Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Majambazi 13 wauawa Kibiti, wakutwa na Bunduki 8 pamoja na Pikipiki 2

Halafu hakuna askari aliyejeruhiwa huku wakisema walikuwa wakijibizana kwa risasi, INA maana hao watu walikuwa wakipiga risasi hewani, afu ilikuwa usiku waliwaonaje wote 13? Hao waliouwawa walikuwa wachoma mkaa tu au wavamizi wa misitu hakuna cha majambazi wala nini, jambazi haishi maisha ya kimasikini namna hiyo, kuishi kwenye Nyumba ya nyasi na udongo...huyu IGP anatufanyia usanii kwa vile naye ni mpenda kiki kwa pikipiki.

Hayo majina yawekwe hadharani na ili yachambuliwe wasifu wao na wananchi wa eneo husika kama ni kweli walikuwa ni majambazi...

Sent using Jamii Forums mobile app
Wape majina unayotaka ila wamekamatwa na vidhibiti walivyowaibia waliowauwa, na lengo la press conference ilikua ni kiwaelezea wahalifu sio mapolisi ulitaka wakupe kila kilichojiri ikusaidie nini? Taarifa zinatolewa kwa mujibu wa utoaji wa taarifa za kipolisi usifikiri wanaropoka tu kama unavyoropoka hapa visivyokua na mantiki.
 
Hakuna majeruhi/survivor hata mmoja tu asaidie kueleza kwa nini walikuwa (allegedly) wanavamia na kuua viongozi wa CCM tu? Kwanini tumewaua wote? Kwanini hata mmoja tu hakupigwa shaba ya mguuni badala ya kifuani au kichwani?
Hujasoma vizuri. Wamesema aliyewapeleka eneo la tukio alikuwa mshukiwa. Hivyo wanao wengi wa kuwapa habari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natoa wito kwa wananchi ambao wanawafahamu watuhumiwa wafuatao kutoa taarifa katika kituo chochote cha Polisi ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria. Picha za watuhumiwa hao zitasambazwa kote nchini ili iwe rahisi kuwabaini. Majina ya watuhumiwa hao ni:
i.Anafi Rashid Kapelo @ Abuu Mariam
ii. Hassan Haruna Kyakalewa @ Abuu Salma @ Shujaa @ Dokta
iii. Haji Ulatule
iv. Shekhe Hassan Nasri Mzuzuri
v. Rashid Mtutula
cc: Ritz, FaizaFoxy
 
kama mtuhumiwa kamtaja Juma kama mshirika wake ulitaka waongeze na John kuleta balance??? Hicho kichwa ulipewa ukitumie kwa mambo mengi sio kushikilia macho tu yakusaidie kutazama magari wakat wa kuvuka barabara
Hili la majna kuwa upnde mmoja ni hoja ya msingi wala sio la kupepesa macho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera Jeshi la Polisi kwa muda wa mwezi mmoja sijasikia kiongozi ama askari akiuwawa.
Hao wauaji mliwapa nafasi wajisalimishe lakini hawakujua mkono wa serikali ni mrefu.
Hongera zaidi kwa kamanda Sirro umeonyesha kuwa wewe ni kiongozi wa kukaa ofisini ni kiongozi unaenda personal kwenye tukio.
Tanzania salama ni muhimu.
 
Hiyo taarifa NAIACHA kama ILIVYO,
Kuna siku huyu huyu alituambia alipokuwa KAGERA , kwamba hao wahalifu walikuwa wakipanga mipango yao kwenye NYUMBA ZA KUABUDIA.

Lakini kwenye HIZI RIPOTI ZA HUKU KIBITI sijasikia hata siku moja akisema "NYUMBA ZA KUABUDIA" akiwa yuko KIBITI.
Ndo mara ya kwanza kuwasikia kuwa "WANAO WAFADHILI WAHALIFU"
(muelewe hao wataitwa MAGAIDI soon sasa hivi bado wanaona AIBU kutangaza ndo maana wanaita WAHALIFU, sijawahi kusikia siku za nyuma polisi wakitafuta wafadhili wa MAJAMBAZI,)

Yaani wanachokifanya wanaingiza kidogo kauhusiano ka UGAIDI then wanarudi kwenye UHALIFU , Then UJAMBAZI.

Ndio maana pia kuna mali za wizi VITENGE nk

Ina maana jukumu la kujichanganya ni letu wakimaliza niaminini nawaambia kuna kitu kitaitwa UGAIDI TANZANIA, Na hii HUWA inasindikzwa na mapambano ya kupinga UGAIDI kwa nguvu zote.

HAYA MAMBO NI HADITHI ZILE ZILE WAHUSIKA TOFAUTI TU.
 
Nashauri uchunguzi wa kina ufanyike, Haya majina Abuu yanaashiria nini na Mariam na Salma yanaashiria nini pia

Historia yao ichunguzwe kwa kina kubaini mahusiano yao na waliouawa na watu wengine baki walioko mtaani, hii itasaidia kubaini mambo mengine outside the box

Abuu Maryam na Abuu Salma maanake Baba Maryam na Baba Salma respectively.
 
Sasa kama kuna mpaka hand grunets kuna nini cha ziada? Wameua imetosha

Sent using Jamii Forums mobile app
Una uhakika hizo grunets zimekutwa huko kwa hao majambawazi? mkuu wote sisi hatupendi kabisa tabia za hao wauwaji. Lakini pia tabia ya kutoa taarifa za ajabu ajabu ili kulinda ajira hazifai na hazileti imani juu ya usalama wetu.
Ngoja nikupe kisa kimoja. Miaka kadhaa huko nyuma kama sikosei RPC akiwa huyo bwana mkubwa kabisa wa sasa au yule aliyekuja mpokea, aliitisha press na akawaonyesha silaha zilizo kamatwa kwenye matukio ya ujambazi. Bahati mbaya kwake mwandishi mmoja mtukutu akachukua namba za moja ya silaha zile zilizo onyeshwa. Cha kushangaza ni kuwa baada ya muda kukatokea tukio linguine na RPC yuleyule akaitisha press na moja ya silaha alizoonyesha pale ni ile ambayo mwandishi alichukua namba yake. Mwandishi akahoji iweje silaha iliyokwisha kamatwa katika tukio la miezi michache nyuma leo tena inakamatwa kwenye tukio lingine la uhalifu?
Ile press conference iliharibikia hapohapo. Nadhani umenielewa. Kuna mambo yanaendelea kwa siri ili kulinda kazi za watu bila kujali maisha ya wengine.
 
Hao waliouawa tayari kuna wengine walitoa ushirikiano hao wakapatwa ktk maficho yao!
Wauliwe tu tena ingependeza wawe wanawakata tu makoromea na kuacha wakifa kama kuku aliyekatwa shingo akaachiwa!
Kama kuna wenzao bado wapo siku wakitaitiwa na polisi nabidi wajisalimishe kuepusha mauti.
 
Wanapeleka watu kule na kuwapiga risasi na kuwawekea bunduki na silaha halafu wanajitekenya kuwa tumeua majambazi kibiti. Ndio tatizo la afrima uongo mwingi kwa kuogopa kufukuzwa kazi. Kwani unafukuzwa kazi pasipo hata kuchunguza kosa. Hakuna majambazi ambao tunaambiwa ni waliobobea na wamepata mafunzo nje leo hii wakae pmj. Watu wanapelekwa kibiti wanauwawa then polisi wanasingizia majambazi wa kibiti. Tusubiri muda utasema ndio polisi tanzania
inaonekana unajua sana
 
Back
Top Bottom