Maisha yangu baada ya miaka 37!

Maisha yangu baada ya miaka 37!

I can feel you.
Pole sana Mkuu.
Kuanzia sasa naona umeashajua tatizo hivo anza kuchukua hatua.
Jitahidi weka akiba kila mwezi hata kama ni kidogo au ikiwezekana hayo marupurupu kila unapoyapata yafanye ndio akiba fungua account weka na hakikisha hutoi kwa namna yoyote ile.
Pia mkeo jitahidi apike hata maandazi atakusaidia majukumu mana anakuwa mjeuri wakati hana mchango wowote badala ya kukuonea huruma.Kama mtoto bado mdogo sana mwache akue kidogo halafu mpe mtaji auze hata genge au kupika mihogo hatokosa visent vyakumsupport nawe pia atakuwa amekupunguzia mzigo Mana vingine atatatua yeye bila kusubiri msaada wako.
Pia punguza matumizi yasiyo ya lazima wala kutaka kuishi kama fulani ilhali hali yako haifanani na wao.Kama ni mnywaji epuka kwenda baa na marafiki zaidi nunua zako mbili tatu nywea nyumbani.Punguza kuchangia sherehe mana sio kila sherehe lazima uchangia chagua zile muhimu sana tu.Matumizi ya nyumbani yalimit jitahidi kila ukipokea mshahara weka stock ndani ya vyakula na gas au mkaa na ukomae vitumike kwa usahihi sio wajinyime ile watumie wanachoeeza kumaliza hii itakusaidia katika kufanya saving.
Nahisi wanao pia wanasoma shule za kulipia hivo unajikuta una mzigo wa kulipa ada hapa wadau wengine watakupa solution.
Usikate tamaa mi naona wewe bado umri haujaenda sana kiasi Cha kupata stress hivo bado mapema anza sasa weka malengo na hakikisha unayaishi hayo malengo.
Mungu akutie nguvu na kukuvusha katika hali hii.
Asante sana
 
Huo mkopo ndo vituko kabisa sitaki hata kukumbuka. Nilikopa 36m. Hapo Hela ya LOAN BOARD ikakatwa. Nikabakiwa na 20. Ukiniuliza nilichofanya sijui... Iliisha kiutani utani
20m hapo ndio shida, alafu msikilizaneni na mkeo sio kisa hana kazi basi unambagua! Watoto wane4 blooo wanatosha, mfungulie shemeji hata kaduka, punguza pombe, anza kwenda church, pata new aideas, panga budget zako vyema kwa kumshirikisha mkeo. Madeni mikopo ya bank na huku unalipa loan board ni hatari mzee, anza kuishi kwa posho, mashara anza kumpa mkeo apange budget za mwezi mzima.
 
Habari.

Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite, Mshana Jr n.k. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo;

1. Ninafanya kazi serikalini mshahara take home ni 1.3 m., hapo nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012, hivyo nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne, mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda, sina kiwanja, sina akiba, bado nimepanga, kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na mke siyo mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha, lakini bado tunasonga.

7. Mke hana kazi, hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, n.k.

10. Sina gari, niliyoanza nao kazi wana nyumba kubwa na magari mawili, moja la mke.

Nahisi nina mkosi, nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale, ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki tano wametoboa mi nipo nipo tu mpaka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Mimi ni dereva,mshahara wangu hauzidi laki7, nina familia kama wewe,nyumba na gari pia....kuna tatizo la kimatumizi uko nalo na kusombwa na tamaa za dunia kimatumizi pasi kujua unachopata ni kikubwa tu,ntarudi ukiniita tena nikufundishe
 
Asante nipe madini tafadhali.
 
20m hapo ndio shida, alafu msikilizaneni na mkeo sio kisa hana kazi basi unambagua! Watoto wane4 blooo wanatosha, mfungulie shemeji hata kaduka, punguza pombe, anza kwenda church, pata new aideas, panga budget zako vyema kwa kumshirikisha mkeo. Madeni mikopo ya bank na huku unalipa loan board ni hatari mzee, anza kuishi kwa posho, mashara anza kumpa mkeo apange budget za mwezi mzima.
Asante sana. Hilo wazo la kumpa mshahara ninalo maana anasema hiyo pesa nikiishika mimi utaona matokeo...labda nijaribu kwa miezi mitatu nione Kuna chochote au utopolo. Kuhusu idadi ya watoto ni kweli wametosha ila nitajaribu kupata wa kiume nikifika miaka 40! Umri wa wife unaruhusu ni mdogo kwangu. Ikitokea tena wa kike nitatundika daruga
 
Bado hujachelewa kaka,hiyo miaka tisa unayojutia fanya kama ni liheso...
Anza sasa ukiwa positiveli na mtangulize mungu japo yeye hajawahi tuacha.
 
