Maisha Yako ya sasa ni Matokeo ya family background yako

Maisha Yako ya sasa ni Matokeo ya family background yako

Kwenye huu uzi nilishawahi kuku tag sijui kama uliusoma? Kama majanga hayajakukuta shukuru Mungu na uwe tayari kwa lolote kukutokea katika haya maisha. Yakikutokea majambo usiyoyatarajia kimbilio la kwanza ni kwa Wazazi lakini Wazazi nao wanakuletea mapichapicha yaani hii dunia iache tu kama ilivyo.

Where We Dare To Talk Openly
[IMG alt="Manyanza"]https://www.jamiiforums.com/data/avatars/m/30/30724.jpg?1699110413[/IMG]

Manyanza

Wakuu maisha ni safari ndefu yenye kila aina ya changamoto, Mimi mwenyewe nina mkasa mzito sana yaani kwa kifupi nilizaliwa kwenye familia iliyokuwa inajiweza kwa kila kitu lakini tatizo lilikuwa kwa Mzee alikuwa hataki Mama afanye kitu chochote na Mzee alikuwa ni mwanajeshi na kipindi hicho miaka ya 1995 fursa za ajira zilikuwa nyingi sana Ualimu na Uaskari lakini baba alikuwa akimwambia Mama yaani Mwanamke ufanye kazi ili uje uanze kuleta dharau?

Baba alikuwa anafanya na michakato mingine akawa anafanya anasa tu akishauriwa jambo hataki kusikiliza na alikuwa sio mlevi lakini ni kiburi tu kuna siku mwaka 1998 nikiwa na miaka 11 alimjibu Mama yaani wewe Mwanamke utanishauri nini?

Na maneno mengi ya kejeli ilipofika mwaka 1999 akanunua gari na Mama akamwambia yaani 6 Milioni unanunua gari? Kwanini usinunue hata Mashamba bado mzee alikuwa ni jeuri tu na kuna siku alinunua pikipiki bovu BMW yale mapikipiki yaliyotumiwa na Wajerumani vita ya pili kwa 2 M mama alimwambia lakini hakujali na hakutaka kushauliwa kitu, gharama za matengenezo sometimes zinafika mpaka laki 4 na kipindi kile hiyo pesa ilikuwa ni nyingi sana na mwaka huo huo 1999 gari ikapata ajali akaisafirisha kuja Dar kwa ajili ya matengenezo na hapo balaa ndio lilikoanzia.

Kule kazini akawa na absent mgogoro ukazuka mkubwa mpaka akawekwa mahubusu ya jeshi aliporudi kutoka Dar baada ya siku 42 lakini mahitaji yote muhimu tulikuwa tunapata.mimi na wadogo zangu, akawa na kesi kazini ilimsumbua sana na Mama ndio akawa anahangaika sana na.ishu zake zikzwa hazipo tena tukawa tunaishi kwa nusu Mshahara hali ilikuwa tough sana lakini kwa upande wangu nilipata rafiki ambaye familia yake ilikuwa inajiweza sana na Mzee wa ile familia alikuwa na Afsa wa idara ya serikali.

Baada ya Mzee kutoka mahabusu akapigiwa simu gari yake imepata kesi ilikamatwa katika tukio la Ujambazi alipagawa akaifuata gari yake na akaitelekeza familia mkoani yaani ni kwa neema ya Mungu tulikuwa tunaishi mkoani na Mimi sasa nilikuwa na rafiki wa kishua ambapo nilikubalika kwa Wazazi wa rafiki yangu kama mtoto wao nikawa napewa Mchele, Unga, Maharage na mimi nikawa napeleka home wanatumia maana Mimi nilihamia kwa rafiki yangu na nikiwa form 2 nilikuwa na kamera ya mzee YASHICA nikawa napiga picha wanafunzi na raia mtaani hapo nikawa napata pesa ya kuisaidia familia maana mama hakuwa na kazi hali ilizidi kuwa mbaya akaja mtoto wa Shangazi ambaye ni dereva wa magari akaibeba familia yote gharama zake.

Kumbe mzee alikuwa amesitafishwa kwa sababu alikuwa ameenda kinyume na kanuni za ajira za jeshi. Niliachwa kwa rafiki yangu niliishi pale vizuri na wadogo zangu wakagawanywa anayenifuata alienda kwa Shangazi na wengine walienda kwa Baba zangu wadogo mkoa.

