Gobret
JF-Expert Member
- Jun 11, 2010
- 320
- 88
Ukimya uliotanda juu ya maendeleo ya majadiliano ya makinikia yana mshindo Mkuu. Taarifa nilizopenyezewa na mtu ninayemwamini inasemekana jamaa wamekomaa kwelikweli na wanajua kupangua hoja. Inasemakana kuwa Hoja zetu zinazojikita kwenye tuhuma na siyo uhalisia zinasagwa na kuyeyushwa kama chuma.
Kana kwamba hiyo haitoshi hata maprofesa walioko kwenye kamati ya Makinikia kutoka Tanzania wameanza kuzilaumu kamati zilizoundwa kuchunguza Makinikia hayo kwani wanashindwa kupangua hoja za Mzungu katika majadiliano hayo ambayo yametawaliwa na rejea kutoka katika matokeo ya kamati mbili za Rais ambayo yalitiliwa shaka na wengi .
Ngoja tusubiri trilioni 300 na zaidi. Tanzania isipokuwa tajiri kwa pesa zote hizo tutakuwa tuna laana.
Duh! Mwana-adamu huyu alivyo mbeya we acha tu! Mbeya mbeya mpaka shida