Maisha yangu baada ya miaka 37!

Maisha yangu baada ya miaka 37!

Habari.

Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite, Mshana Jr n.k. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo;

1. Ninafanya kazi Serikalini mshahara take home ni 1.3 m, hapo nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012, hivyo nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne, mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda, sina kiwanja, sina akiba, bado nimepanga, kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na mke siyo mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha, lakini bado tunasonga.

7. Mke hana kazi, hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, n.k.

10. Sina gari, nilioanza nao kazi wana nyumba kubwa na magari mawili, moja la mke.

Nahisi nina mkosi, nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale, ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki tano wametoboa mi nipo nipo tu mpaka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Pole sana,Anza kwenda kanisan acha pombe
 
UPE Ualimu Pasipo Elimu
Elimu Siyo Cheti Ni Ujuzi
 
Kule Unakokunywa Pombe Umenunua Daftari La Msomi Kuandika Madeni
 
Pole pombe imesababisha mengi,
Binafsi pombe inanitesa ila ipo siku yake.

Kwa idadi hiyo ya watoto be careful usishindwe kuwalisha. Pia tafuta kiwanja ujenge hata kibanda
 
Wewe unazingua, esabu zinakukataaaa kwanza mkopo uliokopa ulifanyia nini? Take home 1.3 alafu unalalamika? Wasio na kazi kabisa nao wasemaje???? Acha starehee chagua priorities za msingi.
 
Usisingi🤪🤣😉zie pombe, anza kwenda kanisani ,soma neno la mungu mtafute yesu ukipata kitabu cha jesus always kitakusaidia, anza kutrack matumizi, nyumba 300k kwa mwezi mmh mbona zipo nyingi goba 150k kwa mwezi, ili kutoboa mke mfungulie kitengo yani huu ndo muda wa kupambana mzee ukifika 40 utadata maisha ni akili na sio kukimbizana na time bali tyming
 
NIKUAMBIE KITU BROO HAYA MAISHA BILA KUJINYIMA NA KUJIWEKEA MISINGI UTAKUJA KUONA KAMA UNAROGWA KUMBE HUNA MIPANGO.

KAMA ULIVYOSEMA KUNA VIJANA WANA MISHAHARA MIDOGO TU NA WAMEJENGA WANATOKEA KATIKA NYUMBA ZAO SEMBUSE WW WA 1.3 ???
KWANZA HAINA HAJA YA KUKAA HAPO KODI KUBWA TAFUTA SEHEMU HATA YA 150.000 AU 200,000 UNAPATA MJINI HAPA
JIRUDISHE NYUMA KIDOGO ILI MAMBO YAKO YAENDE NA UONE FAIDA YA KAZI ULIYO NAYO.

ILA UKITAKA KUISHI KAMA WENGINE UTAJIDANGANYA MWENYEWE .KAMA UNAWEZA KUACHA POMBE ACHA TU MANA SIJAWAI SIKIA POMBE INA FAIDA ZAIDI YA HASARA YA KUMALIZA HELA.!

KUNA VIWANJA VYA MIKOPO SIKU HIZI UNAWEZA UKAANZA NUSU MZEE WANGU NI SIMPLE TU .NA ASIKUDANGANYE MTU ETI VIWANJA VIPO MBALI YA MJI SIO KWELI
SIKU HIZI KILA SEHEMU INAFIKIKA TENA KIRAHISI MANA KUNA BODA BODA NA BAJAJI

NOTE
ILA KAMA UNAONA UKIACHA POMBE UTAONEKANA MSHAMBA AU UMEFULIA BASI ENDELEA KUPIGA ULABU MPAKA UTAKUJA KUSTUKA UMESTAAFU NDIO UNAANZA KUTAFUTA IDEAS ZA BIASHARA UKIWA KWENYE NYUMBA YA KUPANGA
 
Habari.

Nina miaka 37. Sifurahii maisha katika umri huu. Kama kuna mtu anaweza kutoa ushauri wa kunikomboa asisite, Mshana Jr n.k. Mtiririko wa matukio ni kama ufuatavyo;

1. Ninafanya kazi Serikalini mshahara take home ni 1.3 m, hapo nina mkopo wa miaka 5 NMB.

2. Kazi nimeanza tangu 2012, hivyo nina miaka 9+ kazini.

3. Naishi Dar es Salaam.

4. Nina mke na watoto wanne, mtoto wa nne bado ni kichanga.

5. Tangu nianze kazi sijui pesa zangu zinapoenda, sina kiwanja, sina akiba, bado nimepanga, kodi laki tatu kwa mwezi.

6. Mahusiano yangu na mke siyo mazuri sana kwa sababu ya ugumu wa maisha, lakini bado tunasonga.

7. Mke hana kazi, hana biashara.

8. Nakunywa pombe mara kwa mara.

9. Siendi kanisani kabisa ila kwa matukio maalum mfano ndoa, ubatizo wa mtoto, n.k.

10. Sina gari, nilioanza nao kazi wana nyumba kubwa na magari mawili, moja la mke.

Nahisi nina mkosi, nifanye nini? Yapo mengi kuonesha hasara ninayoihisi. Kazini napata marupurupu ya hapa na pale, ila najiona sitoboi. Wadogo zangu wenye mshahara wa laki tano wametoboa mi nipo nipo tu mpaka mama yangu amekata tamaa. Faraja yangu iliyobaki ni binti zangu ambao hawaelewi chochote kwenye hii Dunia ya vita.
Kaka unafanya kazi wapii Wenzako wanaiba na wewe hela yako unakunywa Pombe sasa unataka maisha yabadilike 5M umeifanyaje .Fanya biashara wacha kutumwa kama una msingi fanya biashara zipo biahara nyingi za kufanya,
 
Kama story yako sio chai basi wewe ni bogas

Kama ulikopa na huna kiwanja, nyumba Wala Gali Sasa hiyo pesa ya mkopo ulinunua nini
 
Back
Top Bottom