Maisha yanaenda kasi; Jaffo kutoka kusimamia bajeti ya Tsh 3 trilioni TAMISEMI hadi 28 bilioni Muungano na Mazingira

Maisha yanaenda kasi; Jaffo kutoka kusimamia bajeti ya Tsh 3 trilioni TAMISEMI hadi 28 bilioni Muungano na Mazingira

Hata kama! Marupurupu na bahasha za khaki ndiyo kila kitu! Tamisemi posho na bahasha ni nyingi ukilinganisha na huko aliko.

Jamaa alikuwa anapiga sana misele kukagua miradi ya bosi wake! Zile zote zilikuwa ni hela! Full Per diem! Sasa huko aliko anahangaika tu kukagua maji machafu ya kwenye viwanda!
Na vyuma chakavu!
 
"Hii nyimbo ya sweet kitunguu ya Man moo' hata Jaffo hajawahi kuisikia"
 
Msigwa yuko ikulu pia
Yupo Idara ya Habari na Maelezo kwa sasa. Ofisi yake ipo Jengo la PSSSF Dodoma ghorofa ya 5 kama sijakosea. Nenda pale utamkuta.

Ingawa kwa majukumu yake sio kitu cha kushangaza ukimkuta kwenye ziara za viongozi wa kitaifa. Anaweza kuwa na PM, President na hata VP.
 
Ni kweli kuna Wizara kubwa na ndogo kwa mfano Waziri Jaffo zamani alikuwa akisimama bungeni kuomba kupitishiwa bajeti ya zaidi ya tsh 3 trilioni lakini leo hii amesimama pale pale bungeni kuomba kupitishiwa bajeti ya tsh 28 bilioni.

Lakini mwendazake Magufuli alipounda baraza hili la mawaziri alisema hakuna wizara kubwa wala ndogo zote ziko sawa.

Kazi Iendelee!
Na anakoelekea atasimamia budget za kwenda sokoni na wake zake wanne
 
Back
Top Bottom