kwahiyo hizo nguvu ndo zinaendesha maisha ya mwanadamu kwa hyo hta mafanikio ya mtu yana tokana na hizo nguvu?
Tatizo lenu wakristo ni kutosoma biblia na kuielewa Yesu alipozaliwa nyota ya kung'aa ilionekana kwa wasafiri na ikawaongoza hadi mji alipozaliwa yesu. Biblia haikuchambua kwa kina juu ya nyota japokuwa wakati wa kuzaliwa yesu mamajusi wa mashariki walikwenda yerusalem Math. 2:1-2. Sasa niwaulize swali wakristo je, ile nyota inauhusiano gani na yesu? Au kabla ya kuzaliwa yesu nyota hazikuwepo? Ukweli ni kwamba nyota zina uhusiano mkubwa na maisha yetu sisi wanadamu. Tatizo letu hatupendi kusoma na kuchunguza juu ya maisha yetu. Mungu aliturahisishia maisha yetu ili tuweze kumuabudu bila vikwazo tumeyafanya maisha yetu kuwa magumu ndo maana hata ibada zetu zimekuwa ngumu kwa sababu tumejipa uvivu wa kufikiri na kujifunza.
Nyota inaanza kama kitu kinaitwa "molecular cloud" ambayo inacontain hydrogen na helium... ikitokea inbalance ya forces zinazo hold hizi clouds in place zinaanza ku-collide against one another na hapo ndipo mwanzo wa nyota unapoanza hadi inakua nyota sawa ilivo jua au nyota nyingine... force pekee inayounganisha mtu na nyota ni force of gravitation ambapo kama nyita iko mbali sana basi hii force ni negligible... uchawi uchawi mwingine ni ndoto tu na hauna evidence yoyote, leo asimame mtu aniambie nyota yangu afu aniambie nifanye nini nifanikiwe, nitafanya opposite na nitafanikiwa kumprove wrong... ukisema unaamini predictions za maisha kuoingana na nyota basi dini zooote ni uongo, sayansi ni uongo, study ya nyota tu ndio ukweli which is nonsense, maana utakua umeondoa "free will" kama nyota zinaendesha maisha ya mtu..
Ile nyota ilionyesha direction na haikuendesha maisha ya Yesu, it was simply an indication na hakuna kitu kama nyota kuendesha maisha ya mtu.. Uhusiano pekee ulionao na nyota ni kwanza jua hukupa nguvu,
Pili nyita nyingine angani pamoja na jua zina force inaitwa "gravitation" ambayo ina keep kila kitu in balance... Hakuna nyota kukuendesha wewe ati uwe secretary, nyota inajua usecretary? hahahaha
Your right scientifically although naweza pingana nawe kupingana nawe spiritually. Sayansi ni ishu nyingine na natural force ni ishu ya pili. Vitu hivi huenda pamoja sana ingawa kuna mahali vinapingana na hasa pale sayansi inaposhindwa ku prove jambo ambalo ni la asili. Let me give you an example, kuna imani imeenea kwa jamii ya wtz kuwa kitovu cha mtoto kikiangukia kwenye uume wa mtoto atakuwa -------. If you ask any doctor atakwambia hakuna kitu kama hicho because there is no scientific relation between or not proved scientifically. Ngoja niendelee kufuatilia nitakupa data zaidi
Kwa wakristo BIBLIA TAKATITU imekataza kufuata utabiri wa nyota na mengine yafafananayo na hayo sijui kwa jirani zetu wa kibla
huku kibra aya inasema......hakika kamali,ulevi na kupiga ramli ni amali za shetani, jiepusheni nazo
uliza jingine, uislamu ni hoja bana hahaaaaa
Maisha yetu huongozwa na Mungu
Wale akina mamajusi walifuata nyota mpaka wakafika alipozaliwa mtoto yesu.
Elimu ya nyota ipo sahihi kabisa katika kutabiri ila biblia imekataza.
Kwa wakristo BIBLIA TAKATITU imekataza kufuata utabiri wa nyota na mengine yafafananayo na hayo sijui kwa jirani zetu wa kibla
Well said!
Ila nna maswali ya kukuuliza!
