Majanga ya Asili: Tukafanye utafiti kwa Wahadzabe na wanaofanana nao ili tufahamu jinsi wanavyotambua majanga haya kabla hayajatokea?

Majanga ya Asili: Tukafanye utafiti kwa Wahadzabe na wanaofanana nao ili tufahamu jinsi wanavyotambua majanga haya kabla hayajatokea?

Mkuu,kuna vitu vingine mtu huupuuza na matokeo yake huleta maafa.
Hayayepukiki,lakini kuna uwezekano wa kupunguzwa. Kupunguzwa kwake, ni kuingia gharama na kukubali hasara.
Pichani,ni makazi ya watu. Jiulize, huyo mtu ana miaka mingapi hapo mbele?
Katumia gharama kujenga,lakini ameambulia hasara. Kisa tu,akae mjini.
Jiulize ikinyesha usiku,au kaacha tu watoto! Matokeo yake,serikali inalaumiwa! Kwenye video hapo,utaona mtu kaanika nguo. Hajali,liwalo na liwe.
Kwenye swala la ujenzi,kungekuwep masterplan ya wilaya,ijulikane wapi panafaa ujenzi na wapi hapafai.
Hao watu wana uwezo asilia kugundua,ila ni huko kwao
 

Attachments

  • IMG_20231202_172927_544.jpg
    IMG_20231202_172927_544.jpg
    1,005 KB · Views: 4
  • VID_20231202_173213.mp4
    30.6 MB
  • IMG_20231202_173344_913.jpg
    IMG_20231202_173344_913.jpg
    1.3 MB · Views: 4
  • IMG_20231113_172456_230.jpg
    IMG_20231113_172456_230.jpg
    1.4 MB · Views: 4
Pascal Mayalla
Wewe ni mwandishi mzuri sana, nakushauri uende uhazabeni ukafanye utafiti.
Ukitaka ufadhili useme mapema nitakuunga na wafadhili.
Mkuu Glenn , asante hoja imepokelewa, na ushauri umekubalika, japo mimi sio researcher ila mwandishi yoyote wa habari wa IJ, anaweza kufanya social research yoyote as long as sio scientific research!. Ngoja niifanyie kazi.
P
 
A
Wanasema ulisikika mlipuko mkubwa wakati wa usiku, mlipuko uliodhaniwa kuwa wa volcano, lakini mawe tunayoambiwa yaliporomoka kutoka mlimani yalisababishwa na maji ya mvua iliyonyesha.

Sasa hapo kuna connection ipi kati ya mvua na volcano ya usiku, au volcano pia inaweza kuleta mvua?

Naona hapa lazima wapatikane wanasayansi kututhibitishia hili, na sio hao wabarbaig na wenzao.

By the way sidhani kama kukimbia hatari ni suala linalohitaji kuhusishwa na makabila fulani, mimi au wewe tunapohisi hali ya hatari kwa sababu ya tukio lisilo la kawaida, kukimbia ni jambo la kawaida.

Tatizo naloliona hapo, inawezekana wajanja wa mjini hawakukimbia kwasababu tu ya ujanja wao, na hao jamaa zangu wakakimbia kwasababu tu ya ushamba wao, matokeo yake ushamba wao ukawaokoa.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
ahaaaaaaa
 
Serikali haijatangaza Janga ,Huwa Kuna utaratibu
Kwa hiyo wafe wangapi ndo liwe janga? Waumie wangapi ndo tujue ni janga?
Wangapi wakose makazi ndo serikali itangaze ni janga?
Kama siyo janga, je walijitakia??
Tutajifunza lini kuthamini uhai na maisha ya wenzetu??
 
Wanabodi,

Kama kawa kila nipatapo fursa huja na kwa Maslahi ya Taifa. Leo ni kuhusu Natural Disasters: Jee Tuwafanyie Research watu wa makabila ya Wabarbaig, Wahadzabe, Wataturu, Wasandawe na Watindinga, huwa wanajuaje kutatokea natural disasters na kukimbia eneo hilo kabla ya majanga hayajatokea?

Japo wazungu wanasemekana ni wataalamu sana wa sayansi lakini hawawezi ku detect tetemeko la ardhi kabla halijatokea, au mlipuko wa volcano, lakini wanyama wa porini wana uwezo wa kudetect na makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana uwezo huo!

Mlima Hanang uko kwenye safu ya milima ya volcanic mountains kama Oldonyo Lengai, usikute una volcano hai!. Enzi zile Oldonyo Lengai, ulipofuka moshi mzito, na majivu yale yaliwaathiri wanyama na mifugo, ya kufungwa ndio iliathirika kutokana na kufungiwa lakini wanyama wa porini wao walijua na walikimbia kabla.

Watu wa makabila ya wawindaji wa asili, Wataturu, Wasandawi, Wabarbaig, Wahadzabe na Watindiga, pia wana natural seismology intelligence hivyo wana uwezo huo kwa kuwasikia wanyama pori, wakiwaona wanakimbia kukimbilia direction fulani, nao hukimbia, na baada ya kukimbia ndipo huku nyuma, hutokea la kutokea.

