Beberu Mwitu
JF-Expert Member
- Mar 31, 2019
- 495
- 708
Mimi ni mzee wa miaka 35, mzaliwa wa mkoani Iringa huko nyanda za juu kusini. Historia yangu ya maisha katika nchi hii imekuwa ni yenye kupanda na kushuka mithili ya roller-coaster. Imejaa mambo mengi ya kufurahisha na machache sana ya kuhuzunisha lakini yenye kunijenga zaidi. Shule ya msingi nilianza nikiwa na miaka 10 mwaka 2001, huku nikiwa na ndoto za kuwa mhandisi mkubwa sana🙂.
Nilihitimu darasa la 7 mwaka 2007. Kisha nikajiunga na Elimu ya Sekondari kuanzia kidato cha kwanza mpaka cha nne mwaka 2008- 2011, kidato cha sita 2012- 2014( Japo kidato cha tano sikusoma kikamilifu kwa sababu shule haikuwa na mwalimu hata mmoja na nilichukua PCM). Hivyo mtihani ule wa kidato cha sita sikufanya vizuri sana.
Na kipindi hicho nasoma nilikuwa nafanya kazi mbalimbali ili kujikimu kimaisha na kulipia gharama za masomo yangu. Baada ya kuhitimu kidato cha sita nilihudhuria kozi ya JKT kwa miezi minne pale Ruvu kuanzia Septemba 2014 mpaka Januari 2015.
Na baada ya hapo nikajaribu kuomba vyuo mbalimbali vya ufundi kwa ngazi ya Stashahada kikiwemo Chuo Cha Maji pale Ubungo, ATC na DIT nikilenga kusomea ama Water Supply and Sanitation Engineering au Civil Engineering (Chuo cha Maji walikuwa wanatoa mkopo lakini niliukosa). Nilfanikiwa kupata nafasi katika vyuo hivyo lakini sikuweza kujiunga navyo kutokana na gharama kubwa. Kisha nikaomba ualimu mwaka 2016 pale Vikindu TC na nikapata nafasi lakini sikuweza kuripoti kutokana na sababu zile zile.
Hiyo ilikuwa kama wake up call kwangu. Nikaamua kujikita zaidi katika kufanya vibarua kama saidia fundi, ulinzi, kulima na kuchoma mkaa ili nipate chochote kitu niweze kujilipia ada ya chuo cha kati. Nilipambana sana na Oktoba mwaka 2019 nikajiunga na chuo cha ualimu Msingi kwa kozi ya Kiingereza yaani English Medium. Niliamini kwamba nikihitimu Elimu hii basi naweza kupata kazi na kisha kwa kile kipato chake nijiunge na kozi yangu pendwa ya Civil Engineering. Ee bwana mambo hayapo hivyo!.
Mungu aliniwezesha kupata kibarua mara baada tu ya kuhitimu chuo cha ualimu na GPA yangu ya 4.2,nilikuwa nalipwa Sh 100 000(laki moja) tu kwa mwezi 😁, nilfanya hicho kibarua kwa mwezi mmoja tu na kupata sehemu nyingine kwa malipo ya Sh 300 000. Mambo yakawa magumu sana na nikaamua nifanye betting a.k.a risky investment kama shughuli ya ziada ili kukuza kipato. Hii shughuli nimeifanya kwa phase mbili.
Nathubutu kusema huu ulikuwa ni uamuzi mbovu kuwahi kuufanya katika maisha yangu. All my measly income disappeared down the drain. Nilijuta sana na nikaamua kuachana nayo hiyo biashara. Nadhani Mungu aliniadhibu kwa kumkosea pale nilipofanya betting. Kwa kifupi safari yangu katika maisha imenifundisha mengi sana ikiwemo uvumilivu. Kwa sasa naamini naweza kuishi pahala popote pale bila ya hofu yoyote.
Hapa chini ni mlolongo wa kazi nilizozifanya kwa miaka 27 mpaka hivi sasa, hii ni kwa sababu nilianza kufanya kazi za kulipwa ujira nikiwa na miaka 8 mwaka 1998. Kwenye mabano ni maelezo ya ziada ya kazi husika hasa miaka niliyozifanya.
-Vibarua vya kulima na kupalilia mazao mbalimbali (1998-2020)
-Uwindaji wa ndege kwa kutumia Ulimbo (1996-2017)
-Uvunaji wa Asali msituni (2000-2007)
-Kuuza miwa na mahindi ya kuchemsha (2004- 2007)
- Saidia fundi (2009- 2020)
-Kuuza magazeti Jiji Dar ES salaam(2011- 2013-Mimi ni mmoja wa waanzilishi wa biashara ndogo ndogo pale kituo cha Makonde-Mbezi Beach palipokuwa na NBC Bank)
-Ulinzi kupitia kampuni binafsi Jijini Dar Es Salaam (2018-2019- Securex waliniona mfupi wakanikataa licha ya CV yangu nikajiunga na G1 Security pale Kitonga- Upanga)
-Ualimu (2021- 2025)
-Kuuza genge (2017-2019)
-Kubeti (2016-2019), (2023-Januari 2025)😬😬
-Kuchoma na Kuuza mkaa (2005- 2020)
Kwa sasa naweza kusema mimi ni mstaafu ambaye hana pensheni. Asanteni sana.
#No Reforms No Election