Majaliwa Shujaa wa ajali ya Precision Air ya Bukoba atinga Bungeni leo Novemba 11

Majaliwa Shujaa wa ajali ya Precision Air ya Bukoba atinga Bungeni leo Novemba 11

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Huyu hapa👇
B0C408BF-9F39-4395-9493-4DB8A7BED9BB.jpeg
 
Dogo ni fursa kwa wengine. Kinachoumiza hatoambulia chochote zaidi ya umaarufu wa muda tu.

Usistaajabu hiyo suite na viatu imepigiwa budget ya milioni kadhaa na hao wanaomsimamia.

Kuliko kumfanya kama sanamu la maonyesho ni bora either wangemrudisha shule kumpa elimu ya maana au wampe msingi wa uhakika wa maisha utakaomsaidia mbeleni, kama nyumba na kumboreshea fani yake ya uvuvi kama kupewa nyenzo za kisasa za taaluma yake. At least ana ujuzi na sector hiyo na wapo wengi wanaotajirika kwa kupitia uvuvi tu.

Wengi wanaongelea ajira kama msingi wa kumsaidia kusahau kwamba hiyo ajira hana taaluma nayo, elimu yake ni ndogo na wabongo ni watu wa zengwe.
Huko anakokwenda kuajiriwa atakutana na wakaanga sumu ambao wanaweza kumuona kama tishio kwao kupelekea kumfelisha na hapo atakimbilia kwa nani ikiwa trend yake itakuwa ishakwisha?

Hakuna aliyemuuliza kama yupo interested na huko walikompeleka, ni dhana tu kuwa anataka kuwa muokoaji na maamuzi ya wenye madaraka pasi kumshirikisha muhusika kupata maoni yake.
Kazi usiyoipenda ni sawa na adhabu.

Ni swala la muda, trend ikiisha watamtupa huko.
 
Back
Top Bottom