Huo mkopo ndo vituko kabisa sitaki hata kukumbuka. Nilikopa 36m. Hapo Hela ya LOAN BOARD ikakatwa. Nikabakiwa na 20. Ukiniuliza nilichofanya sijui... Iliisha kiutani utani
Pole sana
Mimi nipe 10 tu uone maana kwa sasa nalipwa 500 000 ila nimenunua kiwanja na kuezeka vyumba 2

Nina watoto 2
Mfanyakazi 1
Mke hana kazi
Wazazi wa mke na wa kwangu wananitegemea mimi lakini bado

Toeni sadaka achaneni na habari za michepuko
 
Bado hujachelewa kaka,hiyo miaka tisa unayojutia fanya kama ni liheso...
Anza sasa ukiwa positiveli na mtangulize mungu japo yeye hajawahi tuacha.
Asante sana
 
Pole sana
Mimi nipe 10 tu uone maana kwa sasa nalipwa 500 000 ila nimenunua kiwanja na kuezeka vyumba 2

Nina watoto 2
Mfanyakazi 1
Mke hana kazi
Wazazi wa mke na wa kwangu wananitegemea mimi lakini bado

Toeni sadaka achaneni na habari za michepuko
Aise hongera, unaishi dsm?
 
Pombe haikufanyi usifanye maendeleo, pombe ni starehe kama starehe nyingine starehe zipo nyingi sana na hakuna tatizo kwa binadamu kufanya starehe baada ya kazi is nature hata Mwenyezi Mungu alifanya siku ya jpili,. Ipo sababu nyingine kaa chini tafakari Hilo.
Kweli kabisa,
Pombe inasingiziwa sana
 
Angalia meza yangu.....just all alone [emoji17]

20221029_205546.jpg
 
Asante nipe madini tafadhali.
Hakuna kitu mbaya kinacho maliza pesa kama kununua vitu vidogo vidogo bila mpangilio,pipi, pombe, vyakula pasi na njaa, kumsaidia tu yoyote bila sababu za msingi, kununua tu viatu ilihali una pea za viatu vingine kama kumi na ni viatu vigumu tu, akili kubeba maoni yasiyo na tija, wewe ni mmoja kati ya wale wanaoamini kujenga ni mpaka uwe na Milion 100.

Jifunze kuweka akiba, tumia pesa ktk mahitaji ya msingi pekee na achana na mambo yasiyo na tija, rejea nyumbani mala tu utokapo kazini ili usiingie kwenye tamaa za Dunia ukiwa mitaani, mtengeneze mke awe mwenye uchungu na familia na maendeleo, akiweza utaona matumizi ya ndani ya elfu 50 per week, badala ya matumizi ya laki mbili per week... Tengeneza miezi yako ya kununua kimoja baada ya kingine, toka nje ya mji tafuta kiwanja nafuu nunua na anza ujenzi taratibu bila kuathili watoto wako swala la chakula na shule, pia hapo kwenye shule, usipeleke watoto kwenye shule ambazo zinakupa umasikini kwa sababu tu unataka watu wakuone umepeleka watoto shule za kulipia pesa nyingi,zenye raha ilihali watoto watakuja kuishi Afrika yenye majeraha yasiyo angalia mtoto alikula mkate shule na kubebwa na Coaster asbh na jioni, naweza kuendelea lakini naamini kwa uchache utakua umejua namaanisha nini.

N.B - mawazo yako yabebe kufanikiwa kimaisha, kutengeneza pesa na vyote unavyo vitaka maishani, utaona vinakuja kimoja kimoja maana utaweka bidii, achana na mambo ya Simba na Yanga huo ni upuuzi mkubwa unaokula muda wa waTanzania wengi mitaani
 
Back
Top Bottom