Na mama ikabidi amfuate Mzee Dar hivyo hivyo. Naikatisha baada ya kufanya mtihani wa form two nikahamishiwa Dar es Salaam kwa juhudi za Baba Mkubwa ambaye alikuwa Afsa kwenye project za USAID nilihitimu kidato cha nne mwaka 2005 naada ya hapo nikaumwa sana miguu ilivimna kama nina matende na huu ilikuwa ni ushirikina na hii ilitokana na kumtukana sana Mjomba ambaye alikuwa akiishi na mdogo wangu maana walikuwa wanamnyanyasa na kumtumikisha kama Punda na shule alikuwa haendi vizuri na hii ilitokea baada ya kumfuata Mkoani Njombe nilipofika na kuikuta ile hali nilichukia na kuamua kutukana sana.

Tulivyoondoka pale kurudi Dar nikiwa mzima kuna siku mchana nimelala nikaota nipo kwenye mteremko kama pale Mkwajuni kwa wale wa Dar es Salaam mjomba akanigonga na baiskeli miguuni ndio hapo tatizo lilipoanza la.miguu niliteseka nalo sana. Nilivyopona sina haja ya.kuelezea.. ni.mengi nilipitia kuna siku nipo kanisani kuna Mama alikuwa ni Mwenyekiti wa NGO fulani akaniita akaniambia kuna kazi unaweza kuzingumza kiingereza nikamwambia nikaaa nafanya.kazi pale kwenye ile NGO kwa ujira wa euro 200 na nyumba ya kuishi pamoja na vijana wa kijerumani.

Hali ya familia ilikuwa ni mbaya mno Mzee alikuwa anafuatilia hela yake tuliomba na kufunga ili afanikiwe na.Mimi hapo nilikuwa nimeshapata kazi kwa Wajerumani ikabidi nijiendeleze kielimu na huku natoa support pale ilipobidi kufanya. Nilijiendeleza.mpaka nikapata diploma ya IT na Mzee akapata.pesa yake akaamua kuitelekeza familia hapa mjini na.

Mimi mkataba na Wajerumani ukaisha nikaingia tena kitaa nikawa nafanya kazi stationary pale posta kulikuwa.kuna dada akawa ananiuliza umesomea nini nikamwambia IT lakini sina uzoefu sana akaniambia hata mume wake kasomea IT kuna.siku mume wake akaja pale stationary akanikuta yule Dada akanitambulisha basi kwa neema ya Mwenyezi Mungu jamaa akawa ananichukua tunaenda kupiga kazi sehemu mbalimbali mpaka jamaa akaniambia dogo umeiva kuna kazi Zanzibar utaenda?

Nikamwambia nipo tayari nikaenda Zanzibar nikaanza kazi ilikuwa sio haba maisha.yalikuwa mazuri niliweza kumsomesha mdogo wangu ninayefuatana nae, hata yule wa tatu wa kiume nae nilimpa support kubwa sana kwenye mavazi na hela ndogo ndogo na mdogo wangu wa kike nae alikuwa shule ya.seminary nae nilimpatia pocket.money kama.kawaida...

Tatizo lilikuja pale nilipopata ajali ya gari nilipata.fracture yaani nilipasuka fuvu la kichwa na neva zinazopeleka taarifa kutoka kwenye jicho kupeleka kwenye ubongo zilitikisika. Nikapoteza kazi kutokana na kuwa napoteza fahamu nikarudi Dar es Salaam sasa hapo mpaka leo bado cha moto nakiona. Baba alishatelekeza familia, mdogo wangu niliyemsomesha kwa kupambana kila namna mpaka tulikuwa tunamwibia Mhindi ili nipate pesa asome,

Mama naye akapata mtaji wa biashara na wadogo zangu wale wengine kuvaa na mahitaji mengine wakaamua kunitelekeza kisa yule dogo alipata kazi ni mengi napitia lakini Maisha yetu yana siri kubwa sana na mamno yanapoenda hovyo inakuwa ni kwa sababu maalum. Kama Mungu amekuandikia kupata utapata tu maisha yanavyokuwa hovyo piga moyo konde. Siku zote nikupambana tu haina haja ya kulalamika hali niliyokuwa nayo Mimi ni mbaya sana nimejikubali na ninapambana.

Nimefanya kazi za hovyo nyingi sana pamoja na elimu kidogo niliyo nayo... Mkuu Maxence Melo ananijua vizuri sana na kipindi hicho nipo na kazi tulikuwa tunakutana hapa mjini tunapanga mikakati mingi tu ila kuna siku kama miezi mitatu alinikuta sehemu namfungulia geti atoke hakuamini ikabidi nimwambie mkasa wote maana hata ile ajali aliona picha zangu...

