java script
Member
- Jan 31, 2017
- 57
- 37
kumjadili mtanzania
kuwa makin pia
makinikia nayatungia
mapini piaaaaaaa
Sent using Jamii Forums mobile app
kuwa makin pia
makinikia nayatungia
mapini piaaaaaaa
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
wewe ni chadema tu kama chadema wengine ambao hawataki kizuri kilichofanywa na serikali kijulikane kwa wananchi.kwa nini wanatangaza lakini? magaidi yanapata hasira za kulipa visasi wanapotangazwa wamepigwa.
kwa nini busara isitumike nyie watu?!!
Hongera jeshi la polisiWatu 13 wanaodaiwa kuwa wahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.
Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------
UPDATES..
Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
![]()
Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.
Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:
1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu mtawa
6. Rajabu Thomas roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
2.
Anti Riot Gun 38mm = 2

3.
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam
4.
MAGAZINI = 2

5.
Risasi za SMG 158

6.
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea
7.
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4

VIELELEZO VINGINE
8.
Pikipiki = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali
9.
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
10.
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe
Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.
b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.
Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.
Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.
Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula
Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.
Imetolewa na;
Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
Upo sahihi lakini umeleta siyo wakati muafaka na ulipaswa kuanza na appreciation kwanza kwa kazi nzuri waliyofanya wenzetu kwani kibiti haikaliki na waliopoteza maisha hawakuwa na makosaHell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....
Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......
Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.
Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Acha mzee, hivi unawajua askari wetu kweli? Tunataka kila wasemacho kiwe verified maana tukikumbuka matukio mengi ya nyuma tunapata mashaka.Tuache siasa kwenye mambo ya ustawi wa nchi. Hii agenda kama wapinzani wataendelea kuibeba wanavyotaka kuibeba wasije mlaumu mtu.
Sent using Jamii Forums mobile app
nasubiri orodha ya washirika wa kundi hili watakao fikishwa mahakamaniWatu 13 wanaodaiwa kuwa wahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.
Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------
UPDATES..
Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
![]()
Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.
Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.
Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.
Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:
1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu mtawa
6. Rajabu Thomas roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
2.
Anti Riot Gun 38mm = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
3.
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam
4.
MAGAZINI = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
5.
Risasi za SMG 158
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
6.
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea
7.
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani
VIELELEZO VINGINE
8.
Pikipiki = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali
9.
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi
10.
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe
Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti
Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:
a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.
b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.
c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.
Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.
Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.
Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula
Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.
Imetolewa na;
Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
Alafu wakienda kuwaonyesha walipo wenzao polisi wanawaua na hao watoataarifa! Hiyo imekaaje?!Wapo mkuu na ndio wanaosaidia kutoa taarifa za kuwapata wengine
Mbona sijaona mahali wameandika magaidi?Hahahaha!!! yaani magaidi yote 13 yalijeruhiwa kwanza halafu yakafia hospitali. Polisi naona washatugeuza misukule... Anyway kama ni kweli wameyaua pongezi ziwaendee... Ila bila picha nitabakia Thomaso tu...
Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Na hata vyombo vya habari vinalia viandike habari za huyo mnaemwita Bashite!Ndiyo maana hata Bashite analilia sana atangazwe na vyombo vya habari!!!!!!
Kwa majina ya dini yao, watakuwa wameishazikwa. La sivyo, nadhani wameishakabidhiwa kwa ndugu zao na wao watatutaarifu siku ya mazishi! Unataka uhudhurie? Tujulishe ukipata taarifa za maziko yao, tafadhali!Wanazikwa lini?
Naweza kuelewa unachomaanisha nini.Upo sahihi lakini umeleta siyo wakati muafaka na ulipaswa kuanza na appreciation kwanza kwa kazi nzuri waliyofanya wenzetu kwani kibiti haikaliki na waliopoteza maisha hawakuwa na makosa
zimetoka stoo hizo ni zile zile alizokuwa anaonyesha kova sasa siro sasa IGP akienekeza huu udaku asije akashangaa anashushwa na kulazwakwa hiyo, Wewe unaona hizo smg walikuwa wanapikia ugali
na umeambiwa walilushiana riss
Kuwafikisha mahakamani ni kupoteza muda, acha wauawe shwaini mbuzi pori haoHell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....
Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......
Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.
Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Wakisha kupa hiyo picha wewe itakusaidia nini? Unajua kuna vitu vingine hata ukivifikiria tu havina mantiki,
Kama una ndugu yako kapotea kapeleke taarifa police station.