Samico Tanzania
JF-Expert Member
- Feb 6, 2022
- 791
- 1,852
Maisha ya uswahilini ukiwa mgeni huwezi kuelewa wanaishi au wanatania.
Umekaa zako tu vizuri chumbani kwako unasikia inje dirishani kwako minong'ono ya watu wakitongozana laivu
Hujakaa vizuri unaona wapita njia wanapita barazani kwenu hawana hata habari wanakatiza tu popote njia
Unabandika maharage yako inje bila hata aibu unakuta jirani kashayaipua akichota mkaa akakolezee kwake!
Ukiwa unajiandaa kufua paap jirani utaona kashadamka mapema kaanika nguo zake kwenye kamba yako na wala haulizi
Ukiacha malapa inje unakuta jirani kashayavaa na yamekatika na wala usitegemee kuombwa msamaha
Yaaani uswahili maisha yake ni ya kipekee yanahitaji moyo tu kwakweli