Maisha yamejaa huzuni kuu, nini kinaleta furaha maishani?

Maisha yamejaa huzuni kuu, nini kinaleta furaha maishani?

clearmind

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2013
Posts
813
Reaction score
1,913
Habari za wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira?

Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.

Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
 
Andiko lako nimelielewa unateswa n upweke , pambana ukiweza kaa au shida baa au lala huko .
Habari za Wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira? Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.
Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
 
Mimi sio mlevi bosi. Wala hata huko baa sijawahi enda
We unahis ukiwa wapi unakosa amani ,nimetumia tu baa kifupi unaonesha unapokua alone ndio unapata huo mda wa kuwaza , usiruhusu kua mwenyewe hakikisha umejichanganya kuanzia muda wa kulala mpka kwenye harakati ,kwa kifupi nilikumbana na hali hio baada ya kupoteza familia yangu ya awali nikawa mpweke sana hasa nikiwa nyumban ,nikachukua ndugu nikaishi nae kwani sikua na nia ya kuoa kwa kipindi hiko
 
Habari za Wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira? Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.
Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
Nilichogundua maisha huwa matamu pale unapopambana ili utimize jambo Fulani ila ukishapata Kila kitu baada ya muda huwa hamna furaha kwani Kila unachikitaka unakifanya bila jasho na akili hivyo halikupi attention uliokusudia, hii changamoto hata Mimi napitia
 
Hii Hali ni ngumu sana. Moyo unauma na hujui shida ni nini. Naweza kujitahidi kuongea na wazazi na ndugu lakini maongezi yakiisha tu Hali inarudi pale pale hasa wikiendi hizi.
 
Yaani unaweza waza mambo mengi sana lakini kumbe tumezaliwa ili tufe
Sema nilichojifunza ni kwamba, usifanye furaha iwe lengo, wewe fanya vile vitu vinavyokuvutia....

Kuna hisia nyingi sana unatakiwa uzihisi kama binadamu, bila ugumu maisha hayana maana usijaribu kukwepa ugumu.

Mfano umesema unatamani kuoa, unaweza ukaoa, unafurahia harusi lakini kuna muda utafika utakosana na mwenzi wako utaona kama ndoa ni kazi.

Kwahiyo huwezi kuwa na furaha 24/7
 
Nilichogundua maisha huwa matamu pale unapopambana ili utimize jambo Fulani ila ukishapata Kila kitu baada ya muda huwa hamna furaha kwani Kila unachikitaka unakifanya bila jasho na akili hivyo halikupi attention uliokusudia, hii changamoto hata Mimi napitia
Umepataje kila kitu mkuu wakati Mengi mwenyewe kafa akiwa bado anatafuta!!
 
Furaha ni wewe mwenyewe, furaha unaitengeneza mwenyewe, hailetwi na mke wala mme wala rafiki.

Jitengenezee furaha yako, furaha yako unaitengenezaje?? Kuwa na pesa? Basi zitafute sana....furaha yako ni kuzagamua?? Nenda kafanye. Furaha yako ni nini??
 
Back
Top Bottom