Maisha yamejaa huzuni kuu, nini kinaleta furaha maishani?

Maisha yamejaa huzuni kuu, nini kinaleta furaha maishani?

Habari za Wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira? Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.
Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
Kila mtu ana namna ya kujiletea furaha, haiwezi kufanana mtu na mtu.

Wewe angalia unachoona unakipenda na unahisi ukikifanya utapata AMANI ya moyo >Furaha.

Unaweza tenga muda kila weekend kwenda maeneo kwa ajili ya kubarizi (Kama sio mnywa pombe), kula, kunywa pata music uupendao, kutana na watu wapya, rudi nyumbani ukiwa mwepesi kabisa.
 
Habari za Wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira? Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.
Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
Ibada mkuu inaachilia amani ya moyo
 
Ni kweli, lakini bado hatokuwa na amani kwa asilimia zote. Kuwa na mke na watoto kuna jambo la kuwafikiria wao pia, vipi kama mtoto/watoto wakapatwa jambo fulani au mke. Bado ni mlolongo aisee
Ni kweli lakini kwa kiasi fulani itapunguza msongo wa mawazo kuliko kukaa single alafu auna hata wa kukuliwaza unaweza ukafa kiholo
 
Nilichogundua maisha huwa matamu pale unapopambana ili utimize jambo Fulani ila ukishapata Kila kitu baada ya muda huwa hamna furaha kwani Kila unachikitaka unakifanya bila jasho na akili hivyo halikupi attention uliokusudia, hii changamoto hata Mimi napitia
You are right.. ukishafika malengo unagundua sio kiLe unachokitamani ni sehemu ya furaha. Unakizoea na unaona kawaida.

Ingawa wengine wanatamani wafikie ulipo
 
Habari za wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira?

Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.

Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
Hii hali hata mimi inanitesa sana
 
Neno la Mungu "BIBLIA". Ukisoma na Mungu akikusaidia kuelewa utapata furaha ya ajabu sana maana utakuwa na matumaini na mahali pa kuiburudisha roho yako.
"Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga" (Maneno Ya Yesu mwana wa Mungu ambayo ni ya kwelli na yametendeka kwetu.

Yohana 14:27.
 
Habari za wikiendi familia? Ni kitu gani huweza kuleta furaha katika Maisha? Mali? Mke? Watoto? Marafiki? Ibada? Au ajira?

Mwenzenu siku za karibuni nakuwa mwenye huzuni sana. Sijioni kuwa mwenye furaha japo mambo mengi niliyoyatamani kuyafikia angalau kwa kiasi namshukuru Mungu.

Wakati mwingine nafikiria pengine nioe lakini akili inagombana na moyo. Ni nini hasa huleta furaha katika Maisha?
Tafuta gym ya karibu,anza kufanyq mazoezi..mawazo huja kama hujachoka
 
Hakuna kitakachokuletea furaha isipokuwa ni wewe mwenyewe.Ridhika na Hali uliyonayo,samehe wengine,jisamehe na wewe mwenyewe binafsi,Usiwabebe watu moyoni kwako Kwa sababu ya mambo waliyokutendea,jifunze kuachilia mambo. chunguza Matendo Yako kama yanaridhisha. mwisho acha kujisumbua na huu ulimwengu,wote tunapita,usiangaishwe na jambo lolote Cha msingi ni uzima.
 
Furaha ni wewe mwenyewe, furaha unaitengeneza mwenyewe, hailetwi na mke wala mme wala rafiki.

Jitengenezee furaha yako, furaha yako unaitengenezaje?? Kuwa na pesa? Basi zitafute sana....furaha yako ni kuzagamua?? Nenda kafanye. Furaha yako ni nini??
Awe na pesa hayo mengine yatakuja automatic.
 
Hakuna kitakachokuletea furaha isipokuwa ni wewe mwenyewe.Ridhika na Hali uliyonayo,samehe wengine,jisamehe na wewe mwenyewe binafsi,Usiwabebe watu moyoni kwako Kwa sababu ya mambo waliyokutendea,jifunze kuachilia mambo. chunguza Matendo Yako kama yanaridhisha. mwisho acha kujisumbua na huu ulimwengu,wote tunapita,usiangaishwe na jambo lolote Cha msingi ni uzima.
Ni ushauri mzuri. Nimeridhika kiasi hapa nilipo bosi. Kutofautiana na watu ni jambo la kawaida maana changamoto ndiyo maisha yenyewe. Ila huwa sibebi kabisa Moyoni mambo ya namna hiyo. Najitahidi kujitafuta hasa kwamba nipate furaha kwa namna gani.
 
Back
Top Bottom