafanya kazi gani ? Zaidi usiwe mtu official sana kimavazi sababu watakuita wa kishua na pia watakuhisi ni usalama sababu hiyo kazi sio mtoto wala mkubwa wote wanaijua .

Uswazi kila ukipiga story na watu wa huko si ajabu kila mtu kukuambia ana nduguye ni afisa usalama

Uswazi sio polisi wala baka baka yaani wajeda hawaogopwi na pia wanakaa vijiweni kula story na wana mtaa ikabidi hata ganja wanavuta wote
Cc .keko magereza na askari wake hasa vijana .

Uswazi hawaogopi cheo chako ila wanaogopa hela yako kwa msemo wa dolari zako tu .

Uswazi kila familia ina ndugu alizamia nje hajarudi mpaka leo .

Uswazi kwa dar wengi ni waislamu isipokuwa wachache sana hasa watu kuja waliowahi mjini zama zile

Uswazi ishi na rika zote vizuri hutajutia ila ukijitia huna muda na wana mtaa huwezi kuendelea utaibiwa mpaka ukome

Uswazi si ajabu choo kimoja kutumika na nyumba tatu kwa mpigo na ratiba ya usafi inazihusu nyumba zote .

Ukifika uswazi usikubali kusema unatoka mkoa gani sema ni wa dar utaheshimika kiasi chake ila kujitabanaisha mkoa utokao wao uanza kukuhisi wewe ni mshamba .

Oya jamani dar asilimia 80% ni uswazi japo kila sehemu inatofautiana uswahili wake hivyo msijipe presha wengi wenu mnaishi uswahilini tu ila hamjajua tu.

Haya nayaeleza kupitia exprience yangu huko KEKO, TANDIKA , TEMEKE na kwingineko katika viunga vya jiji la dasalam

Wale wa Masaki tukutane hapa tukumbushane enzi.
aisee unaweza fananinisha maisha ya uswazi na kijijini, labda vijijii vya mtwara na usukumani, vijijini maisha ni matamu mzee ,mtu anaishi eneo kubwa, anajinafasi , huduma zote za msingi zipo maji, umeme, usafiri na uhakika wa kula mara tatu, vijiji kuna umoja na ukaribu, vijana wanakuzwa na tabia ya upambanaji na kutafta riziki, kijijni kila mtu ana kazi , yaani niishi mazense, mbagala nijione mjanja kwa lipi ,
 
Ila watu wa uswaz wana pesa na furaha kila wakati na ni wakarimu kati yao. Japo hilo lifestyle lao siliwezi
Tuna nyumba ya urithi vingunguti weeee...acha[emoji23]maisha ya kule twayaweza wenyewe though kwa Sasa sidhani km ntaweza Tena kuishi kule Yani Kuna balaa sio dog kuanzia j5 vigoma
 
Nilikuwa natafuta chumba maeneo ya morocco duh nikapelekwa huko ambapo chumba bei rahisi hila sasa pamekaa kichafu sana theni watu wamekaa vibalazani wote wanakushangaa wewe
Kuna kinondoni moscow,pale B katikati na nyuma ya mahakama nuksi yaani palivyo weeee....zaidi ya uswazi pachafuuuu afu nyumba za hovyoooo mnooo
 
Ukiridhika na maisha ya uswahilini..you're done..unaukaribisha umasikini

Uswahilini iwe kama stepping stone kipindi cha kujitafuta ili mambo yakikaa fresh unahamia sehemu zilizotulia lakini kamwe usiridhike na kuishi uswazi
There you are,sahihi kabisaa,ni kwetu pamenikuza ila nshahama nimezaliwa uswazi nimekulia uswazi niliitwa msomi wa mtaa
 
Back
Top Bottom