Jee unatambua kuna wanaotabiri kwa ushirikina (kwa kutumia mashetani) na kunawanaotabiri kupitia sayansi ya anga = astrologers (bila ya kutumia mashetani)???
Kwanini kunaukweli juu ya hao wanaotabiri?
watoa mada wenzangu kwa mtazamo wangu mimi naona wote mpo sawa ila kwa uwakika zaidi na uelewa wa kina jaribuni kufanya tafiti kwenye kitu kinachoitwa Shiriki mtapata mwanga zaidi na kujua tofauti iko wapi na kipi ni lipi na lipi ni kipi
wasallam
Ki-Dini Haswa Dini ya Kiislam kuangalia mambo ya nyota imekatazwaMkuu shirki kutokana na imani yangu, imegawika sehemu 4!
Nikihusisha shirki na hayo mambo ya nyota, ni wazi kuwa nyota ni moja kati ya shirki!
Nimeona hapo juu umemjibu mdau amtafute elimu, nikaona tena umesema hata wachungaji waliifata nyota ya Yesu hadi walimfikia!
Upande wa pili huku, temeambiwa tutafute elimu hata china! Elimu yeyote inaruhusika kusomwa na kutumika! Ispokuwa itumike kwa mambo mema, either kwa kusaidia watu!
Tupaache hapo!
Na kunakitu ningependa nijue:
Kama nyota zinaukweli ndani yake, kwanini imekatazwa kufatilia?
Natambua wenzetu (wazungu na wachina) hutumia nyota kuangalia vipaji vyao na kudetermine nini wafanye ili wapate maendeleo!
Na kunabaadhi ya watu (wanandoa) hutegea hata miezi ya kupeana mimba ili mtoto wao azaliwe ktk nyota wanayoitaka wao na kwa kuamini mtoto atakuwa vile wapendavyo!
Jee unaliongeleaje hilo?
...
Na pia niliskia na watu wazima kwamba kunasiku (tarehe/mwezi na mwezi/mfunguo) fulani ndani ya mzunguko wa mwaka, ukioa ndani ya siku hizo, ndoa yako haitadumu! Wakati kuna baadhi ya siku ukioa ndoa inakuwa imara!
Jee ulishawahi kuskia hilo?
Kama umewahi, kwanini iko hivyo?
Binafsi haya mambo yananichanganya sana, ningependa nitambue kuna nini nyuma ya pazia! Kwa nini iwe hivyo?
Cc: MziziMkavu!
Mengi nimesikia kuhusiana na nyota binafsi bado nko njia panda juu ya hili kutokana na maelezo yake kua watu hutofautiana nyota kulingana na mwezi na tarehe ya mtu kuzaliwa pia tabia ya mtu inatokana na nyota yake ilivyo hata kazi pia hutegemeana na nyota swali langu linakuja kwann iwe ivo inamaana ikitokea mtu nyota yake inamtaka afanye kazi ya aina fulan inabidi afanye hata kma haipend ilimrad tu nyota yake inasema ivo au hata kwenye masuala mazima ya mapenzi mtu itabidi achague yule anaye endana kwa kuangalia nyota ili aweze kudumu nae mbona kuna mambo unaweza ukafanya na ukaenza kudumu katika mapenzi.naomben mchango wenu juu ya hili
Ki-Dini Haswa Dini ya Kiislam kuangalia mambo ya nyota imekatazwa
hairuhusiwi kabisa. Ila kidunia yetu Ki-Sayansi inaruhusiwa kwa Sayansi haiamini mambo ya Dini.
Kuangalia siku tarehe mwezi na mwaka kwa ajili ya kufunguwa duka au kuowa mke au kusafiri au kuafanya jambo lolote lile zuri ipo na ni kweli ni elimu yake Mungu ndio maana tumekatazwa
katika dini ya Kiislam kutaka kujuwa siri zake Mwenyeezi Mungu. Lakini hapa hatupo kwenye
jukwaa la Mambo ya Dini tupo sehemu nyingine ya jukwaa la la ( Jamii Intelligence) tupo huru
kuzungumzia kila kitu kwa uwazi.