Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

kwa nini wanatangaza lakini? magaidi yanapata hasira za kulipa visasi wanapotangazwa wamepigwa.

kwa nini busara isitumike nyie watu?!!
wewe ni chadema tu kama chadema wengine ambao hawataki kizuri kilichofanywa na serikali kijulikane kwa wananchi.
ulikupasa kujua kwamba, wananchi wa maeneo hayo wanahamu kubwa ya kutaka kujua jeshi la polisi limefikia wapi ktk kupambana na uhalifu ktk eneo hilo.
 
Watu 13 wanaodaiwa kuwa wahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------

UPDATES..

Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
1be4dcb1030cefec4c7b5919ad64b788.jpg

Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.

Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:

1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu mtawa
6. Rajabu Thomas roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.

Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

2.
Anti Riot Gun 38mm = 2

3.
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam

4.
MAGAZINI = 2

5.
Risasi za SMG 158

6.
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea

7.
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4

VIELELEZO VINGINE

8.
Pikipiki = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali

9.
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi

10.
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe

Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti

Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.

b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.

c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.

Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.

Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.

Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.

Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula

Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.

Imetolewa na;

Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
Hongera jeshi la polisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nimeona erythrocyte amecomment vizuri, lakini ni ukweli usiopingika kwamba, kuna wana chadema wengi hawajafurahia kabisa hii taarifa ya kazi nzuri ya jeshi la polisi ktk kukomesha uharifu nchini.
ni wakati sasa wa kujitafakari kama upo kwenye chama sahihi cha siasa ama la!
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Upo sahihi lakini umeleta siyo wakati muafaka na ulipaswa kuanza na appreciation kwanza kwa kazi nzuri waliyofanya wenzetu kwani kibiti haikaliki na waliopoteza maisha hawakuwa na makosa
 
Tuache siasa kwenye mambo ya ustawi wa nchi. Hii agenda kama wapinzani wataendelea kuibeba wanavyotaka kuibeba wasije mlaumu mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha mzee, hivi unawajua askari wetu kweli? Tunataka kila wasemacho kiwe verified maana tukikumbuka matukio mengi ya nyuma tunapata mashaka.
Hivi mkuu kile kiss cha wachimbaji Wa Kilombero na Zombe hakikukutoa machozi? Lakini hadithi yake ya mwanzo tulijikuta tukinpongeza Zombe kwa kazi nzuri.
Hapa hakuna itikadi za siasa Bali weledi na ukweli
 
Watu 13 wanaodaiwa kuwa wahalifu wameuawa na Askari wa Jeshi la Polisi. Watu hao wamekutwa na Bunduki nane, Pikipiki mbili pamoja na Begi moja la nguo.

Tukio hilo limetokea katika maeneo ya Tangibovu Kijiji cha Milaweni, huko Kibiti Mkoani Pwani.
View attachment 562464 View attachment 562465
View attachment 562467
View attachment 562466
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Chanzo: Jeshi la Polisi Tanzania(Ukurasa wa Twitter)
--------------

UPDATES..

Orodha ya Majina ya wahalifu 7 kati ya 13 waliouawa leo na Jeshi la Polisi eneo la Tangibovu ktk Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani
1be4dcb1030cefec4c7b5919ad64b788.jpg

Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu.

Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake.

Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam.

Ndugu Wanahabari
Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:

1. Hassani Ali Njame
2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani
3. Saidi Abdallah Kilindo
4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu
5. Issa Mohamed Mseketu mtawa
6. Rajabu Thomas roja
7. Mohamed Ally Kadude @Upolo
Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.

