Kulikuwa hakuna cha fisi wala nini. Ukitaka ukweli mtafute mtu mzima kama mimi akupe ukweli. Enzi hizo nilikuwa nakaa Mburahati zile numba za Jeshi (National Housing) ambazo zilijengwa wahamie watu toka kariakoo wakazikataa kwa sababu kulikuwa porini. Wakati huo mabasi (DMT/UDA) yakiishia Kigogo mwisho kwa Binti Kaenga. Binti Kaenga alikuwa mganga al-maaruf hata simu alikuwa ameweka nyumbani kwake (miaka). Jina la uwanja wa fisi lilitokana na vyakula na pombe aina zote. Enzi hizo Wagogo, Warangi, Wanyaturu, Wanyiramba ndiyo palikuwa kwao huko. Napakumbuka vizuri maana nilikuwa kwenye "late 20s", na nilikuwa nachungulia huko mara chachechache.