Sasa kwa upande wa Tanzania kanda ya ziwa yote, makabila yanayokaa kwenye mikoa hiyo ambao kwanza ndio wenye population kubwa ya Tanzania, wanatumia udaga/makopa (unga wa mihogo) kama chakula chao kikuu pamoja na mchele sababu ya schemes za umwagiliaji kutoka kwenye ziwa Victoria kilimo cha mpunga kipo juu sana
Mahindi kule ni nadra sana kukuta yakilimwa, kanda ya ziwa wanaongoza kulima pamba, mpunga, mihogo, viazi vitamu na mazao mengine
Hii ni nzuri sababu inaleta options nyingi za vyakula na kutotegemea chakula aina moja tu.
Kwenye jedwali hapo unaweza kuona mihogo na mahindi yanaenda sambamba kwenye uzalishaji huku ndizi, viazi vitamu na mchele vikiwa sambamba havijaachana sana na mihogo na mahindi.
Unaweza sema mbona mahindi yapo juu lakini ujue kwamba mahindi tunayozalisha yanaenda kuuzwa nje ya nchi kwa wingi pamoja na kutumika kwenye matumizi yasio ya chakula kama kutengeneza vyakula vya mifugo
Lakini hayo mazao mengine kama mihogo, viazi, ndizi, mchele etc vyote vinatumika kama vyakula na haviuzwi nje kwa wingi, hivyo inapelekea kutoa taswira kwamba ndio vyakula vikuu vinavyotumika kwa wingi kuliko mahindi.