Maisha yako hivi Ulaya na Marekani

Maisha yako hivi Ulaya na Marekani

Huku familia maskini kupata 40,000 ya TASAF wanaenda kubebeshwa matofali ktk miradi ya Serikali, Hadi wazee.

Yanayofanyika Kwa wanufaika wa TASAF Awamu hii, haikuwahi Kutokea.
TASAF ni moja ya maeneo yanayotakiwa kuangaliwa na kupitiwa upya na serikali. Kuna maelfu ya wanufaika vijana, wasio na ulemavu wowote wanaoishia kulewa kila wanapolipwa hiyo pesa.

Serikali ingeelekeza pesa za TASAF kwa wazee waliofikisha umri wa kustaafu ambao hawana social security cover, na hawana kipato kuweza kujikimu.

Ni rahisi kuwatambua kupitia viongozi wa serikali za mitaa husika.
 
Vijana hao ni UVCCM.

Unaweza ona sasa tatizo linapoanzia.
 
Tanzania hakuna maskini- watanzania wanakuawaje maskini wakati kila mtu walau ana ardhi 70 kwa 70

Hapa Tanzania masikini wengi ni wale wanaomiliki ardhi. Tazama mtu anayeuza bar hapa mjini ndio anasaidia ndugu zake huko vijijini wanaomiliki ardhi kuanzia 5+ acress!
 
Vi clip uchwara vitakufanya ufie bongo bila kutembea,hao ni Alcoholic,drugs user,lakini umesikia wanapewa msosi msosi ambao wewe huwezi ula,mtaani kwenu kuna mtu yupo Nje sio Uarabuni au Uturuki wala Urusi namanishe Westminster,kama hayupo nenda Zanziber, halafu fananisha huo mshahara wako wa milion moja na wao.
 
Mkiambiwa muweke mlinganyo wa democracy kama marekani hamtaki!!
Trump analia kuibiwa kura. Waliojaribu kutumia haki yao ya kidemokrasia na kikatiba Januari 6 mwaka juzi kuandamana kupinga wizi wa kura, wanasota mahakamani.

Hiyo demokrasia yao ina tofauti gani na hii ya bongo?!
 
mtoa posti mazingira kama hayo hapa bongo unaweza kuyafananisha na wapi?
embu onyesha upande wa pili wa watu kama hao kwa hapa tanzania halafu ucompare
 
TASAF ni moja ya maeneo yanayotakiwa kuangaliwa na kupitiwa upya na serikali. Kuna maelfu ya wanufaika vijana, wasio na ulemavu wowote wanaoishia kulewa kila wanapolipwa hiyo pesa.

Serikali ingeelekeza pesa za TASAF kwa wazee waliofikisha umri wa kustaafu ambao hawana social security cover, na hawana kipato kuweza kujikimu.

Ni rahisi kuwatambua kupitia viongozi wa serikali za mitaa husika.
Wameshajengewa nyumba zao kwa msaada wa TASAF na wale ambao hawakua na umeme wamevutiwa umeme kwa msaada wa TASAF saaafi sasa nini kingine mzee, 40k mboni pesa ndogo tu mboni unaanza kuweka nongwa?
 
mtoa posti mazingira kama hayo hapa bongo unaweza kuyafananisha na wapi?
embu onyesha upande wa pili wa watu kama hao kwa hapa tanzania halafu ucompare
Hakuna labda zamani ilikua k/koo ndio watu walikua wanalala nje ya yale maduka siku hizi hakuna labda daraja la kijazi pale ukipita sahizi utawakuta watu wamejilaza mda huu homeless in town, pia daraja la mfugale pembeni ya KIWANDA cha Azam kuna sehemu za kulala pale nakutaga wadau wamejilaza saaaafi kabisa, njia km unaelekea Airport ukipita kalakana angalia kwenye mitaro mule jamaa hua wanajilaza kwenye makalavati nikipita hua nawakuta

Karibu Dar,
 
Duh!

Hivi ulishafika huko; au unapasikia tu!

Kwa hiyo hapa unajisikia umeelezea maisha halisi wanayoishi watu wa huko?

Kwa hiyo wewe unasemaje, maisha wanayoishi waTanzania wengi ni ya kuridhisha kwamba hakuna sababu tena ya kulaumu viongozi wa hovyo wanaovuruga maisha na juhudi za wananchi wetu kujiondoa kwenye umaskini?

Kwanza kwa akili yako ilivyo, ni wazi kwamba wewe ungetokea kuwa huko, ungekuwa ni mmojawapo wa hao watu walioko mitaani na kuharibu mazingira.

Wewe huna tofauti yoyote na hao wanaoonyeshwa kwenye video kitabia.
 
