Hoja yako ni dhaifu. Kuhusu suala la maendeleo na ustaarbu mzungu ametupita kwa mambo mengi, hilo halina ubishi.
Hata hiyo video yako ya hao watu maskini, mie kikubwa nilichokiona ni jambo namba moja katika ustaarabu (civilization) ambalo ni jambo la mipango miji.
Ukitaka kujua kama nchi ina akili kubwa kiasi gani kipimo ni kidogo tu:
1. Mipango miji.
2. Usafi wa mitaa.
Sasa kwetu nchi za watu weusi hali iko namna hii:
1. Kushoto ni Oysterbay (eneo ambalo lilipangiliwa na Mzungu), na kulia ni Namanga (eneo ambalo serikali haikuona umuhimu wa kulipangilia).
2. Makazi holela nje ya Dar es Salaam. Maeneo kama haya yanaumiza sana kwa sababu yalikuwa ni mapori tu katika uhai wangu huu huu, lakini nimeyashuhudia yakichipuka kuwa makazi holela na serikali inaangalia tu. Serikali ilikuwa wapi kuyapangilia na kukata viwanja wakati bado yakiwa mapori? Kwanini serikali inaacha watu wanajenga makazi kiholela?
3. Hii ni kutoka Windhoek, Namibia:
Kwa hiyo kama nchi tunaposhindwa kufanya kitu chepesi sana kama vile kupangilia tu makazi ya watu wetu, tunakosa nguvu ya kuongea chochote kuhusu akili, na maendeleo yetu. Yaani hata kumkosoa mzungu katika suala zima la maendeleo unapata wapi hiyo nguvu?
Mipango miji sio mpaka uwe tajiri. Ona haka kamji ka Challapata nchini Bolivia kalivyopangiliwa kwa utamu japokuwa kanaonekana ni kamji maskini maana barabara zote ni za vumbi. Lakini kwa kuwa kameshapangiliwa siku nchi ikipata hela za kujenga barabara za lami inajenga tu kwa urahisi. Hakutakuwa na habari za bomoabomoa.
View attachment 1676326016989.jpeg