Maisha yetu ni mafupi sana

 
Inaumiza sana yaan😭
 
Eeeh..
Kifo ni kitu cha hovyo sana..
Siri za ulimwengu hatuzijui, huenda kifo ni kizuri. Imagine mpo ndani ya jengo ambalo kila baada ya muda mmoja wenu anavutwa nje ambapo hampaoni na aliyevutwa haonekani tena, Lazima woga utatengeneza hitimisho baya kuhusu huko nje sababu tulio ndani hatujui kilichowapata waliovutwa, ila katika uhalisia tunaweza tusiwe sahihi.
 
Kinachofukiwa ni mwili usio na hisia zozote...

Kama ambavyo hana kumbukumbu ya maisha kabla ya kuzaliwa, ndivyo itakuwa
Au kama ulalapo fofofo
 
Tozo hizi,ajali hizi,kuuana huku.... depression kibao
Hadi unajikuta unatamani kuishi primitively , usipande vyombo vya moto... Usijongee ubaki ulipo...

Lakini Maisha yanakulazimu ...

Sawa ni kuuvaa UJASIRI kwenda KWA codes and patterns .

Muhimu afya ya mwili na akili.

Mtaji wa kwanza huo..

Mengine Asili/universe/Muumba ataamua
 
Kinachofukiwa ni mwili usio na hisia zozote...

Kama ambavyo hana kumbukumbu ya maisha kabla ya kuzaliwa, ndivyo itakuwa

Tatizo ukiwaza kwamba baada ya kifo hakuna kinachoendelea INATISHA! Yaani kwamba ukishakufa tu basi, kila kitu kinazimika na hakitakuja kuwaka tena.. dah inatisha sana aisee

Ila pia ukiwaza kwamba baada ya kifo kuna kinachoendelea nayo pia INATISHA! Maana sasa hujui kitakachoendelea ni kipi...
 
Dah mkuu leo niliamka nikaanza kutafiti kama Tukifa consciousness nayo inakufa ...sijapata majibu ..

Nimeamua kutupilia mbali ... Ni mambo ya kuogofya ...
 
Yule mkenya??
Hata mie imenisikitisha sana, jamaa alishamaliza kabisa safari, kafia kwenye kadamnasi.
 
Amiin
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…