Maisha yamebana wakuu, natafuta kazi yoyote ya halali

Holota

Senior Member
Joined
Feb 20, 2022
Posts
146
Reaction score
142
Habari wakuu,

Naomba msaada wa connection ya kazi yoyote halali, hasa kwenye viwanda, maghala, site za miradi au sehemu yoyote yenye uhitaji wa wafanyakazi. Nina Degree ya Finance lakini imekuwa ngumu kupata nafasi ya kazi ya fani yangu, hivyo kwa sasa niko tayari kufanya kazi yoyote ya halali kwa bidii na uaminifu.

Kazi ikipatikana Dodoma, Singida au hata mkoa mwingine wowote niko tayari kwenda kufanya kazi. Kwa kweli hali yangu ya maisha ni ngumu sana kwa sasa, hivyo naomba msaada wa connection au taarifa yoyote ya kazi kutoka kwa wadau.

Nina uwezo wa kujifunza haraka, kufanya kazi kwa juhudi na kushirikiana vizuri na watu wengine. Kikubwa ninachotafuta ni nafasi ya kufanya kazi na kujikwamua kimaisha.

Mwenye taarifa au msaada wa connection naomba aniunganishe.

Ahsanteni sana wakuu
 
Duh Finamce unakosa kazi, kuna kitu hakiko sawa kwako.

Kila siki lazima kuwe na matangazo ya Finance
 
nyingi wanahitaji experience au mambo ya CPA kuingia hivi hivi bila hizo vitu unaweza kutuma maombi hata 10 na usipate interview hata 1

Mkuu opone your eyes, zipo kampuni changa, zinalipa malipo ya wastani, hivo soko lao ni recent graduates.

Ndo hua tunaanzia huko, baada ya 2yrs, una jump kwa hawa magiant.
 
Jinga hilo,lenyewe linakaza fuvu kutafuta eti kazi ya fani yake.
kwa nin unasema neno" jinga " broh , umesoma nilichoandika kweli au we umerukia kujibu tu
 
Habari wakuu,

Naomba msaada wa connection ya kazi yoyote halali, hasa kwenye viwanda, maghala, site za miradi au sehemu yoyote yenye uhitaji wa wafanyakazi. Nina Degree ya Finance lakini imekuwa ngumu kupata nafasi ya kazi ya fani yangu, hivyo kwa sasa niko tayari kufanya kazi yoyote ya halali kwa bidii na uaminifu.

Kazi ikipatikana Dodoma, Singida au hata mkoa mwingine wowote niko tayari kwenda kufanya kazi. Kwa kweli hali yangu ya maisha ni ngumu sana kwa sasa, hivyo naomba msaada wa connection au taarifa yoyote ya kazi kutoka kwa wadau.
Nina uwezo wa kujifunza haraka, kufanya kazi kwa juhudi na kushirikiana vizuri na watu wengine. Kikubwa ninachotafuta ni nafasi ya kufanya kazi na kujikwamua kimaisha.

Mwenye taarifa au msaada wa connection naomba aniunganishe.
Ahsanteni sana wakuu
+255795386999 chat WhatsApp na huyo mvimba macho
 
Mkuu opone your eyes, zipo kampuni changa, zinalipa malipo ya wastani, hivo soko lao ni recent graduates.

Ndo hua tunaanzia huko, baada ya 2yrs, una jump kwa hawa magiant.
dah sijui nisemeje ila kiufupi ninafanya application ila feedback hata za kuitwa tu interview ndo changamoto , ndio maana nimeomba kwa mdau yeyote hata kazi ambayo siyo ya finance kama umesoma vizuri nilichoandika
 
Back
Top Bottom