Utandawazi umewaharibu vijana, msijisahau bila hao wazazi usingekuwepo duniani leo.
Hapa tukiwaweka pembeni wale wazazi waliotelekeza watoto wao wakiwa wadogo....
Inasikitisha kijana miaka 25+ bado unalalamika mzazi hajakutengenezea njia, amka pambana maana wao walifanya kadri ya uwezo wao.
Kuna watu wametokea familia za kimasikini sana Ila hiyo iliwapa motisha wakakaza saivi wanaenjoy mema ya nchi na wazazi wao.
Kwenye huu uzi nilishawahi kuku tag sijui kama uliusoma? Kama majanga hayajakukuta shukuru Mungu na uwe tayari kwa lolote kukutokea katika haya maisha. Yakikutokea majambo usiyoyatarajia kimbilio la kwanza ni kwa Wazazi lakini Wazazi nao wanakuletea mapichapicha yaani hii dunia iache tu kama ilivyo.
https://www.jamiiforums.com/
[IMG alt="Manyanza"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/30/30724.jpg?1699110413[/IMG]
Wakuu maisha ni safari ndefu yenye kila aina ya changamoto, Mimi mwenyewe nina mkasa mzito sana yaani kwa kifupi nilizaliwa kwenye familia iliyokuwa inajiweza kwa kila kitu lakini tatizo lilikuwa kwa Mzee alikuwa hataki Mama afanye kitu chochote na Mzee alikuwa ni mwanajeshi na kipindi hicho miaka ya 1995 fursa za ajira zilikuwa nyingi sana Ualimu na Uaskari lakini baba alikuwa akimwambia Mama yaani Mwanamke ufanye kazi ili uje uanze kuleta dharau?
Baba alikuwa anafanya na michakato mingine akawa anafanya anasa tu akishauriwa jambo hataki kusikiliza na alikuwa sio mlevi lakini ni kiburi tu kuna siku mwaka 1998 nikiwa na miaka 11 alimjibu Mama yaani wewe Mwanamke utanishauri nini?
Na maneno mengi ya kejeli ilipofika mwaka 1999 akanunua gari na Mama akamwambia yaani 6 Milioni unanunua gari? Kwanini usinunue hata Mashamba bado mzee alikuwa ni jeuri tu na kuna siku alinunua pikipiki bovu BMW yale mapikipiki yaliyotumiwa na Wajerumani vita ya pili kwa 2 M mama alimwambia lakini hakujali na hakutaka kushauliwa kitu, gharama za matengenezo sometimes zinafika mpaka laki 4 na kipindi kile hiyo pesa ilikuwa ni nyingi sana na mwaka huo huo 1999 gari ikapata ajali akaisafirisha kuja Dar kwa ajili ya matengenezo na hapo balaa ndio lilikoanzia.
Kule kazini akawa na absent mgogoro ukazuka mkubwa mpaka akawekwa mahubusu ya jeshi aliporudi kutoka Dar baada ya siku 42 lakini mahitaji yote muhimu tulikuwa tunapata.mimi na wadogo zangu, akawa na kesi kazini ilimsumbua sana na Mama ndio akawa anahangaika sana na.ishu zake zikzwa hazipo tena tukawa tunaishi kwa nusu Mshahara hali ilikuwa tough sana lakini kwa upande wangu nilipata rafiki ambaye familia yake ilikuwa inajiweza sana na Mzee wa ile familia alikuwa na Afsa wa idara ya serikali.
Baada ya Mzee kutoka mahabusu akapigiwa simu gari yake imepata kesi ilikamatwa katika tukio la Ujambazi alipagawa akaifuata gari yake na akaitelekeza familia mkoani yaani ni kwa neema ya Mungu tulikuwa tunaishi mkoani na Mimi sasa nilikuwa na rafiki wa kishua ambapo nilikubalika kwa Wazazi wa rafiki yangu kama mtoto wao nikawa napewa Mchele, Unga, Maharage na mimi nikawa napeleka home wanatumia maana Mimi nilihamia kwa rafiki yangu na nikiwa form 2 nilikuwa na kamera ya mzee YASHICA nikawa napiga picha wanafunzi na raia mtaani hapo nikawa napata pesa ya kuisaidia familia maana mama hakuwa na kazi hali ilizidi kuwa mbaya akaja mtoto wa Shangazi ambaye ni dereva wa magari akaibeba familia yote gharama zake.
Kumbe mzee alikuwa amesitafishwa kwa sababu alikuwa ameenda kinyume na kanuni za ajira za jeshi. Niliachwa kwa rafiki yangu niliishi pale vizuri na wadogo zangu wakagawanywa anayenifuata alienda kwa Shangazi na wengine walienda kwa Baba zangu wadogo mkoa.
