Ishmael
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 15,039
- 6,017
MUHAMMAD SIO MTUME KWASABABU HAKUWAI ONGEA NA MUNGUKwa pointi hiyo, sababu hiyo (ya jina) bado haijamtofautisha Yesu na Issa. Lakini kama ilivyo kwa Yohana, Yahya au John, basi Issa na Yesu ni yule yule mmoja aliyezaliwa na Bikira Mariam (Quran 3:45 na Luka 1:26-31). Isitoshe, Quran Tukufu ilipoeleza kwamba Nabii Issa siyo Mungu (5:72), hakusulubiwa (4:157-158), na ametumwa kwa wana wa Israeli peke yao (3:49), Waarabu waliokuwa Wakristo hapo kabla walimfahamu kwamba huyo ndiye "Yesu sahihi" aliyekana "Uungu" katika Biblia pia (Marko 12:29-34) na ndiye aliyenusuriwa kuuawa kama ilivyoelezwa na Quran Tukufu na Biblia pia (Waebrania 5:7) na kweli katumwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli peke yao (Mathayo 2:6 na 15:24). Sa we ni Myahudi au kondoo wa kiyahudi, jibu swali dogo hapo.
Leo ningependa tujikumbushe mambo machache ambayo labda hatukuyatilia maanani. Mitume wote na manabii wote wa Biblia waliwai ongea na Mungu. Lakini, Mtume wa Allah "Muhammad" hakuwai ongea na Mungu HATA MARA MOJA. Je, utume wake tutauamini vipi maana hakuwai ongea na aliye mtuma?
Lakini Mitume wote wa Biblia waliongea na Mungu.
1. Musa anoangea na Mungu: Kutoka 3:1-21
2. Elia anaongea na Mungu: 1 Wafalme 19- Soma yote
3. Paulo anaongea na Mungu: Matendo ya Mitume 18:9
4. Yesu anaongea na Baba yake Matayo 3:17, Yohana 5:19-47,
Hiyo ni mifano michache kutoka Biblia.
Kama Muhammad alikuwa Mtume wa Mungu, kwanini hakuongea na Mungu?

