Majaji na Mahakimu nyie hamuwezi kujitetea mahali popote dhidi ya mashambulizi ya Mawakili, tafadhali tumieni rungu lenu kwenye Sheria ya Mawakili

1979magufuli

New Member
Joined
Dec 6, 2024
Posts
2
Reaction score
2
Majaji wa Mahakama Kuu ni sehemu ya mamlaka ya nidhamu ya Wakili, Jaji anaweza kumchukulia hatua za kinidhamu Wakili kwa kukiuka sheria ya uwakili The Advocates Act, siku hizi Mawakili wakishindwa hoja mahakamani wanatoka nje na kulaumu mahakama kuwa imekosea ili wananchi tuamini kuwa mahakamani hakuna haki, this is quite wrong.

Tafadhali Mhe Jaji Mkuu, msivumulie mambo haya ya majaji kudhalilishwa na mawakili namna hii, leo nimemsikia Madeleka akiwalalamikia sana nyie, mshikisheni adabu kwa kuzingatia mamlaka mlizokuwa nazo kama ilivyokuwa kwa Mpare Mpoki, sasa hivi ameshika adabu yake.

Majaji lazima mheshimiwe na mawakili ambao ni maofisa wa mahakama, mtu kashindwa hoja mahakamani anajua nyie hamna platform ya kuongea kwenye public, yeye anakuja kuwashambulia nyie kwenye public akijua nyie hamna nafasi hiyo.Wakili ana awajibu kwa Mahakama kuheshimu mahakama, ana wajibu pia kwa Public, ana wajibu pia kwa taaluma yake, sasa kwanini Madeleka awe anawadhalilisha mnamkalia kimya? Nimeumia sana mimi.
 
ukiona wana mamlaka na wameshindwa kuitumia kumwajibisha ujue na wao wamekiuka sheria kwa manufaa yao hivyo kaa kwa kutulia wakubwa wakiparuana.
 
Tanzania hakuna mahakama Wala majaji Kuna kundi la wajinga huko kwenye mahakama.Nani asiye jua uchafu wa mahakama zetu hizi za kisutu ?Rostam Aziz alitoa ukweli mchungu kuhusu mahakama zetu,tukubali kuishi kwa yaliyo kweli.
 
Kwa katiba yetu ilibidi mahakama, Bunge na serikali kila mhimili uwe na nguvu lakini matokeo yake wote wamekua watetezi wa serikali, Cha kusikitisha zaidi anae wateua wa mhimili wa mahakama ni mtu uyo uyo kiongozi wa serikali tutegemee nini ?
 
ukiona wana mamlaka na wameshindwa kuitumia kumwajibisha ujue na wao wamekiuka sheria kwa manufaa yao hivyo kaa kwa kutulia wakubwa wakiparuana.
Hizi nafasi za kuteuliwa zinafanya watu washindwe kujitambua na kusimamia kile wanacho kiamini..njaa ni mbaya saana.
 
Mawakili wa serikali wanasemaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…