Maisha sio kulalamika ni kupambana tu.
Mkuu story yako imenigusa sana, mwenyenzi Mungu akufanyie wepesi
 
Hapa Duniani ukizaliwa pambania maisha yako tu, wazazi wetu wanaturudisha nyuma sana wanakuwa ombaomba, mara wanataka kujengewa nyumba ilihali wao hawakujenga mm nawezaje kuwajengea

Mwaka 2024 sitatoa hata mia yangu Kwa mtu yoyote yule na Sina mke Wala mtoto
🤣🤣🤣🤣
 
Wazazi wanaimpact kubwaa sana katika future ya watoto ukizaliwa katika family isio jali future ya watoto automatically upo kwenye risky ya kuongia kwenye chain ya umaskin.

Once ukishaingia kwenye cycle ya umaskin kuchomoka ni ngumuh Sana.
Wazaz wengi WA kiafrika WAnazaa watoto kutafuta sifa watoto hawapat elimu Bora ,no ushauri wowote WA future life n.k

Nenda maeneo mengi ya kijijin utagundua wazazi ni kiwanda Cha kutengeneza poor generations.

Mtoto since day one mzazi hampi mtoto ushauri wowote hâta WA future carrier.

Wewe kama baba mtoto akiwa 7yrs Kaa nae chini mwambie fact about life ,mkazie
asome,mtengenezee hobby ya carrier ya kueleweka kwa Faida ya maisha yake .

Sio baba na mama wote kupost mtoto Mitandaon. Ndo wanaona furaha

.
Sure 💯💯 na ukitaka utoke kwenye mnyororo wa umasikini wa familia lazima ujitenge nao kwa muda otherwise utakuwa unapoteza muda tu..
 
Hapa Duniani ukizaliwa pambania maisha yako tu, wazazi wetu wanaturudisha nyuma sana wanakuwa ombaomba, mara wanataka kujengewa nyumba ilihali wao hawakujenga mm nawezaje kuwajengea

Mwaka 2024 sitatoa hata mia yangu Kwa mtu yoyote yule na Sina mke Wala mtoto
HAHAHAAA, Aisee umenikumbusha kitu. NCHI ya Japan watu kuoa na kuzaa hawana time. Nilikua nasikiliza documentary fulani ya maisha yao. Unakuta mtu ana miaka 50 hana mke wala mtoto anaishi na paka au mbwa tu. Watu wako busy na uchumi( Ubeberu mambo leo). Serikali ya japan ikawa kwenye mchakato wa kufanya marekebisho ya sera ya uhamiaji Vijana kutoka nje maana wazee ni wengi kuliko vijana.
Sasa mkuu na wewe unatupeleka huko kwenye ubeberu mambo Leo.

Ni ukweli mchungu kuwa familia nyingi Tanzania zina wategemezi wengi kuliko watafutaji na hili limepelekea ile Vicious circle of poverty kuendelea. Mtu mmoja anategemewa na watu zaidi ya watano akija kustuka kashazeeeka na hana kitu yaani alikua anafanya kazi kwa ajili ya wengine tena ndugu na marafiki.
 
Ndio kusema wewe ufahamu kiswahili au ulimbukeni wa lugha[emoji2957][emoji2957][emoji2957]
Nafahamu mkuu Ila ni katika kuelezea hili jambo hivyo lugha inaweza kubadilika ili kuleta maana iliyokusudiwa kwa jamii lengwa.
 
Pole Sana mkuu MUNGU akusimamie Sana it pain
Mungu ni mwema sana Mkuu unaambiwa na Wanasaikolojia ukiona haupatwi na Changamoto ingia ndani jifungie lia sana na umlalamikie Mungu mwambie kwanini Mungu huniamini? Hunipa hata changamoto?
 
Hapa Duniani ukizaliwa pambania maisha yako tu, wazazi wetu wanaturudisha nyuma sana wanakuwa ombaomba, mara wanataka kujengewa nyumba ilihali wao hawakujenga mm nawezaje kuwajengea

Mwaka 2024 sitatoa hata mia yangu Kwa mtu yoyote yule na Sina mke Wala mtoto
Huu ukweli mchungu, wazazi walioshindwa kujijengea nyumba wao wanawapa jukumu hilo watoto wao.

Inshort ,bongo unazaliwa kwa maslahi ya mtu mwingine (wazazi).
 
HAHAHAAA, Aisee umenikumbusha kitu. NCHI ya Japan watu kuoa na kuzaa hawana time. Nilikua nasikiliza documentary fulani ya maisha yao. Unakuta mtu ana miaka 50 hana mke wala mtoto anaishi na paka au mbwa tu. Watu wako busy na uchumi( Ubeberu mambo leo). Serikali ya japan ikawa kwenye mchakato wa kufanya marekebisho ya sera ya uhamiaji Vijana kutoka nje maana wazee ni wengi kuliko vijana.
Sasa mkuu na wewe unatupeleka huko kwenye ubeberu mambo Leo.

