Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Habari za leo!
1. Kutafuta mtaji ni kazi ngumu sana.
2. Kuendesha biashara ikasimama ni kazi ngumu sana. Inahitaji uvuje jasho na uwe mstahimilivu.
3. Najua uchungu wa kuibiwa biashara na kuvunjiwa biashara uliyoisotea kwa miaka na miaka.
4. Kwa kujua hilo ndio maana tunawapa pole wale waliovunjiwa biashara zao na wahalifu wakati wa maandamano.
5. Lakini hata uwe na biashara uliyoijenga miaka elfu moja. Uliyovuja jasho miaka nenda rudi.
6. Biashara yako haiwezi kutosha thamani ya maisha hata ya mtu mmoja.
7. Maisha ya mtu yanathamani kuliko kitu chochote katika huu ulimwengu.
8. Yesu alisema, itakufaa nini upewe ulimwengu mzima alafu ukapoteza maisha yako?
9. Kabla ya kilichotokea juzi. Miezi kadhaa iliyopita pale kariakoo kuna jengo lilikuwa linaungua kama sio kuanguka.
10. Alipoulizwa yule mmiliki anamaoni gani yeye alisema kwa kifupi kuwa Mali zinatafutwa lakini sio uhai wa mtu. Ingawaje alikuwa ameumia lakini alimshukuru Mungu sana kwa sababu yeye yupo ila kilichoungua ni ghorofa tuu.
11. Kazi namba moja ya Dola thabiti ni kulinda Maisha ya watu. Maisha ya mtu mmoja kwa serikali thabiti yanathamani kuliko mali au ghorofa lolote hapa duniani.
12. Ni uchochezi kulinganisha maisha ya watu na biashara.
13. Wenzako wamepoteza maisha wewe unakuja na biashara. Really?
14. Ni hatua ya juu ya hatari kwa jamii kuanza kuthamini mali kuliko utu na maisha ya watu.
15. Katika mapambano yoyote ni muhimu kuzingatia zaidi kuokoa na kulinda roho za watu kuliko kitu chochote.
17. Kutothamini na kuheshima uhai wa mtu mwingine ni kuruhusu maisha ya mwituni katika jamii. Maisha ya kinyama.
18. Hata mtu afanye kosa gani, maisha yake yanathamani. Lazima yalindwe na yaheshimiwe na hata kama kuna adhabu za kifo lazima taratibu zifuatwe.
19. Ndugu zangu Watanzania. Bado tuko na nafasi ya kuwekana sawa.
20. Tunafanya kazi na biashara kuokoa, kuyahifadhi na kulinda maisha ya watu.
Ni muhimu kuyaangalia haya.
Linda maisha ya watu wako.
Huko ndio kulinda nchi yako na mali zake.
Acha nipumzike sasa.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam