Hii ilitokea mtaani miezi kadhaa leo nimekumbuka nikabaki mdomo wazi.
Kuna nyumba mme na mke wote waajiriwa, sijajua wameajiriwa wapi ila kiukweli wana maisha mazuri sana na ndoa yao walifunga hizi ndoa za maMC wakubwa, ndoa ilifana kweli kweli.
Sasa pale nyumbani kwao si kuna mfanyakazi wa kiume na wa kike, madam house akawa anahisi anaibiwa na mfanyakazi wa kike, kafuatilia wee hakuelewa ikabidi ambane mfanyakazi wa kike siku moja, cha kushangaza kumbe anaibiwa na mfanyakazi wa kiume, wakatega mtego wahusika wakanaswa.
Nisiongee sana, ila ilikua aibu kubwa sana, jumba lipo tupu hadi sasa wote wamelikimbia.