Na mama ikabidi amfuate Mzee Dar hivyo hivyo. Naikatisha baada ya kufanya mtihani wa form two nikahamishiwa Dar es Salaam kwa juhudi za Baba Mkubwa ambaye alikuwa Afsa kwenye project za USAID nilihitimu kidato cha nne mwaka 2005 naada ya hapo nikaumwa sana miguu ilivimna kama nina matende na huu ilikuwa ni ushirikina na hii ilitokana na kumtukana sana Mjomba ambaye alikuwa akiishi na mdogo wangu maana walikuwa wanamnyanyasa na kumtumikisha kama Punda na shule alikuwa haendi vizuri na hii ilitokea baada ya kumfuata Mkoani Njombe nilipofika na kuikuta ile hali nilichukia na kuamua kutukana sana.
Tulivyoondoka pale kurudi Dar nikiwa mzima kuna siku mchana nimelala nikaota nipo kwenye mteremko kama pale Mkwajuni kwa wale wa Dar es Salaam mjomba akanigonga na baiskeli miguuni ndio hapo tatizo lilipoanza la.miguu niliteseka nalo sana. Nilivyopona sina haja ya.kuelezea.. ni.mengi nilipitia kuna siku nipo kanisani kuna Mama alikuwa ni Mwenyekiti wa NGO fulani akaniita akaniambia kuna kazi unaweza kuzingumza kiingereza nikamwambia nikaaa nafanya.kazi pale kwenye ile NGO kwa ujira wa euro 200 na nyumba ya kuishi pamoja na vijana wa kijerumani.
Hali ya familia ilikuwa ni mbaya mno Mzee alikuwa anafuatilia hela yake tuliomba na kufunga ili afanikiwe na.Mimi hapo nilikuwa nimeshapata kazi kwa Wajerumani ikabidi nijiendeleze kielimu na huku natoa support pale ilipobidi kufanya. Nilijiendeleza.mpaka nikapata diploma ya IT na Mzee akapata.pesa yake akaamua kuitelekeza familia hapa mjini na.
Mimi mkataba na Wajerumani ukaisha nikaingia tena kitaa nikawa nafanya kazi stationary pale posta kulikuwa.kuna dada akawa ananiuliza umesomea nini nikamwambia IT lakini sina uzoefu sana akaniambia hata mume wake kasomea IT kuna.siku mume wake akaja pale stationary akanikuta yule Dada akanitambulisha basi kwa neema ya Mwenyezi Mungu jamaa akawa ananichukua tunaenda kupiga kazi sehemu mbalimbali mpaka jamaa akaniambia dogo umeiva kuna kazi Zanzibar utaenda?
Nikamwambia nipo tayari nikaenda Zanzibar nikaanza kazi ilikuwa sio haba maisha.yalikuwa mazuri niliweza kumsomesha mdogo wangu ninayefuatana nae, hata yule wa tatu wa kiume nae nilimpa support kubwa sana kwenye mavazi na hela ndogo ndogo na mdogo wangu wa kike nae alikuwa shule ya.seminary nae nilimpatia pocket.money kama.kawaida...
Tatizo lilikuja pale nilipopata ajali ya gari nilipata.fracture yaani nilipasuka fuvu la kichwa na neva zinazopeleka taarifa kutoka kwenye jicho kupeleka kwenye ubongo zilitikisika. Nikapoteza kazi kutokana na kuwa napoteza fahamu nikarudi Dar es Salaam sasa hapo mpaka leo bado cha moto nakiona. Baba alishatelekeza familia, mdogo wangu niliyemsomesha kwa kupambana kila namna mpaka tulikuwa tunamwibia Mhindi ili nipate pesa asome,
Mama naye akapata mtaji wa biashara na wadogo zangu wale wengine kuvaa na mahitaji mengine wakaamua kunitelekeza kisa yule dogo alipata kazi ni mengi napitia lakini Maisha yetu yana siri kubwa sana na mamno yanapoenda hovyo inakuwa ni kwa sababu maalum. Kama Mungu amekuandikia kupata utapata tu maisha yanavyokuwa hovyo piga moyo konde. Siku zote nikupambana tu haina haja ya kulalamika hali niliyokuwa nayo Mimi ni mbaya sana nimejikubali na ninapambana.
Nimefanya kazi za hovyo nyingi sana pamoja na elimu kidogo niliyo nayo... Mkuu
Maxence Melo ananijua vizuri sana na kipindi hicho nipo na kazi tulikuwa tunakutana hapa mjini tunapanga mikakati mingi tu ila kuna siku kama miezi mitatu alinikuta sehemu namfungulia geti atoke hakuamini ikabidi nimwambie mkasa wote maana hata ile ajali aliona picha zangu...
Maisha sio kulalamika ni kupambana tu.