Tusiwategemee sana Wazungu na research zao, na vifaa vyao, tufanye utafiti wa haya makabila ya wawindaji wa asili wanatumia nini na viashiria gani kuyakimbia maeneo kabla majanga hayajatokea!.

Kwa mujibu wa mashuhuda, wanasema walisikia mlipuko kama wa volcano usiku wa manane na hali kama ya tetemeko la ardhi, ndipo ikanyesha mvua kubwa mlima Katesh na kusababisha maporomoko ya udongo yaliyosombwa na mafuriko na kuzisomba nyumba za wakazi wa chini ya mlima ambapo watu zaidi ya 50 wamefariki dunia, mamia kujeruhiwa na mamia wengine hawana makazi wala mahali pa kuishi.

Mashuhuda hao wamesema mpaka kunakucha walikuwa wanaona mvuke ukipaa juu kutoka mlima Hanang.

Ikifanywa research ya waathirika wa janga hili la mafuriko ya Mlima Katesh unaweza kukuta, wale wanaioshi milimani na wanyama wa porini waliisha kimbia usiku usiku kabla ya janga hilo!

Na kufuatia imani za kiasili, (siiti za kishirikina), kuna watu wana nguvu na uwezo wa ajabu ama kusababisha majanga ama ku control majanga. Mkama Rumanyika wa Karagwe, alikuwa akiwapiga maadui zake kwa mvua ya mawe na kumrarua kiongozi wao kwa kumpiga radi.

Kuna watu wanapaa usiku kwa ungo, kuna watu wanapanda fisi anapaa hewani, kuna watu wanatumia nyoka kulinda mashamba yao, kuna watu wanatumia mazindiko fulani, ukiingia kuiba, unamangamanga mpaka asubuhi unakutwa.

Hizi zote ni sayasi za kiasili za Kiafrika, zikifanyiwa research, zitalisaidia sana taifa letu. Mnaonaje kama tutafanya research kwenye hili?

Natoa tena pole kwa wahanga wa janga hili na nimemsikia Mama, amekatisha ziara ya Dubai kurejea nyumbani kuimarisha juhudi za uokozi na utengemano.

Enzi za JPM kulipotokea Tetemeko la ardhi Bukoba, JPM aliahirisha ziara ya Zambia tukitegemea angeibukia Bukoba lakini kilichotokea tukabaki kuulizana Mhe. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli, "Sema Neno Moja Tuu, na Roho Zetu Zitapona!"

Mungu inusuru Hanang,
Mungu Ibariki Tanzania.

Paskali.
Update

Mkuu Glenn , asante hoja imepokelewa, na ushauri umekubalika, japo mimi sio researcher ila mwandishi yoyote wa habari wa IJ, anaweza kufanya social research yoyote as long as sio scientific research!. Ngoja niifanyie kazi.
P
paschali Kila binadamu ni researcher tofauti ni kwenye methodology. Na waandishi wa habari wazuri ni ma-researcher wazuri
 
Situation Iko controlled
How!?
Mbona wanazungumzia kuunda time ya wataalamu wa miamba?
Mbona mafuriko ya Mozambique na tetemeko Ugiriki walijiongeza?
Anyway subiria siku ya mazishi ya alaiki utaona hao viongozi wako watakavyo uza sura zao na matamko yao ya kuwahakikishia ccm haitoruhusu hilo janga lijirudie!
Shame!
 
Wabarbaig wepi unawazungumzia, Pale Hanang ndio kwao na ndio hao wamekufa na kaya zaidi ya 28 hazijulikani zilipo, bila shaka wamefukiwa na matope. Hali ya Hanang ni mbaya kuliko viongozi wanavyoeleza. Vitongozi vitatu vimefukiwa. Nenda kaangalie kwenye ripoti ya sensa ya mwaka jana 2022, kaangalie kijiji cha Gendabi ina watu wangapi. Watu ambao wamefukiwa ni wengi sana.

Aisee
 
Nyoka, jongoo na wadudu wengine watembeao kwa tumbo pamoja na baadhi ya mijusi ni wanyama wenye uwezo wa kudetect majanga, hata tetemeko la ardhi

Wanyama hawa wana tabia ya kuhama siku 3 mpaka 5 kabla ya kutokea kwa majanga haya

Mababu zetu waliexperience hicho na hata hizi jamii za Wawindaji pia
 
Upo sahihi sana Paschal, indigenous knowledge ni muhimu sana kwenye kutafuta majawabu ya hizi natural disasters.
 
Nnaangaika na kinachonipa ugali mezani hayo mengine angaiken nayo ninyi majiniaz
Wewe msssssenge innocent dependent unapenda kuongea uongo kisa tu dayamondi anakutatua marinda. Wewe matterco lokole tunakujua vizuri shoga wewe mpigwa miti
 
Back
Top Bottom