Maisha yamefanya Vijana wanaokaa vijiweni kupotea

Maisha yamefanya Vijana wanaokaa vijiweni kupotea

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Kipindi cha nyuma kidogo ilikuwa ni kawaida sana kukuta vijana wamekaa vijiweni wanapiga soga asubuh hadi jioni,.

Lakini siku hizi mambo ni tofauti na zamani ni nadra kukuta vijana wamekaa kaa hovyo bila shughuli maalum.

Picha kwa hisani ya mtandao.

Screenshot_20230414-060319.png
 
Hongera huku kwetu kuna segemu nikipita lazima nikute vijana asubuhi nawahi kupita siwakuti ila kuanzia mida ya saa tatu asee ni kelel mpka jioni ukiona pamepoa wameenda kula majumbani mwao.

Siku moja nimepita hapo kuna kiduka nikakukua soda nikakaa nikanywa stor wanazopiga hazieleweki kama ni mpira wanabishana mpka haina maana kama ni mapenzi aloo wanaongea mpka matusi. Kiufupi vijana wanaokaa vijiweni bado walo asilimia chache wanastuka wakaondoka
 
Mkuu wapi huko unaishi hakuna hao vijana? Huku kwetu wapo sana tu, tena ukiwakuta wamekaa lazma na "cha arusha" kihusike...

Ila kiuhalisia ni kweli wamepungua, sio kama zamani, wengi vijiwe vyao sikuhizi ni kwenye bodaboda.
 
Sina takwimu sahihi ila asilimia kubwa sana ya vijana unakuta wamekaa haswa vijiwe vya bodaboda, huku dar kila baada ya mita chache unakuta kundi la vijana sio chini ya kumi wapo kijiweni, hapo ni stori za mipira, burudani, kamari na mapenzi!

Sijajua haswa ni mtindo gani wa maisha unajengeka kwenye taifa hili kupitia vijana .
 
Kipindi cha nyuma kidogo ilikuwa ni kawaida sana kukuta vijana wamekaa vijiweni wanapiga soga asubuh hadi jioni,.

Lakini siku hizi mambo ni tofauti na zamani ni nadra kukuta vijana wamekaa kaa hovyo bila shughuli maalum.
Picha kwa hisani ya mtandao
View attachment 2587096
Ni maeneo gani hayo?
 
Siku hizi vijana wadogo wanamiliki visenti kutokana na shughuli kama bodaboda na bajaj kuwepo. Kama kijana hana bajaj au bodaboda ya kuendesha atapewa na mwenzake kwa kuitwa day worker, safari mbili tatu zinatosha kumpa day worker senti za matumizi, hivyo basi hakuna kijana anayekaa kijiweni wakati vijana wenzake wanafanya shughuli za maendeleo
 
Wapo wengi tu kazi hakuna.

Wanajadili kila anayepita mbele yao utafikiri wamewazaa wao.

Wanaweza kupa details za kila mtu hapo mtaani kwao hatua kwa hatua.
Ila jamii ya watanzania ni mitambo ya umbea. Hata ukijifichaje watakujua tu unavyoishi. Ingependeza wakatumia huo weledi kutatua changamoto za maendeleo kwenye tafiti za elimu, kisayansi na kiuchumi.
 
Labda mtaani kwenu mkuu, huku kwetu npaka tumeamua kukopa mageti ili tu kuepuka kero zao,. Yaani asubuhi ukiamka wao wapo mpaka unajiuliza hawa jamaa hawana makwao jamani hawalali?? Ni masaa 24 siku 7 za wiki mwaka mzima,uuwwii wanatia kinyaa aisee chaaa!!!!
 
Sina takwimu sahihi ila asilimia kubwa sana ya vijana unakuta wamekaa haswa vijiwe vya bodaboda, huku dar kila baada ya mita chache unakuta kundi la vijana sio chini ya kumi wapo kijiweni, hapo ni stori za mipira, burudani, kamari na mapenzi!

Sijajua haswa ni mtindo gani wa maisha unajengeka kwenye taifa hili kupitia vijana .
Inasikitisha aisee, maana ndio wanaume hao ambao ndio "kichwa" cha familia... Yaani nikiwaza hivyo nasema wanawake/wake kazi tunayo na watoto wetu[emoji56]
 
Back
Top Bottom