Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Maisha yanahitaji umiliki vitu vitatu tu:-
- Makazi -nyumba ya kuishi
- Usafiri- wa kukutoa sehemu moja kwenda kwingine
- Biashara- kitu cha kukuingizia kipato, iwe majengo, usafirishaji n.k
Na wengi wanapambana kuajiriwa, kutafuta nafasi n.k ili tu kuweza kufanikisha hayo mambo makuu matatu.
Ukiyatafuta mengine zaidi ya hayo, ni kuuchosha mwili kwa vitu visivyokuwa na msingi; kwa sababu hata upambane vipi, hutokuja kumiliki 'private jet' wala 'train' kwa mazingira uliyopo.
Wengi mtatofautiana kwa ukubwa katika hayo maeneo matatu, lakini haitaathiri hivyo vitu vitatu.
Kwa hiyo kama umeshakamilisha hivyo vitu vitatu, unatakiwa utembee kifua mbele na usiangaike na mengineyo yatakayokuletea presha na kufa mapema.
Njooni kwa mjadala.