Maiti kugoma kuzikwa mpaka mahari itolewe

Maiti kugoma kuzikwa mpaka mahari itolewe

Bamdogo yangu lilimkuta jambo na tabia yake ya kupenda kuoa oa.
Tena unalipishwa hela nyingi sana
 
Ujahil tu , utaiotoleaje mahari Maiti ?!
 
Sio tukio la ajabu bali mimi naita ni UMASKINI wa watanzania walio wengi. Hao ndugu wa mwanamke ni MASKINI..Malofa.
 
Iwe fundisho kama hutaki ndoa fuata jamii isyotaka ndoa .
 
Afrikan customs must be followed sisi kwetu ukitos mahari tunakupa uondoke nae

Kwenye African customs and norms hakuna jina Selemani Sele wala hakuna jina Robert wala hakuna Ukristo wala uislamu.

Mkitaka kufuata utamaduni fuateni wote acheni unafiki.
 
Nami
Kuna tukio nalo lilitokea kilombero morogoro la ajabu sana.
Baba wa binti alisafiri kutoka tabora hadi kilombero akiambatana na watoto wake wa kiume 2 kwenda kudai mahari iliyobaki kwa kijana aliyeoa binti yake na kwenda kuishi naye huko kilombero.
Kufika huko hawakielewana ukatokea ugomvi na vurumai yule baba na watoto wake wa kiume 2 kaka za binti aliyetolewa mahari nusu wakamshambulia yule kijana ambaye hakumalizia mahari na kwa bahati mbaya akafariki.
Wakakamatwa wakawa na kesi ya mauaji
Niliisikia hii.
 
Watu wanakimbiaga gharama za harusi ndo maana wanaamua kufanya local cohabitation
Sele

Nani alikuambia harusi ni jambo la lazima?

Halafu kichwa cha habari maiti kugoma kuzikwa wakati si kweli. Ilipaswa kuwa ndugu wa marehemu wagoma kuzika mpaka mahari kulipwa.
 
Umenikumbusha...mama alivyofariki baba aliambiwa amalizie mahari ndiyo aruhusiwe kumzika mke wake.

Uzuri hakuwa mbishi nadhan alikuwa anajua .. aliwakabidhi wazee chao akaenda kumzika mke wake.
 
KAMA MTEMBEZI WA MTAANI NIMESHUHUDIA JAMBO AMBALO LIMENISHANGAZA NA KUNISTAAJABISHA KWA WAKATI MMOJA NA HII NI MARA YA MBILI KULIONA HAPA VINGUNGUTI JE NI JAMBO GANI? KAA CHONJO.

NI HIVI NDUGU WA MKE AU MUME KUFORCE KUFUNGA NDOA NA MAITI
ILIKUWA JUZI WAKATI NAHANGAIKA NA SHUGHULI ZANGU ZA KUJENGA TAIFA NIKAONA NDUGU WAMEMSHIKIA PANGA MWANAUME KWENYE MSIBA WA MKE WAKE AMBAYE WALIFANIKIWA KUPATA WATOTO WANNE ILA WALIKUWA HAWAJAOANA SASA NDUGU WAKASEMA HAWAZIKI MPAKA ATOE MAHARI NA AMUOE YULE MAREHEMU BWANA AKAFIKIRI UTANI ILA ALIKALIWA KOONI MPAKA NDUGU WAKAJICHANGA NA KUTOA MAHARI NDO MAITI IKARUHUSIWA KUZIKWA.

NYINGINE NILIPATA TAARIFA AU UITWAVYO UMBEA KUTOKA KWA JIRANI YANGU KWAMBA NDUGU WALIKUWA KANISANI WANASUBIRI MAITI IINGIE ISALIWE KWA AJILI YA MAZISHI AMBAPO NDUGU WA MKE WALITINGA NA VURUGU KWAMBA NDUGU YAO HAZIKWI MPAKA MAHARI ITOLEWE YAANI ILIKUWA VURUMAI VURUGU TUPU MPAKA AIBU ASEEE, NDUGU WA MME ALIYEFIWA WALICHANGA MILIONI 2 NA VITU VINGINE ALITAKIWA AWASILISHE, BAADA YA HAPO NDO MAREHEMU WALIENDA KUZIKWA.

JE USHAWAHI KUSHUHUDIA KAMA MIMI UTUPE STORY YAKO.TUSHEE IDEA MBALI MBALI
WAKO SELEMANI SELE.
JAMII FORUMS NEWS Update nimepata link inayoshabiana na hii ishu. Aibu ya mwaka: kumbe mahari ina umuhimu sana
Rahisi tu hawataki azikwe waambie wachukuwe wakakae nayo kwao ikishapasuka watazika tu. Mwanaume angekufa napo wa upande wa kiumeni wadai mahari? Huu utaratibu wa mahari ndo chanzo cha wanaweke kujiona viumbe tofauti.
Lakini pia ndo maana hata wanadiriki kujiuza manake tunawanunua kihalali na kiharamu pia. Kwa nini mahari? Kwa nini nitoe hela kwa ajili ya mgono ambayo wafaidika ni sisi sote wawili?
 
Siyo sheria ya nchi, ila ni Mila na desturi ya baadhi ya makabila

Nchi haiongozwi na sheria za makabila.
Kwanza nchi hii inapinga vita ukabila.

Sheria za nchi ndiosingi wa jamii ya watanzania.

Kama hayo makabila yangehitaji sheria za makabila yao ziendelee ku- exist yangeunda nchi zao lakini kwa vile yamekubali interactions na kuunda taifa moja la Tanganyika.
Kisheria hizo sijui mila sijui desturi ni batili.
 
Unyakyusani nako hivohivo ila unatoa tu mahari na sio kufunga ndoa na maiti
 
Rahisi tu hawataki azikwe waambie wachukuwe wakakae nayo kwao ikishapasuka watazika tu. Mwanaume angekufa napo wa upande wa kiumeni wadai mahari? Huu utaratibu wa mahari ndo chanzo cha wanaweke kujiona viumbe tofauti.
Lakini pia ndo maana hata wanadiriki kujiuza manake tunawanunua kihalali na kiharamu pia. Kwa nini mahari? Kwa nini nitoe hela kwa ajili ya mgono ambayo wafaidika ni sisi sote wawili?
Kuna uchungu mke anauma alafu wao wanataka mahari tu
 
Nchi haiongozwi na sheria za makabila.
Kwanza nchi hii inapinga vita ukabila.

Sheria za nchi ndiosingi wa jamii ya watanzania.

Kama hayo makabila yangehitaji sheria za makabila yao ziendelee ku- exist yangeunda nchi zao lakini kwa vile yamekubali interactions na kuunda taifa moja la Tanganyika.
Kisheria hizo sijui mila sijui desturi ni batili.
Sheria za makabila zipo ila zinabidi zisiingiliane na sheria za nchi
 
Umenikumbusha...mama alivyofariki baba aliambiwa amalizie mahari ndiyo aruhusiwe kumzika mke wake.

Uzuri hakuwa mbishi nadhan alikuwa anajua .. aliwakabidhi wazee chao akaenda kumzika mke wake.
Hope hawakuleta vurugu
 
Kuna jamaa alifariki hajatoa mahari ya mkewe wakiwa na watoto watatu, ndugu walilipa.
 
Back
Top Bottom