Maisha yangu baada ya miaka 37!

Huo mkopo ndo vituko kabisa sitaki hata kukumbuka. Nilikopa 36m. Hapo Hela ya LOAN BOARD ikakatwa. Nikabakiwa na 20. Ukiniuliza nilichofanya sijui... Iliisha kiutani utani
Hizi m.36 ulizipeleka wapi,Ulizitumiaje?
 
Ni kwa sababu huoni. Una macho lkn upo gizani. Watu kama wewe wapo lkn ni rare kwa mtu mwenye elimu. Elimu husaidia kufukuza mapepo ya ujinga. Jicho lako la 3 limezibwa. Sasa naona linaanza kufunguka.
Lingine ni kwamba una pepo la umaskini ambalo hufanya kazi kama laana. Yaani hufifisha nyota.
Unakuwa mtu wa kuamini ili ufanye jambo, hadi uwe na hela nyingi wakato hata buku 10 ulionayo, hujaifanyia kitu cha maana.
Toka kwenye hicho kifungo.
Rahisi kwako ni kurahisisha mishipa ya ubongo. Acha kufanya mishipa ya ubongo kuwa migumu.
Kuwa na macho yanayoona fursa haraka sana.
Fungua jicho lako la 3.
Uwe na uwezo wa kutofautisha kati ya Assets and Liabilities.
Nimekuwa na watu wa karibu kama wewe kwa hiyo naongea kwa experience.
 
Uzi wako huu una majibu tosha ya kwa nini hujafanikiwa mpaka sasa.

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Hapo omba mke wako asipate pesa
Akizopata tu umeachwa ndugu.
Ok.
Turudi kwenye mada: Panga chumba na sebule ulipe 60-80 per month.
Hapo utaanza maisha mapya
Usiogope kuchekwa, Mimi nilipooa kodi nililipa 100k per month, nikafulia nikaenda kupanga chumba cha 30 per month tena kwa ugumu. Sasa nimehamia kwangu kidogo naona nafuu ingawa bado napambana.
 
Unalipa Kodi ya nyumba laki tatu kwa mwezi unasema una maisha magumu sisi tunaolipa elfu 30 kwa mwezi mbona hatulalamiki
 
Kwanini unafuga mtu asiyezalisha na una kipato kidogo?
Mfanye mke wake naye awe mzalishaji
 
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya usitumie pesa zaidi ya mapato yako. Lakini jaribu kusoma vitabu vya uchumi I recommend you to read The richest man in Babylon it might help you, pia usione kama umechelewa amini bado muda unao wa kurekebisha ulipokosea.
 
Chumba na sebule na ana watoto wanne,ubahili gani wakijinga hivi,mtu ulipwe mshahara milioni ulipie chumba na sebule tu Cha elfu 60,ushidwe ata kuchakata papuchi ya mke wako barabara,kwa mshahara huo nyumba nzuri ungemshauri ya laki na nusu au laki mbili,sio 60 au 80 ,ingekua mikoani uko ndio labda ungesema 80 apate ata vyumba viwili na sebule Ila sio kwa dar
 
Umemshauri vema...kuongezea atafute nyumba ya bei rahisi kidogo maan laki 3 kwa mwezi ni nyingi kwa mshahara wake.
 
Watoto 4, Mke na 300k kodi, gambe kimtindo, hapo balaa, kwa maisha ya kibongo noma hapo bado zile dharula za hapa na pale, Muhimu wife angekuwa naye anapiga mishe ingesaidia sana, bila ya hvyo komaa upate biashara ya maana kwa pesa unayolipwa unaweza kuanzisha kitu kikakutoa zaidi
Usipofanya maamuzi mapema madogo wote wakiwa school ndo shughuli yako imeishia hapo , utapanga for long time ukizingatia age ishaenda mzee, m namjua mtu mzima mmoja hivi anakazi lakini anaishi kwenye chumba na sebure (kapanga) yeye , mke, watoto wake wawili na mmoja wa hao watoto wake nayeye ana mtoto, na jamaa anakaribia 60 sasa hivi, haya mambo yanaogopesha sana kwa sisi vijana maada muda hausimami
 
Uko vzr, najua ameondoka na kitu hapa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…