Namalizia
Maisha yangu na matapeli na nilivyojifunza utapeli
Kipindi iko enzi za mzee wa msoga pesa zilikuwepo yani na utoto wangu wa miaka 19 nilikuwa na simu ya lenovo touch, na nokia ya touch
Nilivyomaliza four maisha ya kujichanganya nikajikuta nipo interest na matepeli wazee wa town, kwanza ndo wamenilea tangia naingia mjini nyumba niliyofikia kulikuwa na bar na ndo yalikuwa makutano yao kila siku asubuh na jioni wakitoka kutapeli
So walikuwa wananijuwa vyema , matapeli wana lugha zao wanaweza zungumza na usiwaelewena pia wana lugha zao za ishara na alama
Kwaiyo mi lugha yao nilikuwa naijuwa hata wakiwa wanasimuliana deal zilivyokuwa kwa siku iyo nilikuwa nawaelewa,
..
Waliiuwa wanachnanganya maneno asilimia kubwa ni maneno ya kikongo na mengineyo
Mfano , mbongo ni polisi,. Famme ni mwanamke , mwasi ni mke , garison ni mwanaume
Tororoo ni pikipiki, njenje ni baskeli,. Miguu ni nauli,
Kipeme ni mwenye pesa au boss , brokea kushawishi,
Vuraa ni gari, maiti imefufuka yani alietapeliwa kawadaka,
Kansee ni kufa, kashoo ni jela , pogoma ni kuongea, kimaseke ni kwa akili, maseke yani akili
Chungamira yani tizama au chungulia
Zoba. Yani anaetapeliwa
Wa foo yani mtu nuksi au snichi,
Pakee,mbumba, ni pesa
Elfu moja walikuwa wanaaita mgongo mmoja alafu elfu kumi wanaiita katani, laki wanaiita tani , milioni nimesahau,
Manjee yani kula, doro yani kulala,
Kansee au amekansee yani amekufa,
Ukimwi walikuwa wanaiita takataka yani ana matakataka means ana ukimwi,
Konyee ni ****, alafu makonyezi ndo kutombna
Kumchekecha mtu yani kumsomesha deal kama anaingia mkenge
Mizoo measn nyumbani
Battlee yani kukamatwa
Kashoo yani jela
Pombe ni mokeji yani tupate mokeji measn tupate kunywa pombe,
Msongoro yani kwenye deal au kazini ukisikia twende msongoro ndo wanaenda kwenye kazi za kutapeli
Shako means begi
Kitu cha biee au famme wa biee yani kitu kizuri au mwanamke mzurii , biee means kizuri
Pembe au kiberiti ni kifaa flani ivi walikuwa wanatumia kuwekea madini feki
Agghh nimechoka kiufupi matapeli walikuwa na lugha zao
Kipindi iko utapeli ulikuwa wa aina nyingi sana na walikuwa wanapiga pesa sana,
Tapeli ni mtu mmoja mchangamfu sana , charming, inteligent, haogopi, anamaneno matamu, hana huruma na pesa, hajali cheo chako akitaka kukutapeli,
Njia walizokuwa wanatumia si za kumdhuru mtu zaid ya maneno tu, ila hapo hapo kulikuwa na makundi tofauti kuna ambao walikuwa wanaingia maofisini au maduka ya simu wanasunda
Au ktk supermarket kubwa wanasunda mfano pombe kali za bei, yani vile vitu vya bei vinavyobebeka kirahisi, kuna wale waliokuwa wanajifanya watu wa TRA, uhamiaji na maofisa wengine amabapo wanajuwa wanatarget vipi ulaji, wengine yani wanavyo jiweka hakika utoboi
.ntaendelea