Hao wengi wao ni mateja na mental issues, hao hawasaidiki na hawajakosa kazi, bongo hata kama uko OK na unataka kufanya kazi hiyo opportunity hakuna, ukiona mtu ombaomba US wengi ni choice au madawa lakini kazi zipo nyingi sana, waajiri wanatafuta watu wa kufanya kazi na kulipa bonus lakini hawapati, hao unawaomna wakienda Hospital wanatibiwa kila kitu na sehemu za kwenda kula bure kila siku,huwezi kukosa watu kama hao katika society hata muwe matajiri kiasi gani, madawa ni kitu cha ovyo sana
 
Hakuna labda zamani ilikua k/koo ndio watu walikua wanalala nje ya yale maduka siku hizi hakuna labda daraja la kijazi pale ukipita sahizi utawakuta watu wamejilaza mda huu homeless in town, pia daraja la mfugale pembeni ya KIWANDA cha Azam kuna sehemu za kulala pale nakutaga wadau wamejilaza saaaafi kabisa, njia km unaelekea Airport ukipita kalakana angalia kwenye mitaro mule jamaa hua wanajilaza kwenye makalavati nikipita hua nawakuta

Karibu Dar,
Nimezaliwa ocean road hospital kipindi hicho 80s .
Nimesoma msingi dsm, chuo udsm.
Nimefanya kazi mitaa ya Kkoo na posta Kwa muda sana.
Naijua dar labda kulipo wewe.
Dar/ Tz hakuna maskini wanaoishi mazingira ya hivyo ya kuwa na uhakika wa chakula na kausafi ka hivyo.
Bongo maskini design hiyo ni destuite .
Mtoa post ni mwehu flani huwezi kufananisha maskini wa US na wa huku asilani.
Hata kama umaskini ni umaskini ila umaskini wa huku umezidi yaani hadi vijana wanaamua kuimba eti bora angezaliwa mbwa ulaya.
Mtoa post umechemsha na hiyo post sijui ulitaka kumaanisha nini
 
Hoja yako ni dhaifu. Kuhusu suala la maendeleo na ustaarbu mzungu ametupita kwa mambo mengi, hilo halina ubishi.

Hata hiyo video yako ya hao watu maskini, mie kikubwa nilichokiona ni jambo namba moja katika ustaarabu (civilization) ambalo ni jambo la mipango miji.

Ukitaka kujua kama nchi ina akili kubwa kiasi gani kipimo ni kidogo tu:

1. Mipango miji.
2. Usafi wa mitaa.

Sasa kwetu nchi za watu weusi hali iko namna hii:

1. Kushoto ni Oysterbay (eneo ambalo lilipangiliwa na Mzungu), na kulia ni Namanga (eneo ambalo serikali haikuona umuhimu wa kulipangilia).

1676325328777.jpeg

2. Makazi holela nje ya Dar es Salaam. Maeneo kama haya yanaumiza sana kwa sababu yalikuwa ni mapori tu katika uhai wangu huu huu, lakini nimeyashuhudia yakichipuka kuwa makazi holela na serikali inaangalia tu. Serikali ilikuwa wapi kuyapangilia na kukata viwanja wakati bado yakiwa mapori? Kwanini serikali inaacha watu wanajenga makazi kiholela?

1676325553280.jpeg

3. Hii ni kutoka Windhoek, Namibia:

1*F4shaRUrjzg93TeQr2iNzg.jpeg

Kwa hiyo kama nchi tunaposhindwa kufanya kitu chepesi sana kama vile kupangilia tu makazi ya watu wetu, tunakosa nguvu ya kuongea chochote kuhusu akili, na maendeleo yetu. Yaani hata kumkosoa mzungu katika suala zima la maendeleo unapata wapi hiyo nguvu?

Mipango miji sio mpaka uwe tajiri. Ona haka kamji ka Challapata nchini Bolivia kalivyopangiliwa kwa utamu japokuwa kanaonekana ni kamji maskini maana barabara zote ni za vumbi. Lakini kwa kuwa kameshapangiliwa siku nchi ikipata hela za kujenga barabara za lami inajenga tu kwa urahisi. Hakutakuwa na habari za bomoabomoa.

View attachment 1676326016989.jpeg
 
Katika kitu ambacho sielewi ni serikali kushindwa kupanga miji na kupima viwanja vizuri, unaweza kufikiri labda zamani ndio ilikuwa hivyo lakini hata miji mipya ni ya ovyo kabisa , huhitaji kuwa tajiri kuwa msafi na kupanga miji yako ionekane vizuri lakini tumeshindwa, aibu sana hii na sijui kama umeme na maji tutaweza
 
Back
Top Bottom