Ni ukweli mchungu kuwa familia nyingi Tanzania zina wategemezi wengi kuliko watafutaji na hili limepelekea ile Vicious circle of poverty kuendelea. Mtu mmoja anategemewa na watu zaidi ya watano akija kustuka kashazeeeka na hana kitu yaani alikua anafanya kazi kwa ajili ya wengine tena ndugu na marafiki.
Na hii laana ya single mothers ndio inaleta utegemezi haswa kwa wajomba.
.Unakuta mtu dada zake wamezaa watoto kibao wapo home tu baba zao wamekula kona.
 
Wazazi wanaimpact kubwaa sana katika future ya watoto ukizaliwa katika family isio jali future ya watoto automatically upo kwenye risky ya kuongia kwenye chain ya umaskin.

Once ukishaingia kwenye cycle ya umaskin kuchomoka ni ngumuh Sana.
Wazaz wengi WA kiafrika WAnazaa watoto kutafuta sifa watoto hawapat elimu Bora ,no ushauri wowote WA future life n.k

Nenda maeneo mengi ya kijijin utagundua wazazi ni kiwanda Cha kutengeneza poor generations.

Mtoto since day one mzazi hampi mtoto ushauri wowote hâta WA future carrier.

Wewe kama baba mtoto akiwa 7yrs Kaa nae chini mwambie fact about life ,mkazie
asome,mtengenezee hobby ya carrier ya kueleweka kwa Faida ya maisha yake .

Sio baba na mama wote kupost mtoto Mitandaon. Ndo wanaona furaha

.
OT: Kuna mmoja alisema napaswa kumpa jina mtoto like precious, gifts, loveness etc ila nisimwite like tata, madiba, liti, Ghati etc kwamba majina haya yamejaa laaana na mikosi.

Nikizingatia heading bila content, naenda kidogo tofauti na wewe. Tuna fugures nyingi ambazo ni vielelezo tosha kutoka kutembea kutafuta chakula mpaka kutakiwa kutembea ili kusaga chakula tumboni.
 
Na hii laana ya single mothers ndio inaleta utegemezi haswa kwa wajomba.
.Unakuta mtu dada zake wamezaa watoto kibao wapo home tu baba zao wamekula kona.
Tanzania ujamaaa unatumaliza. Kwa hili Nyerere awajibike. Kuna mambo ukisikia unatamani kulia.
Staff mwenzangu baba yake kastaafu mwaka juzi na hana nyumba mjini karudi kijijni. Just imagine mtu alikua mkuu wa idara ofisi ya umma mshahara milion 4 na perdiem na semina kila Leo, alipewa nyumba na gari la ofisi lakini alikua anasomesha watoto wa dada zake na ndugu wa kijijini alikotoka kwenye shule za private ( Catholic schools).
Leo aliosomesha hawana time naye hata kijijini hawaendi kimsalimia.

Inatia hasira aiseee yaani unazaliwa kwa maslahi na ustawi wa wengine.
 
Self-care inabidi kuwa kubwa kuliko giving care. Ukifeli hapo lazima utakwama .

Kuna kitabu nimesoma hayo mambo "The art of say no"
 
Tanzania ujamaaa unatumaliza. Kwa hili Nyerere awajibike. Kuna mambo ukisikia unatamani kulia.
Staff mwenzangu baba yake kastaafu mwaka juzi na hana nyumba mjini karudi kijijni. Just imagine mtu alikua mkuu wa idara ofisi ya umma mshahara milion 4 na perdiem na semina kila Leo, alipewa nyumba na gari la ofisi lakini alikua anasomesha watoto wa dada zake na ndugu wa kijijini alikotoka kwenye shule za private ( Catholic schools).
Leo aliosomesha hawana time naye hata kijijini hawaendi kimsalimia.

Inatia hasira aiseee yaani unazaliwa kwa maslahi na ustawi wa wengine.
Noma aiseee
 
Utandawazi umewaharibu vijana, msijisahau bila hao wazazi usingekuwepo duniani leo.
Hapa tukiwaweka pembeni wale wazazi waliotelekeza watoto wao wakiwa wadogo....

Inasikitisha kijana miaka 25+ bado unalalamika mzazi hajakutengenezea njia, amka pambana maana wao walifanya kadri ya uwezo wao.
Kuna watu wametokea familia za kimasikini sana Ila hiyo iliwapa motisha wakakaza saivi wanaenjoy mema ya nchi na wazazi wao.
waambie shangazi watoto wana viburi hawa
 
MKuu

Tatizo hata hiyo elim ya Sasa nayo!

Inaumiza TU vijana haitii suluhisho pa kesho ya kijana mwenyewe!!

Labda carrier za medicine ajiajiri lakini sio hiki ninachoona kinaendelea!!

Back
Top Bottom