Ndugu Wanahabari
Vielelezo mbalimbali vilipatikana katika eneo la tukio, kama ifuatavyo:
S/N
KIELELEZO
UTAMBUZI
SILAHA, RISASI NA MABOMU
1.
SMG = 5
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

2.
Anti Riot Gun 38mm = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

3.
SAR = 1
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari Polisi huko Stakishari Jijini Dar es Salaam

4.
MAGAZINI = 2
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

5.
Risasi za SMG 158
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

6.
Bomu la kurusha kwa mkono = 1
Uchunguzi dhidi ya Bomu hilo unaendelea

7.
Mabomu ya kutuliza ghasia = 4
Mali ya Jeshi la Polisi tukio la kupora Silaha Askari huko Mtengeni – Jaribu Mpakani

VIELELEZO VINGINE

8.
Pikipiki = 2
Pikipiki hizi zilitumika kuwasafirisha wahalifu hawa kwenye utekelezaji wa matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali

9.
Vitenge na Nguo mbalimbali
Vitenge na nguo mbalimbali viliporwa baada ya kufanya tukio la kumuua Diwani wa Zamani wa Kibwiwi

10.
Begi = 1
Liliporwa baada ya kumuua Mtendaji wa Kijiji cha Mangwe

Ndugu Wanahabari
Kwa mujibu wa taarifa za utambuzi wa vielelezo vilivyopatikana eneo la tukio na utambuzi wa baadhi ya miili ya watuhumiwa waliofariki inaonyesha kuwa walishiriki matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Kuua OC CID na Watumishi 2 (Wawili) wa Idara ya Maliasili katika tukio la Jaribu Mpakani – Wilaya Kibiti
2. Kuua Askari Polisi 8 (Nane) katika tukio la Mkengeni – Wilayani Kibiti
3. Kuua Trafiki 2 (Wawili) katika tukio la Bungu “B” – Wilaya ya Kibiti
4. Kumuua Diwani wa Zamani CCM katika tukio la Kibwibwi – Wilaya ya Kibiti
5. Kuua Afisa Mtendaji, Mwenyekiti wa Mtaa na Mkulima katika tukio la Kijiji cha Mangwi – Wilaya ya Kibiti

Ndugu Wanahabari
Wito wangu kwa Wananchi ni kuhusu mambo muhimu yafuatayo:

a. Wananchi wote nchini kuondoa hofu ya kwamba eneo hili si salama. Nawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi na kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu. Aidha nawaomba wananchi kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapohisi kuna jambo lolote wanalolitilia mashaka.

b. Natoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Pwani, hususani maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri, kuendelea na shughuli zao mbalimbali za kujiletea maendeleo. Nawasihi kwa dhati kabisa waendelee kutupatia taarifa zitakazosaidia kumaliza kabisa uhalifu kwenye eneo hili. Nitumie fursa hii kuwashukuru sana wananchi wa maeneo ya Mkuranga, Kibiti na Ikwiriri kwa ushirikiano mnaotupatia ambao umesaidia sana kuwadhibiti wahalifu.

c. Mamlaka za Hospitali, Zahanati, Vituo vya Afya, Maabara za Afya ya Binadamu na Maduka ya Kuuza Dawa za kutibu Binadamu zijiepushe na utaratibu wa kutoa matibabu kienyeji au kificho kwa watu waliojeruhiwa bila kufuata taratibu za kisheria ikiwemo kupata taarifa ya Polisi “kupitia Fomu maalum ya kuruhusu matibabu (maarufu kama PF. 3)”. Wahalifu wakijeruhiwa ni lazima watafute matibabu.

Kwa hiyo idara hizi ni muhimu sana kutoa ushirikiano ili kutuwezesha kuwakamata watuhumiwa maana baadhi yao wamekutwa na majeraha sehemu mbalimbali za miili yao na walikuwa wanaendelea kujitibia kwa kificho kwa kutumia dawa za hospitali.

Natoa wito kwa Mamlaka hizo kutoa taarifa mara moja kwa Jeshi la Polisi wanapoona ama kumbaini mtu ambaye ataonekana kuwa na majeraha na anatafuta tiba bila ya kufuata taratibu.

Ndugu Wanahabari
Napenda kuujulisha Umma kwamba wapo baadhi ya Watuhumiwa, Wafadhili na Washirika wa Uhalifu na Wahalifu wa ujambazi maeneo haya ambao bado hawajakamatwa. Jambo la kufurahisha ni kwamba taarifa zao zipo kwa Jeshi la Polisi nchini na zinaendelea kufanyiwa kazi ili waweze kukamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa Sheria mara moja.

Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula

Ndugu Wanahabari
Nimalizie kwa kusema kwamba uhalifu kwenye eneo hili ni suala la muda mfupi. Na tunaendelea vizuri sana. Hali ya usalama imeimarika sana eneo hili. Nazidi kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuliunga mkono Jeshi la Polisi ili kufikia malengo yake ya kuzuia, kubambana na kutanzua uhalifu nchini.

Imetolewa na;

Simon Nyakoro Sirro
Inspekta Jenerali wa Polisi
IKWIRIRI
10.08.2017
nasubiri orodha ya washirika wa kundi hili watakao fikishwa mahakamani
 
Wapo mkuu na ndio wanaosaidia kutoa taarifa za kuwapata wengine
Alafu wakienda kuwaonyesha walipo wenzao polisi wanawaua na hao watoataarifa! Hiyo imekaaje?!

Kwanini mara zote polisi wakienda na mtoa taarifa/shahidi ambaye wanamshikilia tayari kuwaonyesha walipo wengine, wakifika naye huko porini wanamuua?! Kwanini?!
 
Hahahaha!!! yaani magaidi yote 13 yalijeruhiwa kwanza halafu yakafia hospitali. Polisi naona washatugeuza misukule... Anyway kama ni kweli wameyaua pongezi ziwaendee... Ila bila picha nitabakia Thomaso tu...

Sent from my Nokia-tochi using JamiiForums mobile app
Mbona sijaona mahali wameandika magaidi?
 
Upo sahihi lakini umeleta siyo wakati muafaka na ulipaswa kuanza na appreciation kwanza kwa kazi nzuri waliyofanya wenzetu kwani kibiti haikaliki na waliopoteza maisha hawakuwa na makosa
Naweza kuelewa unachomaanisha nini.
Siasa nzuri ni kujitofautisha na wao.

Mandela wanamuenzi sababu he was wise enough to know the difference.

After all, kuna wakati they really do their work

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ningekua mkuu wa kikosi nadhani,ningeomba wakamatwe kadhaa,wahojiwe kule kule site af tunawazawadia risasi za vichwa then tunachanganya na wengine waliokufa......hamna kuwaonea huruma hao pimbi.
 
Mura weitu amangana,Nyakoro hongera sanasana kwa kazi nzuri sana unayofanya tokea ukabidhiwe kuongoza Jeshi Letu.
 
Yaani kati ya watu 13 waliouwawa hakuna hata Police aliyejeruhiwa wala kupoteya maisha hii ya kweli au ndio yale yale ya siku zote then baadae uhalifu uko pale pale,ila kama ni kweli itakuwa safi sana.
 
Mbona Polisi haisemi na wao wameuawa wangapi?? jahiwezekani watu 13 wenye siraha wafe kizembe hivyo, lazima na wao waliwatungua kadhaa...Polisi iache sanaa.
 
kwa hiyo, Wewe unaona hizo smg walikuwa wanapikia ugali
na umeambiwa walilushiana riss
zimetoka stoo hizo ni zile zile alizokuwa anaonyesha kova sasa siro sasa IGP akienekeza huu udaku asije akashangaa anashushwa na kulazwa
 
Mpaka watakapo angalia na kuielewa movie ya snipper ndio wataona kuwa hawako sahihi sana.
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
Kuwafikisha mahakamani ni kupoteza muda, acha wauawe shwaini mbuzi pori hao
 
Wakisha kupa hiyo picha wewe itakusaidia nini? Unajua kuna vitu vingine hata ukivifikiria tu havina mantiki,

Kama una ndugu yako kapotea kapeleke taarifa police station.

Picha ni kitu muhimu sana usijifanye huelewi labda tukiona picha tunaweza kuwatambua na kujua marafiki zao wengine tukatoa msaada kwenye vyombo vya ulinzi kwani hizo picha za bunduki na mabomu zinatudaidia nini
 
Back
Top Bottom