Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

kwa nini wanatangaza lakini? magaidi yanapata hasira za kulipa visasi wanapotangazwa wamepigwa.

kwa nini busara isitumike nyie watu?!!
kwa sababu watu kama nyinyi mpo wengi sana ,hamkawii kuuliza "mbona kibiti kimya?"

lazima tulipe kodi
 
Hivi ulisha wahi tembelea Kibiti wewe!!
Hawa watu hujificha kwenye vichaka vikubwa vikubwa
pia ukumbuke kuwa Pwani inaeneo kubwa sana lenye misitu misitu

Sasa hapa ndio umetoa ufafanuzi au ni kukoroga tu? Mlio wa risasi unazuiwa kusikika kwa sababu ya msitu mkubwa? Hatukatai hili igizo la kuuliwa hao majambazi, lakini toka wameanza hilo zoezi majambazi, yote yameuwawa hakuna hata mmoja aliyekamatwa akiwa hai asaidie uchunguzi? Kwa jinsi yale mauaji yalivyokuwa yanafanyika huwezi kuniambia eti hao majambazi wanauwawa tu, tena wakiwa na smg na wala tone la damu lasionekane wala polisi kujeruhiwa. Haya bana kama mmetuona wajinga wa hivyo.
 
Hell no. .that shouldn't be the way!
Washukiwa hawatakiwi kuuwawa hata kidogo.....

Kazi ya police ni ku enforce law and order na sio judgement......

Tukiwaachia police uhuru huo... Tumekwisha.

Hili ni kwa Usalama wetu sote, Hakuna Chama Wala Ushabiki kwenye mambo kama haya......
wewe umeona picha hizo ni silaha sio matoi hayo sasa unategemea watu kama hao utawakamataje au utalenga miguu wakati yeye target yake ni kukuuwa ili achukue silaha vitu vingine si lazima upinge kila kitu aisee....
 
Je, kulikuwa kuna ulazima wa kuwaua? Ingependeza kama wengine wakamatwe wakiwa hai ili kulisaidia jeshi la polisi katika upelelezi.
Tatizo ukiachiwa na uhai wao, watatetewa mahakamani na watashinda. Wakishinda ndipo wataendeleza ugaidi. Dawa yake ni kuwapoteza ili wenzao waongope. Nadhani kabla ya hukumu ya kipolisi wanakuwa washawahoji na kujua mtandao. Hii ni tekniki inayotumiwa na magaidi pia
 
Tunaudhika askari police na raia wanapouawa na majambazi. Lakini mara kadhaa kuna matukio ya police kubambika watu kesi. Jana tu Mwanza imenyesha mvua ya risasi za police. Siku zote ni nadra police kutaja serial number ya siraha wanazoshika kwa wahalifu. Kujua ukweli walio uawa ni majambazi tunaliacha mikononi mwa police.
 
Picha ziwekwe!Hivi kwanini siku zote tunasikia wameuwawa?Hakuna majeruhi hata mmoja kati ya hao 13?
Kuna tatizo sehemu!!
 
Wanapeleka watu kule na kuwapiga risasi na kuwawekea bunduki na silaha halafu wanajitekenya kuwa tumeua majambazi kibiti. Ndio tatizo la afrima uongo mwingi kwa kuogopa kufukuzwa kazi. Kwani unafukuzwa kazi pasipo hata kuchunguza kosa. Hakuna majambazi ambao tunaambiwa ni waliobobea na wamepata mafunzo nje leo hii wakae pmj. Watu wanapelekwa kibiti wanauwawa then polisi wanasingizia majambazi wa kibiti. Tusubiri muda utasema ndio polisi tanzania
Haya sasa mbona kibiti kunetuliatulia kama wanao uwawa sio majambazi/wahusika!? au hata wake waliokuwa wanauwawa ilikuwa naigizo tu ya serikali?!
 
wahalifu 13 wauawa na Polisi huko kibiti, watelekeza silaha 8, pikipiki 2 angalia picha hapo chini:-
Hapa ndio nashindwa kuelewa, wahalifu 13 wauwawa na kutelekeza silaha 8. Hao walio uwawa ndio wametelekeza silaha au kuna wengine wamekimbia? Waliouwawa ni kina nani kwa majina?
 
Safiiiii!! Good job!!, Well done kwa polisi wetu..!!
 
wewe umeona picha hizo ni silaha sio matoi hayo sasa unategemea watu kama hao utawakamataje au utalenga miguu wakati yeye target yake ni kukuuwa ili achukue silaha vitu vingine si lazima upinge kila kitu aisee....
Unakosea Sana.
Hivi unaamini kabisa Polisi waliwauwa wote kwa mpigo na wote walikuwa na silaha hizo nane?
 
Back
Top Bottom