Unaposema Khadija alikuwa wa kwanza kumuamini Mtume Muhammad na kuwa Muislam, hujakosea kabisa. Sababu baada ya Yesu kuondoka duniani kukawa hakuna Uislam tena. Sababu Paulo alileta dini yake ya kikristo akawapoteza watu, na wewe mmoja wapo mpaa kesho kaisha kukupoteza. Kama hujaomba Mungu wako akurudishe katika njia iliyo kuwa ya haki, basi uko kwenye hasara kubwa hapa duniani na siku ya malipo. Hapo duniani wewe sala zako zinakuwa zinamtukuza mungu wa Paulo yule shetani. Tatizo lako wewe unavamia tu bila kutumi a akili, Lazima ujuwe kwanini Mungu alileta Mitume siku za Mwanzo. Sababu walikuwa wakija wanaleta sheria za kuamrisha watu wafate neno moja tu, hakuna miungu isipokuwa Mungu mmoja tu. Sa wewe akili yako iunafikiria vipi;
Kwanini Mungu aliwaleta kina Nuhu, Ibrahim, Lutu, Mussa, Issa(Yesu) kama watu walikuwa wametulia na wanafata dini moja tu. Tokea zamanai watu wanarudi wakisha ondoka mitume wanarudi kufanya madhambi yale yale, kama mnayo fata wakristo ya miungu sio Mungu. Hivi mtu mwenye akili kweli anaweza kusema Yesu ni Mungu au binadamu? Hayo ngojea mimi nikiwekee Qur'an inasema nini. Hata Bibilia haitakuja waelezeni vile kwa point, wacha nianzie pale mama yake Yesu alipo fatwa na malaika, mpaa amemzaa Yesu akiwa anaongea bado mdogo kasema nini. Watu wanasema siku zote mtoto akiwa mdogo siku zote hasemi uwongo, na kwakukufahamisha zaidi Yesu hakuwa muongo hata siku moja, usije ukasema nimesema Yesu ni muongo mana nyie wakristo ndio zenu kuzusha uwongo. Si unajua mmejifunza kwa mtume wenu Paulo.
Fatilia hapa Qur'an kwa point juu ya point sawa ndugu, haya twende afu wewe uniletee pia Bibilia yako inasema nini tokea Yesu hajazaliwa mpaa amefikia kusema kama inavyo sema Qur'an kama unaweza.
19. SURAT MARYAM
16. Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki; ***
17. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu. ***
18. (Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu. ***
19. (Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika. ***
20. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? ***
21. (Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa. ***
22. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. ***
23. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningeli kufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! ***
24. Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako Mlezi amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! ***
25. Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. ***
26. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. ***
27. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! ***
28. Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. ***
29. Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? ***
30. (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. ***
31. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, ***
32. Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. ***
33. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. ***
34. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. ***
35. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapo lihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. ***
36. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mola wangu Mlezi, na Mola wenu Mlezi. Basi muabuduni Yeye. Hii ndiyo Njia Iliyo Nyooka. ***
37. Lakini makundi yakakhitalifiana wao kwa wao. Basi ole wao hao walio kufuru kwa kuhudhuria Siku iliyo kuu! ***